ASKOFU Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema maaskofu wasifundishwe namna ya kufikisha kazi ya Mungu na kufikisha ujumbe wao kwa waumini.
Kauli hiyo ya Pengo ambayo aliitoa mbele ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, pasipo kutaja waraka, imetolewa baada ya waraka uliotolewa na kanisa hilo kuzua mjadala mkali nchini, ukihusisha watu wa kada mbalimbali. Mjadala wa hoja hiyo pia ulifika katika Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM ambako ulijadiliwa na kutolewa maazimo.
Katika maazimio hayo, NEC iliwataka viongozi wa Serikali na Kanisa Katoliki kukutana, ili kupata ufumbuzi wa mzozo wa waraka huo ambao unataka wananchi wachague viongozi waadilifu wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani.
Mbali na NEC, wakati akijibu mwaswali ya papo kwa papo bungeni hivi karibuni, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema ni vema uongozi wa kanisa hilo ukapeleka waraka huo serikalini, ili iweze kusambaza kwa wananchi, badala ya utaratibu wa sasa unaotoa mwanya kwa kila dhehebu kujiandikia na kusambaza nyaraka...................
source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment