August 8, 2009

Nini kinaendelea CCM,

KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amepinga kauli ya makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela kwamba, chama hicho kitakuwa na wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu ujao. Juzi Malecela alisema CCM itakuwa na wakati mgumu katika uchaguzi huo wa mwaka 2010 kwa sababu ya tuhumu nyingi za ufisadi na baadhi ya wabunge wake kushindwa kutekeleza ilani ya chama hicho ya mwaka 2005.
Kwa mujibu wa Malecela, vita dhidi ya mafisadi ni ngumu kwa sababu ndani ya CCM kuna baadhi ya watu wanaokichafua chama kwa tabia zao za kuungana na mafisadi. Lakini, Makamba jana alisema ufisadi anaozungumzia Malecela kwamba utakisambaratisha chama hicho mwakani ni wa kufikirika kwa sababu mpaka sasa hakuna mwenye ushahidi unaodhihirisha kwamba fulani ni fisadi.
"Mimi siwajui hawa mafisadi. Hebu wewe nitajie jina la mtu mmoja ambaye una ushahidi kuwa ni fisadi," alisema Makamba.
Alipoulizwa kuhusu baadhi ya makundi ya mafisadi ambayo tayari yameanza kampeni ya kusambaza pesa za kuwaangusha kwenye majimbo wabunge walio mstari wa mbele katika vita dhidi yao, Makamba alisema, "siyo kweli ila ni jambo ambalo linakuzwa tu."

Hongera Sylivia Shally

Sylivia Frank Shally ndiye kaibuka Miss Ilala 2009 na Michuziblog Photogenic pia, blog hii inapenda kukupa hongera sana kwa kunyakua mataji hayo, na inakutakia kila la kheri ktk safari ya kunyakua taji la Miss TANZANIA 2009, BP ilishakuona na kukupigia kura na kura hiyo haikuaribika.
Naam karibu ktk ulimwengu huu wa ulimbwende ambao marafiki zake wa karibu sana ni wachukua sura au wapiga snap ka BP au Mzee wa Libeneke na kwa kuwa umekuwa Miss Photogenic yaani lens ndo zitakuwa patna zako una UJANJA una pa kukwepe Dada, na zaidi ni kuwa si lens zote zitakuwa na lengo la kukupamba kwa mazuri tuu, hapana zipo ambazo kazi yake kubwa ni nkupaka matope tuu, jiandae na hizo pia, kwani huna pa kuzikwepea dada.
Picha kwa hisani ya wadau

Ka - Skuli na ka mtoko finito

Mpiga Picha Mkuu wa AFP Afrika Alexander JOE akimkabidhi cheti Mzee Bongo Pix kuashiria Ka mtoko na Ka skuli kalonleta Sauzi kufikia mwisho leo hii nataraji panapo majariwa yake mwenzezi basi kesho ntakuwa home

Athuman na Mtui wanaendelea vyema

Leo tena nilipata nafasi ya kuwatembelea Wadau Athuman na Mtui na kushuhudia wakifanyishwa mazoezi ya viungo pamoja na kusoma, kwa kweli Munguni mwema sana kwani wanaendelea na wanafanya vyema kwenye matitabu. BP kwa niaba ya wadau wote twawatakia mpone haraka na mrejee Bongo mkiwa wa Afya tele ili kulijenga taifa letu.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...