September 27, 2010

If thats true, you made my day! @VODACOM

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ya Intaneti ambayo itawawezesha wateja wake kuchati kwa intaneti bure.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba alisema jana kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kuchati bure kwenye tovuti za Face Book, the Grid na Vodamail.
Alisema Vodacom Tanzania inatoa huduma hiyo kwa lengo la kuwawezesha wateja wake kupata muda wa kuchati zaidi.
Alifafanua kwamba hayo yote yatawezekana kwa kutumia mtandao wa 3G ambao una kasi na nguvu kubwa.
“Tunapenda wateja wetu watumie mtandao wetu kwa kuwasiliana bure na hivyo kukata kiu yao ya mawasiliano”.
Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma hiyo ya mtandao wa Intaneti.
Aliwaomba Watanzania kujiunga na Vodacom ili kupata huduma hiyo bure na hivyo kuwasiliana zaidi.
Alisema huduma hiyo itapatikana kwa simu za mkononi na pia kwa Laptop zilizounganishwa na USB Modem.
My take:
Ki ukweli sijawai kuwa mteja wa Vodacom, (usiniulize, sijui ni kwanini) lakini kwa ofa hii na hasa kama itakuwa inapatikana katika modem ambapo itaniwezesha kutumia katika laptop yangu na si kwenye simu peke yake, na iwe UNLIMITED ACCESS, Sio siri leo hii hii na si kesho nitajiunga haraka sana.
Lakini ni nani wa kunihakikishia hilo? Bi Makamba au Bw Mafuru? gharama za internet kwa sisi wengine imekuwa kama damu maishani mwetu ktk dunia hii iliyochanganyikiwa na mtandao (ICT ERA), uwa najiuliza siku nitakayo amka na kukuta mitandao imeparaganyika, sijui itakuwaje, na kwa hakika sitaki kuota wala kujua siku iyo.
.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...