August 31, 2009

"UNSITTING A STRONGMAN"

Wadau si vibaya siku moja moja kuwashirikisha kile tukipatacho katika nyumba za ibada kama nilipopata bahati ya kuuzulia Ibada ya jana katika Kanisa la Ufufuo na Uzima pale Ubungo, na ujumbe wa jana ulikuwa "Unsitting a Strongman" likitoka Isaya 49: 24-26 Ni namna gani shetani anaweza kukalia baraka au kuinuliwa kwa wateule na kutaka kuwatala kwa kitambo kidogo (kwani hana uwezo wala kibali cha kuwatala wateule milele) na kukutesa kwa kitambo hicho lakini pale unapotambua kuwa we ni nani na kumtambua shetani na nguvu zake, ndipo uwa rahisi kwako na kwa kutumia jina lipitalo majina yote la YESU waweza kujinasua na mbinu na mitego ya mwovu shetani. Ndipo pale yule aliyedhani amemfunga mlango ujikuta akifungua si tu na madirisha bali na paa pia. Amen Soma huo mstari wa mwisho uone vile BWANA anaenda kutenda kwa watesi wako, si wewe bali ni yeye asemaye maneno haya, hayo yatoka kinywani mwa Bwana wa Majeshi, je wataka aseme nini tena? Ubarikiwe sana mpaka ushangae weye unayeteswa na kudhulumiwa sasa maana uponyaji wako huu karibu.
24 Can plunder be taken from warriors, or captives rescued from the fierce [b] ? 25 But this is what the LORD says: "Yes, captives will be taken from warriors, and plunder retrieved from the fierce; I will contend with those who contend with you, and your children I will save. 26 I will make your oppressors eat their own flesh; they will be drunk on their own blood, as with wine. Then all mankind will know that I, the LORD, am your Savior, your Redeemer, the Mighty One of Jacob."

Kashehe la umeme ni OPPORTUNITY pia, Tanesco mpooooo???

The perennial electricity shortage in East Africa should be considered an opportunity for exploiting other energy sources that are abundant in the region, a power expert has said. Speaking recently in Dar es Salaam, the executive secretary of the East African Power Pool (EAPP) project, Mr Jasper Oduor, said the use of renewable sources in the region was long overdue.
GA_googleFillSlot( "AllAfrica_Story_InsetA" ); He said East Africa had abundant sunshine and good weather that would viably support investment in power and energy provision, adding that scarcity was the mother of opportunities and a source of progress.
"In an era that emphasises clean energy, renewable energy sources such solar, wind and hydro provide opportunities in the provision of electricity power necessary to drive economies and improve the wellbeing of citizens in the region.
"Beneath our feet is also the vast potential of geothermal energy, which is another renewable source," Mr Oduor added.

Dr Shein yuko Geneva

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Gavana mkuu wa Geneva David Hiler katika chumba maalum cha kupumzikia wageni alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa mjini Geneva leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano mkuu wa tatu wa kimataifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa Duniani unaotarajiwa kuanza kesho mjini Geneva. Katikati Mama Mwanamwema Shein.

JK atua Tripoli

Rais JK akipokewa na waziri wa kilimo na mifugo wa Jamhuri ya Libya Aboubakari Mansoor mara tu baada ya kuiwasiri kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi jijini Tripoli , rais yuko libya kuhudhuria kikao cha siku moja cha wakuu wa nchi za Afrika kinachofanyika leo 31 .8.09 kuzungumzia masuala ya usalama barani afrika na baadaye kuhudhuria sherehe za miaka 40 ya utawala wa Rais Muammar Gadafi.

August 27, 2009

Msitufundishe kazi - Pengo

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema maaskofu wasifundishwe namna ya kufikisha kazi ya Mungu na kufikisha ujumbe wao kwa waumini.
Kauli hiyo ya Pengo ambayo aliitoa mbele ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, pasipo kutaja waraka, imetolewa baada ya waraka uliotolewa na kanisa hilo kuzua mjadala mkali nchini, ukihusisha watu wa kada mbalimbali. Mjadala wa hoja hiyo pia ulifika katika Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM ambako ulijadiliwa na kutolewa maazimo.
Katika maazimio hayo, NEC iliwataka viongozi wa Serikali na Kanisa Katoliki kukutana, ili kupata ufumbuzi wa mzozo wa waraka huo ambao unataka wananchi wachague viongozi waadilifu wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani.
Mbali na NEC, wakati akijibu mwaswali ya papo kwa papo bungeni hivi karibuni, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema ni vema uongozi wa kanisa hilo ukapeleka waraka huo serikalini, ili iweze kusambaza kwa wananchi, badala ya utaratibu wa sasa unaotoa mwanya kwa kila dhehebu kujiandikia na kusambaza nyaraka...................
source: Mwananchi

August 26, 2009

Askofu Mkuu Anthony Mayala azikwa

Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwishom kwa mwili wa Marehemu Askofu Mkuu Anthony Mayalla wakati wa ibada ya mazishi huko Mwanza mapema leo.

