October 2, 2011

Salamu toka IGUNGA

Kijana (bila shaka shabiki wa CHADEMA) akimsadia mwenzie wa CCM kutundika bendera wakati wa kampeni zilizoisha jana huko Igunga. Picha hii nimeipata JF, nimeipenda sana, inasema maneno zaida ya 1000 kuhusu siasa jimboni humo.
Kila mtu anaweza kuwa na tafsiri yake, na  hakika kila mtu ana haki kuwa na maoni au tafsiri yake, ndio demokrasia. 

Igunga UPDATES: Marehemu wafufuka kupiga kura!

Kwa mujibu wa ITV Igunga Live, 

 • kuna wafu wamefufuka na kwenda kupiga kura leo hii,
 • Watu kadhaa hawaoni majina yao vituoni
 • Wapo waliopiga kura mwaka jana leo hii kadi na majina haviendani. 
 • Kuna baadhi vituo vifaa havijafika, 
 • Sehemu nyingine vimepelekwa kwa baiskeli na punda kutokana na ubovu wa miundombinu. 
 • Vijana wamejitokeza kwa wingi kuliko mwaka jana,
 • Hari ni shwari mpaka sasa.


Wana igunga kukata mzizi wa fitina leo.

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akimnadi Mgombea wa CCM Peter Kafumu. Umati mkubwa wa watu ukimsikiliza Benjamin Mkapa Rais Mstaafu wa Tanzania na Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM wakati akifunga kampeni.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakijaribu kumdhibiti mgombea wa ubunge wa jimbo la Igunga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Leopard Mahona, ambaye alitaka kupigana wa wafuasi na viongozi wa Chadema kutokana na CUF kuingilia mkutano katika kijiji cha Nyandekwa jana. (Picha na Joseph Senga)

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakijaribu kumdhibiti mgombea wa ubunge wa jimbo la Igunga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Leopard Mahona, ambaye alitaka kupigana wa wafuasi na viongozi wa Chadema kutokana na CUF kuingilia mkutano katika kijiji cha Nyandekwa (Juu), Julius Mtatiro wa CUF akitoa malalamiko kwa askari (CHINI) (Picha na Joseph Senga)

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwaongoza wakazi wa mji wa Igunga na vitongoji vyake kuonyesha ishara ya kukikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati wa mkutano wa kufunga kampeni, kwenye Uwanja wa Barafu jana. 


Baada ya kampeni za takriban mwezi Mmoja zilizokuwa zimejaa kila aina ya vibweka na vituko na matukio yasiyotarajiwa ambazo hazikuwai kushuhudiwa jimboni humo na kuitimishwa kwa mbwembwe za kutimuliwa vumbi la kutosha kutoka kwa helikopta zipatazo nne hatimaye leo hii wana Igunga wataamua ni nani kati ya wagombea nane atakuwa mwakilishi wao.


Jumla ya vyama nane vimesimamisha wagimbea navyo ni
 1. CCM Peter Kafumu
 2. CHADEMA – Joseph Kashindye
 3. CUF – Leopold Mahona
 4. AFP – Steven Makingi
 5. CHAUSTA – Hassan Ramadhani
 6. DP – Abdalah Chem
 7. UPDP – Hemed Ramadhan
 8. SAU – John Magifi


Kampeni za Igunga zimeshuhudia vyama vyenye nguvu ama jeuri ya pesa vikitumia kila aina ya usafiri na tambo kuwafikia wapiga kura kuanzia Mashangingi mpaka Helikopta huku vinyonge vikiishia kutumia Punda na pikipiki na hivyo kuwafikia wapigakura wachache sana achilia mbali vingine kuanza kampeni siku nne kabla ya uchaguzi.


Kila le kheri wana Igunga.  

Google+ Followers

There was an error in this gadget
There was an error in this gadget

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...