February 8, 2013

R.I.P Bishop Thomas Laiser, R.I.P Amadeus Msarikie

Bishop Thomas Laiser
Askofu Thomas Laizer wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini dayosisi ya kaskazini kati, amefariki dunia katika hospitali ya rufaa ya Seliani iliyopo jijini Arusha ambako alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa akipata matibabu. Taarifa zaidi juu ya kifo chake tutakupatia pindi zitakapo tufikia katika dawati letu la GK.

Wakati huohuo aliyekuwa askofu wa jimbo la moshi kanisa katoliki Amedeus Msarikie amefariki dunia jana alfajiri mkoani Kilimanjaro. Askofu Msarikie alistaafu baada ya kutumika kwa muda mrefu na kuleta maendeleo mbalimbali katika jimbo la Moshi ikiwemo ujenzi wa shule pamoja na masuala ya kiroho. 

Habari kwa mujibu wa Gospel Kitaa

National ID - At last!

Hatimaye baada ya muda mrefu na danadana za hapa na pale Watanzania nao sasa kuwa na vitambulisho vya taifa lao, hii ni baada ya Rais Jakaya M Kikwete kuzindua rasmi vitambulisho hivyo hapo jana jijini Dar. Mradi huu unasimamiwa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA). Picha na Ikulu. 

Mv Victoria Chupu chupu kuteketea kwa motoMeli ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini(MSC)imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea sehemu mojawapo ya Meli hiyo.

Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zlizo patikana toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto ulipoangukia katika sehemu ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.

Hata hivyo moto huo ulithibitiwa na meli kuweza kuendelea na  safari zake kuelekea Bukoba kama kawaida. 

Google+ Followers

There was an error in this gadget
There was an error in this gadget

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...