JK apokea hati za utambulisho

Rais JK akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi mteule wa uholanzi nchini mheshimiwa Dr. Kuindert Adriaan Koekkoek.

Mafua ya ndege yapigwa jeki.

Katibu Mkuu wa Jumaiya ya Afrika mashariki Balozi Juma Mwapachu (kushoto) akipokea funguo na nyaraka za magari saba kutoka kwa Meneja kampuni ya CMC tawi la Arusha Suresh Nathwani (kulia) jana katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya AICC.Magari hayo yametolewa kama msaada na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ajili ya mradi wa kuthibiti ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege katika nchi wananchama wa jumuiya hiyo

Mtoto wa Mkulima na Zawadi ya Sarafu

Mtoto wa Mkulima Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kitazama sarafu ya Australia iliyotengenezwa maalumu kama pambo ambayo alikabibidhiwa na Waziri wa Afya wa Australia , Kim Desmond Hames baada ya mazungumzo ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar leo

Mazishi ya pamoja ya Wanafunzi 12 wa Sule ya Idodi katika picha

Waziri wa Elimu Prof Jumanne Maghembe akiweka shada maua. Mmoja wa wafiwa akisaidiwa mara baada ya kushuhudia mazishi ya mwanae Mbunge wa Isimani ambako ndiko iliko shule ya Idodi na Mkuu wa Mkoa wa Dar William Lukuvi akiweka shada. Familia ikiomba mbele ya kabuli la pamoja. Picha kwa hisani ya mdau Francis Godwin

August 25, 2009

Mishahara ya Waheshimiwa JUU

SERIKALI imewaongezea mishahara viongozi wa kisiasa, majaji, wakuu wa mikoa na wilaya kuanzia Julai mwaka huu, huku jaji mkuu na spika wakiongezewa maradufu.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mshahara wa jaji mkuu na spika, ambao ni viongozi wa mihimili mikuu miwili ya nchi, umepanda kutoka Sh2,760,000 hadi Sh4,850,000 kuanzia mwezi Julai na ongezeko hilo ni sawa na asilimia 75.7

Mishahara ya wabunge,mawaziri na majaji imepandisha huku wa spika wa bunge ukipanda mara dufu. Kwa kifupi tu; Spika na Jaji mkuu Tshs 2,760,000/= mpaka 4,850,000/= Naibu spika Tshs 2,080,000/= mpaka 2,172,000/= Mbunge Tshs 1,840,000/= Mpaka 1,921,000/= jaji wa mahaka kuu tshs 2,160,000/= mpaka 3,645,000/= jaji Mahakam ya rufaa Tshs 2,310,000 mpaka 4,250,000/= Kwa hali hii kweli tutapona? Source:Mwananchi

Mazishi ya Wanafunzi 12 yanafanyika leo

Mazishi ya Wanafunzi 12 wa Shule ya Sekondari ya Idodo mkoani Iringa waliofariki kwa ajali mbaya ya moto Bwenini yanafanyoka leo hii hapo shuleni katika kaburi la pamoja. Wanafunzi waliokufa katika tukio hilo ambalo leo watazikwa kaburi moja ni ni Matrida Mtewele, Adelvina Kwama na Elizaberth Mtavila ambao walikuwa wanasoma kidato cha kwanza.Wengine ni Digna Nduguru, Chake Kuyaa, Seciliana John, Lazia Kihwele, Witness Mbilinyi na Stellah Mwigavilo waliokuwa wanasoma kidato cha pili.Pia wamo Falha Abdallah na Jesca Wissa waliokuwa kidato cha tatu na Maria Ndole wa kidato cha nne ambapo alisema kutokana na marehemu hao kuteketea kiasi cha kutotambulika, wametumia njia zingine kupata majina yao Imebidi miili hii izikwe kwa pamoja kutokana na zoezi la kutambua miili hiyo kuwa gumu kutoka na kuungua vibaya. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Picha za Mazishi zitafuta si muda. Picha kwa hisani ya Fransis Godwini

August 22, 2009

Mfungo Mwema

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ndo umeanza, blog hii yapenda kuwatakia mfungo mwema wa mwezi huu mtukufu na pia kuwaasa wale wote wanaofunga kuwa kufuata mafundisho ya Quran Tukufu kuhusu mwezi huu. Tunasema Ramadan Kareem.

August 21, 2009

Kumbe JK atembea na peremende!!

Rais JK akimpatia peremende mtoto wa huko Lindi anakoendelea na ziara.

Michelle Obama azidi kuwachengua wamarekani na Dunia

Mama Michelle Obama akiwa na mwanae ndani ya vikaptula akishuka ktk Air Force One ni Mke wa Rais wa Kwanza (nathani Ulimwenguni) kutoka namna hiyo.

Tausi Likokola wamkumbuka??

PRESS RELEASE: Tausi Likokola has walked countless runways, appeared on various magazine covers and has worked with some of the top fashion designers and houses such as Gucci, Christian Dior, Issey Miyake, Esacada, and Tommy Hilfger.
We have been reading all the blogs where we see many people asking, “Where is Tausi?” The answer to the much asked question is Tausi has quietly taken on the role of motherhood to her two children while continuing to walk red carpets, make special appearances as well as continue writing her books.
Her fourth book "The Touch of an Angel" is out August 2009 in North America and will be available in September 2009 in all major bookstores suchas Barnes and Nobles, Borders, etc. across America. Internationally, Touch of an Angel will be available through Amazon. Com. Tausi also just appeared on this cover of "Her Scene", which is an upscale glossy fashion magazine. She is honored to be selected as the first woman of color to ever appear on this cover.

To the many journalists who have sent inquiries to Tausi, this is her response: "I am well and blessed. I’m most grateful for my largest life blessings which are my children Imani and Neema. I enjoy modeling, but I most enjoy being a model mom, because I love being a mother. Thanks to all who have supported me and all those who continue doing so. God bless"
Tausi now resides in USA. WWW.TAUSIDREAMS.COM http://www.youtube.com/watch?v=7_hhfofLjsI
Mwanamitindo wa kimataifa toka Tanzania Tausi Likokola bado anatesa ktk anga za mitindo wengi waweza kuwa mmemsahau hebu mcheki hapa katika youtube jinsi vile badi anatesa kwa sana.

August 20, 2009

Serikali yamkatia rufaa Zombe

Kulingana na taarifa zilizoifikia blog hii ni kuwa Mahakama ya Rufaa imekiri kupokea kusudio la kukata rufaa dhidi ya ACP Abdalh Zombe na wenzie nane leo hii na uenda kesi hiyo ikaanza kusikilizwa ktk mahakama hayo Jumatatu.

Ndundu - Somanga Road kuwa rami

President Jakaya Mrisho Kikwete cuts a tape to officially inaugurate the construction of a 60 km Ndundu –Somanga road at Nyamwage village, Coastal Region yesterday afternoon.
Others in the picture from left are Karafi Holdings Group Managing director,Mahmoud Shehata,The First Lady Mama Salma Kikwete(third left), The Minister for Infrastructure Development Dr.Shukuru Kawambwa, and The minister for Justice Mathias Chikawe

August 19, 2009

Hili la CCM na UFISADI Limekaaje wadau?

HALMASHAURI Kuu ya CCM juzi ilifikia uamuzi wa aina yake baada ya kuunda kamati maalumu ya kuwashughulikia wabunge wake wanaoikosoa serikali ya chama hicho tawala, huku ikimwekea kinga rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
“Bunge limeanza kuwa kama mchezo wa (kikundi cha televisheni cha vichekesho) The Comedy,” alisema katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati wakati akizungumza na waandishi wa habari jana.
“Yaani kila mtu anafanya mambo yake mwenyewe, hali ambayo inaweza kusababisha watu kurushiana hata viatu ndani ya Ukumbi wa Bunge, sasa hali hii maana yake nini? “Kwa hiyo tumesema inatosha, hapo tulipofikia tusiendelee mbele.
Wanaoropoka ovyo ni walevi na tumeona kuna kundi dogo ambalo limejiona kama ni wateule wa kuzungumzia sakata hilo (la ufisadi) bila ya kujua wabunge wote wana haki ya kuzungumzia suala hilo, lakini kwa utaratibu tena kwa kupitia katika vikao vya kamati za wabunge.”
source: mwananchi

ASKOFU MAYALA AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufikia kutoka Rock City zinasema kuwa Askofu Mkuu Anthony Mayala( 69) wa Kanisa Katoliki Mwanza amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Bugando alikopokelewa baada ya kuugua ghafla.
Taarifa kutoka Mwanza kwa Msaidizi wake, Padri Renatus Nkwande zilieleza kuwa Askofu Mkuu Mayala aliugua ghafla saa mbili asubuhi baada ya kuishiwa nguvu na alikimbizwa katika hospitali hiyo kabla mauti hayajamkuta saa 8:30 mchana.
“Hatutajua ni nini zaidi maana alikuwa mzima na asubuhi ali-collapse ghafla tukamkimbiza hospitali,” alisema Padri Nkwande ambaye alifafanua kuwa awali Askofu Mayala alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo mara kwa mara.
Alisema Jimbo hilo limepokea kwa masikitiko taarifa za madaktari kuhusu kifo hicho na kuongeza kuwa Jimbo limempoteza msimamizi aliyekuwa wakati wote msikivu wa shida za watu bila kujali imani zao, mcha Mungu, mpole na mnyenyekevu wa kuigwa na kwamba daima hakupenda kupigizana kelele na watu hata kama nafasi yake ingemruhusu kufanya hivyo.
Alisema utaratibu wa mazishi utafanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kwa kushirikiana na Jimbo hilo na kwamba taarifa zaidi zitapatikana kesho.Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TEC, Anthony Makunde alithibitisha taarifa za kifo cha Askofu Mayala na kueleza kuwa taarifa nyingine za maziko ya Askofu Mayala zitaelezwa baadaye.Askofu Mkuu Mayala alipata daraja la Upadri mwaka 1970 na mwaka 1979 aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Musoma kabla ya kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza mwaka 1988.
Sisi tunasema Bwana Alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Chandimu!!

Wengi tumepitia hapa, hata baadhi ya mastaa wamepita pia hapa, na hawa ni kina Ronaldo au Etoo wa kesho wakijaribu huko Sumbawanga kama mdau Peti Siyame alivyowashuhudia leo hii.

Mama Salma na Malkia wa Uswazi

Mama salma kikwete akigonganisha glasi na mke wa Mfalme Mswati III wa Swaziland Malkia Nomsa Matsebula wakati wa chakula cha usiku ambacho mama kikwete alimwandalia malkia huyo,ikulu

Hashim Thabeet alipomtembelea JK Ikulu

JK and HT
Hasheem Thabit and his mother Rukia Presents a basketball Tshirt number one to Presisent Jakaya Mrisho Kikwete at Dar es Salaam State house yesterday afternoon when the president hosted a lunch in honor of the professional basketballer currently an NBA member.

August 17, 2009

Zombe na wenzie ni KICHEKOOO

Habari zilizotufikia punde ni kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania imewaachia huru ACP Abdalah Zombe na watuhumiwa wingine wote na kuwaona hawana hatia ya mauaji ya Wafanyabiashara watatu na dereva teksi waliyokuwa wakishtakiwa nayo na kudaiwa kuyatendenda mnamo Januari 14 2006.

JK na hadithi ya Nabii kutokukubalika kwao

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali muasisi wa TANU na CCM Mzee Omar Selemani Mwenye umri wa miaka 104 aliyelazwa katika hospitali mkoa wa Dodoma. Mzee Omar Selemani ni mweyekiti wa Umoja wa wazee Mkoani Dodoma.Wakati wa harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika Hayati Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alikuwa akifikia nyumbani kwa Mzee Omari Selemani na kufanya shughuli za siasa
Naomba kwanza nikiri hapa kuwa si kawaida yangu kumwaga ngojera ktk Bongo pix bali taswira zaidi, lakini yapo ambayo wakutana nayo na uwezi kuyaweka ktk taswira ili watu wajionee hivyo wafanyaje? watoto wa mjini wanasema unakubali yaishe.
Hivi karibuni nilipata bahati ya kutoka nje ya nchi kidogo na kwenda Jo'burg kwa Mzee Madiba katika kuongeza ama kujinoa zaidi na taaluma yetu hii ambayo yabadilika kila uchao, yapo mengi niliyaona na kuyasikia katika juma zima nililokaa huko bondeni, mazuri na mabaya pia lakini moja wapo ya ambayo nilisikia mara kwa mara ni juu Rais wetu JK na vile jinsi ya wenzetu wamwonavyo.
Siku ya kwanza ya darasa letu tulianza kwa utambulisho kama ilivyo kawaida au ustaarabu kwa sehemu zote watu wakutanapo mara ya kwanza, niliposena kuwa natoka TZ nilipata macho mia mia toka kwa washiriki ka watatu hivi, mwanzo sikufahamu kwa nini ila nilikuja jua baadaye wakti wa breki, kulikuwa na washiriki toka Cameruni, Comoro, Afrika Kusini, Sao Tome and Principle, Tanzania na Zimbabwe, wakti wa mapumziko hayo walikuja kunisalim kwa karibu zaidi washiriki toka Comoro, Zimbambwe na Afrika Kusini, walikuja si kunisalimu tu na kutaka kujua zaidi habari za Bongo na zaidi Rais wetu JK, wote (sijui kama waliambiana) walimsifu kwa namna ya pekee JK na kuonyosha kumkubali kwa jinsi vile anavyoendesha nchi, na kuonyesha wazi kuwa wanatonea wivu sana kuwa na rais kama huyu. Mi sikuwa na la kusema kwa sababu kwa akika si kitu nilikitarajia, na labda sidhani kama WATZ nao ndivyo wamwonavyo au la sijui kwani sijawai kufanya utafiti huo, lakini pia nilidhani labda ni kutokana na kauli ya Rais Obama aliyoitoa wakti wa kuanza ziara yake ya kwanza barani Afrika, sijui, lakini kila mmoja alikuwa na sababu yake tofauti kabisa na hilo, mfano Mzimbabwe ye alisema JK alikuwa ni Rais pekee aliyethubutu kumnyooshea kidole Mugabe ktk kikao cha wakuu wa SADC na kupelekea kutoa tamko lile lililosomwa na Waziri Membe ambalo limepelekea kuwa na serikali ya umoja, anasema japo hali ya kiuchumi haijatengemaa na kuwa wanalazimika kutumia pesa za kigeni hata kununua chungwa na kuwa Zimdollar yalipia Daladala tu lakini angalau kuna utulivu wa kisiasa ambao anazani una mchango mkubwa wa JK. Mcomoro anamwona ni kiongozi shujaa hasa kwa kuthubutu kutuma majeshi kukomboa kisiwa cha Anjuani na kumwondosha Mtawala Mohamed Bacar mbali na juhudi nyingine za upatanishi wa kidiplomasia barani Afrika na zaidi mgogoro wa Kenya. Msauzi anamwona ni kiongozi wa mfano barani Afrika, haya ni baadhi tu ya yale niliyoyasikia au kuyakumbuka angalau kwa sasa kwani kwa siku sita nilizokaa Jo'burg ni mengi yaliongelewa ni sifa nyingi zilimiinwa kiasi cha hata washiriki wengine ambao hawakumjua JK kufanya kazi ya ziada kwenye mitandao kusaka habari zake na TZ kwa ujumla. Siku ya kuondoka nilipata bahati ya kukutana na baadhi ya wabongo wenzangu pale uwanjani na bila kuchelewa tulijikuta tuna chati haya na yale mmoja akitokea Harare na mwingine Jo'burg na sote tukirejea Dar, mara likaibuka ktk maongezi yetu hili la JK na jinsi anavyokubalika na zaidi Wazim wanavyomkubali, ikabidi kujiuliza kulikoni JK? na kwa hakika sidhani umaarufu huu au sifa hizi wampazo watu hawa je anazipata hapa nyumbani? au ndo nabaii uwa akubaliki kwao? Haya yamewapata manabii wengi Bwana Yesu akiwamo. Je weye mdau wasemaje?

Zim nauli ya Daladala Bilion tatu

Zimdollar ni pesa ya kulipa ktk Daladala tu, uwezi nunulia chochote huko.
HARARE, Zimbabwe – A woman pays her bus fare with 3 trillion in old Zimbabwe dollars — the equivalent of 50 U.S. cents. The collector accepts the brick of neatly folded bundles of a trillion each without bothering to count the notes.
"No one seems to worry, and it works," said the woman, Lucy Denya, a Harare secretary who says she's seen police officers using old notes to board buses.
The Zimbabwe dollar is officially dead. It was killed off in hopes of curbing record world inflation of billions of percentage points, and Zimbabwe has replaced it with the U.S. dollar and the South African rand.
Yet the role of the old Zimdollar, as it is known, remains in flux. It is still used, and has become another point of contention for the divided leadership of the country, now one of the poorest in the world.

August 14, 2009

Fidia ya mabomu ni balaa tupu.

MAANDALIZI ya kuwalipa fidia wakazi wa Mbagala walioathiriwa na mabomu yameingia dosari baada ya baadhi ya majina ya watu kukosekana kwenye orodha ya malipo, huku majina mengine yakitofautiana na namba za nyumba zilizoathiriwa.
Jumla ya Sh8.5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wakazi ambao nyumba zao ziliathiriwa na milipuko ya mabomu iliyotokea Aprili 29 kwenye ghala la silaha la kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) iliyo Mbagala na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 29. Fedha hizo zitatumika kulipa fidia nyumba 9,259 zilizoharibiwa na mabomu hayo na ambazo zilihakikiwa na serikali.
Lakini uchunguzi wa gazeti hili jana umebaini kuwa mchakato wa malipo hayo umeanza kuingia dosari baada ya watu kadhaa waliofika ofisi ya afisa mtendaji kata ya Mbagala Kuu, kugundua kuwa majina yao hayapo kwenye orodha iliyobandikwa ukutani na wengine kukuta tofauti ya majina na namba za nyumba.
Afisa mtendaji wa kata hiyo, Basil David alisema kuwa zaidi ya watu 50 waliofika ofisini kwake kuangalia majina yao, walikuta aidha yamekosewa au hayaendani na namba za nyumba zao. "Ni kweli zimejitokeza kasoro kwenye mchakato huu. Zipo namba za nyumba zilizokosewa na majina mengine yanatofautiana na namba za nyumba hizo,” alisema.
"Kutokana na hali hii tumeziagiza ofisi za serikali za mitaa kuorodhesha majina ya watu ambao majina yao au namba zao zimekosewa, ili ayapeleke kwa mkuu wa mkoa kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho kabla ya kuandaliwa kwa hundi za malipo," alisema.

Katoliki- Kingunge amepwelea,

MALUIMBANO kuhusu waraka wa Kanisa Katoliki (RC) yanaendelea kuwa makali, baada ya waumini wa kanisa hilo kumuelezea mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru kuwa amepwelea. Mbali na kauli hiyo iliyotolewa jana na Baraza la Walei, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Valentino Mokiwa amemtaka Kingunge kuliomba radhi kanisa badala ya kuombwa radhi kama alivyotaka. Matamko hayo mazito yalitolewa kwa nyakati tofauti jana wakati wahusika hao walipokuwa wakizungumza na gazeti hili kuhusu utashi wa Kingunge kuwa Kanisa Katoliki limuombe radhi na kuungama kutokana na kumwita kuwa ni mkongwe. Mwenyekiti wa Baraza la Walei, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Balozi Nicholas Kuhanga alisema baraza limewataka maaskofu wa kanisa hilo, kutoendelea kujibishana na Kingunge badala yake kazi hiyo sasa itafanywa na baraza hilo. Kuhanga, ambaye amewahi kuwa waziri, alisema wamefikia uamuzi huo kwa kuwa baraza linamjua kwa undani mwanasiasa huyo kwa kuwa wanaishi naye.
Balozi Kuhanga alisema anamshangaa Kingunge kuupinga waraka huo wakati unawasisitizia wananchi kuwachagua viongozi waadilifu na wanaojali maslahi ya wananchi. Alisema kanisa haliwezi kumwomba radhi Kingunge kwa kuwa hana tofauti na mafisadi kutokana na kitendo chake cha kupinga waraka unaowapinga mafisadi.
"Yeye anaingia katika kundi hilo, (Mafisadi) kutokana na msimamo wake wa kuupinga waraka huo unaopinga ufisadi nchini," alisema Kuhanga. "Wale ambao hawana hulka za kifisadi wanaunga mkono waraka wakati wale ambao wana hulka za kifisadi wanaupinga, kwa sababu unatishia maslahi yao." Alifafanua kuwa waraka huo umetolewa kama somo la uraia ambalo limeonekana kufifia na kusababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii.
source: Mwananchi

August 13, 2009

Kingunge vs Maaskofu ngoma bado mbichi

MWANASIASA Mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru, ameendelea kuung'ang'ania waraka wa Kanisa Katoliki na sasa amelitaka kanisa hilo limwombe radhi kwa kumwita fisadi alipoupinga bungeni.

Waraka huo uliotolewa Machi mwaka huu, ulilenga kuwapa mwongozo waumini wa Kanisa Katoliki wa namna ya kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao, vipaumbele vya kitaifa na aina ya kiongozi anayefaa kuchaguliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana, Kingunge alisema alishangaa kusikia kanisa hilo likisema wanaohofia waraka huo ni mafisadi baada ya yeye (Kingunge) kutoa angalizo bungeni katika Mkutano wa 16 uliomalizika Julai 31 mwaka huu.

"Maaskofu wamenisikitisha sana katika hili. Hatuwezi tukakubali nchi ikapelekwa wanavyotaka wao, tunaomba waache," alisema Kingunge na kuongeza:

"Nashangaa, askofu mzima akazungumza na kuniita fisadi, hiyo ni dhambi. Askofu huyo akaungame. Mimi sipendi neno fisadi ni afadhali kama rushwa iitwe rushwa".

Hata hivyo, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Method Kilaini jana alikataa kujibu kauli hiyo ya Kingunge akisema hataki kulumbana na mkongwe huyo wa siasa.

"Sitaki kulumbana naye, mzee wa watu ni mzee wa watu tu, hivyo sitaki kuendeleza malumbano naye,"alisema Kilaini.

Kwa mujibu wa Kingunge, viongozi wa Kanisa Katoliki wamemkejeli na kumtukana kuwa hajasoma kwani anaamini kwamba aliusoma waraka huo vizuri na kuulewa kwa kina kabla hajatoa kauli hiyo.

'Niliusoma vizuri na kuelewa. Hivi nitashindwa kuelewa walichoandika, nimesoma maandiko ya dini ya Kiislam, Kihindu na nyingine, siwezi kushindwa kusoma na kuelewa waraka huu." alisema Kingunge juzi alipokuwa akihojiwa na kituo cha Channel 10 na kuongeza:

"Sikutaka kuingia katika maudhui, maana nikiingia katika maudhui ningelumbana nao kwamba dini inakuaje na ilani, ilani inapaswa kuandaliwa na vyama vya siasa tu na si vinginevyo," alisisitiza.

Kingunge alisema ni vizuri kanisa likaelewa kuwa lenyewe sio chama cha siasa na kwamba, halina uwezo wa kuandaa ilani ya uchaguzi.

Alifafanua kwamba, wakati anazungumzia waraka huo bungeni hakuwa anataka uhasama na kanisa kwa kuwa anaheshimu imani, ila alikuwa akitoa angalizo kwa kuwa dini haiongozi nchi kama serikali.

"Ukiona vyaelea, jua vimeundwa" angekuwepo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hapa, kanisa hilo lisingethubutu kuandaa waraka huo, mimi pia ni mkongwe, hivyo hakuna yeyote ambaye anaweza kusimama na mimi kuhusu historia ya nchi hii.

Nataka niwaambie kwamba, tunajua mambo ya Kanisa Katoliki, lakini kwa bahati mbaya mwalimu hayupo,"alisema.

Kingunge aliendelea kulishambulia kanisa hilo akidai kuwa linataka kuwatoa Watanzania katika utamaduni wao na kulishauri kuunda chama cha siasa kama linaona ni vyema.

Alisisitiza kuwa dini si chombo cha kuunganisha watu, bali kuwatenganisha ndiyo maana kila mtu ana dini yake, lakini serikali ni moja, hivyo nchi yenye dini nyingi haiwezi kuunganishwa na dini bali siasa.

Katika malumbano hayo yaliyodumu kwa muda sasa, kanisa liliutetea waraka huo likisema kuwa sio mara ya kwanza kuutoa kwa waumini wake.

Lilisema huu umekuwa utaratibu wa kanisa hilo tangu mwaka 1995 ukiwa na lengo la kuwaelimisha waumini wake kuhusu namna ya kutekeleza haki yao ya kupiga kura.

source: Mwananchi

August 12, 2009

JK ziarani Mbinga

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Bi.Martha Mahundi na mwanae aliyejifungua kwa upasuaji katika kituo cha Afya Lituhi,wilayani Mbinga,Mkoani Ruvuma, jana.Wapili kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki Mbinga Dr.Emmanuel Mapunda na kushoto ni mganga mkuu wa kituo hicho Martin Ndunguru.Rais Kikwete alikitembelea kituo hicho cha Afya ambapo Askofu Mapunda aliomba kituo hicho kupandishwa hadhi na kuwa hospitali kamili.

Happy Birth Day Mtoto wa Mkulima

Leo ni siku ya kuzaliwa ya Mtoto wa Mkulima Mizengo Pinda.

August 11, 2009

Waziri aomba uume wa mwalimu aliyemjaza mimba mwanafunzi usifanye kazi

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza amewataka wananchi wa kijiji cha Muze wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kumuombea dua mbaya aliyekuwa mwalimu wa shule ya sekondari Mazoka aliyempa mimba mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo.
Mahiza alisema taarifa ya shule ilimsikitisha na baadhi ya matatizo yaliyoainishwa yatashughulikiwa na serikali.
" Na hili la huyu bazazi, aliyemkatisha masomo mwanafunzi ni lazima tumuombee dua ili asisimame daima,uume wake uache kufanya kazi" alisema.
Alisema mwalimu ndiye kioo cha jamii, lakini mwalimu anapomkatisha masomo mwanafunzi ni lazima achukuliwe hatua kali za kisheria na kinidhamu na kwamba kwa vile alitoroka dua limfuate huko aliko.

Iluminata anawakilisha Miss Universe 2009

Illuminata Wize, Miss Tanzania 2009; Ekta Chowdhry, Miss India 2009;Jenel Cox, Miss Guyana 2009, and Jewel Selver, Miss Turks & Caicos2009, pose for a photo with a dolphin at Dolphin Cay in Atlantis,Paradise Island, Bahamas on Saturday, August 8, 2009. They are in theBahamas for the 2009 Miss Universe competition which will be held inthe Imperial Ballroom at ATLANTIS, Paradise Island, Bahamas, LIVE onNBC Television network at 9 pm ET on Sunday, August 23, 2009. ho/MissUniverse Organization

Mama Pinda ziarani

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwasalimia wanchi wa kijiji cha Naleta wilani Kiteto akiwa ameongozana na Mumewe Mtoto wa Mkulima Mizengo Pinda aliyeziarani mkoa wa Manyara

August 8, 2009

Nini kinaendelea CCM,

KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amepinga kauli ya makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela kwamba, chama hicho kitakuwa na wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu ujao. Juzi Malecela alisema CCM itakuwa na wakati mgumu katika uchaguzi huo wa mwaka 2010 kwa sababu ya tuhumu nyingi za ufisadi na baadhi ya wabunge wake kushindwa kutekeleza ilani ya chama hicho ya mwaka 2005.
Kwa mujibu wa Malecela, vita dhidi ya mafisadi ni ngumu kwa sababu ndani ya CCM kuna baadhi ya watu wanaokichafua chama kwa tabia zao za kuungana na mafisadi. Lakini, Makamba jana alisema ufisadi anaozungumzia Malecela kwamba utakisambaratisha chama hicho mwakani ni wa kufikirika kwa sababu mpaka sasa hakuna mwenye ushahidi unaodhihirisha kwamba fulani ni fisadi.
"Mimi siwajui hawa mafisadi. Hebu wewe nitajie jina la mtu mmoja ambaye una ushahidi kuwa ni fisadi," alisema Makamba.
Alipoulizwa kuhusu baadhi ya makundi ya mafisadi ambayo tayari yameanza kampeni ya kusambaza pesa za kuwaangusha kwenye majimbo wabunge walio mstari wa mbele katika vita dhidi yao, Makamba alisema, "siyo kweli ila ni jambo ambalo linakuzwa tu."

Hongera Sylivia Shally

Sylivia Frank Shally ndiye kaibuka Miss Ilala 2009 na Michuziblog Photogenic pia, blog hii inapenda kukupa hongera sana kwa kunyakua mataji hayo, na inakutakia kila la kheri ktk safari ya kunyakua taji la Miss TANZANIA 2009, BP ilishakuona na kukupigia kura na kura hiyo haikuaribika.
Naam karibu ktk ulimwengu huu wa ulimbwende ambao marafiki zake wa karibu sana ni wachukua sura au wapiga snap ka BP au Mzee wa Libeneke na kwa kuwa umekuwa Miss Photogenic yaani lens ndo zitakuwa patna zako una UJANJA una pa kukwepe Dada, na zaidi ni kuwa si lens zote zitakuwa na lengo la kukupamba kwa mazuri tuu, hapana zipo ambazo kazi yake kubwa ni nkupaka matope tuu, jiandae na hizo pia, kwani huna pa kuzikwepea dada.
Picha kwa hisani ya wadau

Ka - Skuli na ka mtoko finito

Mpiga Picha Mkuu wa AFP Afrika Alexander JOE akimkabidhi cheti Mzee Bongo Pix kuashiria Ka mtoko na Ka skuli kalonleta Sauzi kufikia mwisho leo hii nataraji panapo majariwa yake mwenzezi basi kesho ntakuwa home

Athuman na Mtui wanaendelea vyema

Leo tena nilipata nafasi ya kuwatembelea Wadau Athuman na Mtui na kushuhudia wakifanyishwa mazoezi ya viungo pamoja na kusoma, kwa kweli Munguni mwema sana kwani wanaendelea na wanafanya vyema kwenye matitabu. BP kwa niaba ya wadau wote twawatakia mpone haraka na mrejee Bongo mkiwa wa Afya tele ili kulijenga taifa letu.

August 6, 2009

Salam toka Soweto

Leo nimetembelea Soweto na kupata bahati ya kufika katika nyumba aliyokuwa akiishi Mzee Madiba ambayo sasa imegeuzwa kuwa kivutio cha utalii, Nyumba hii Mzee Mandela aliishi na familia yake kuanzia Mwaka 1949 mpaka miaka ya tisini alipoitoa ili iwe makumbusho.
Ukiwa Jo' burg si sehemu ya kukosa kwenda.

August 5, 2009

Love strengthens the union

Sote tukaoe Zenji ili kudumisha muungano?
Ndo ushauri wa Adam Mwana wa Lusekelo

Chinga wa SAUZI waandamana.

Ch
Kumbe ile kashehe ya Chingaz na Mgambo sio Dar mpaka Jo'burg ipo pia, Leo hii Chingaz wa Jo' burg wameandamana mitaani kupinga unyanyasaji unaofanywa na polisi na kuwapola mali zao, maandamano hata hivyo yalikuwa ya amani huku polisi wakilinda usalama.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...