July 10, 2008

AMKENI KWAYA

HII NDO AMKENI KWAYA. UZINDUZI WA KWAYA HII UMEKUWA GUMZO PENGINE KULIKO KWAYA NYINGINE ZOZOTE HAPA BONGO, NA HAPANA SHAKA UTABAKI KUWA KUMBUKUMBU KWA BAADHI YA WATU. KISA HASA ETI NI KUMWALIKA ROSTAM AZIZ
Posted by Picasa

Rostam azua balaa

AYA NDO YALINUKULIWA NA MDAU TOKA KINYWA CHA ROSTAM AZIZ MBUNGE WA IGUNGA AMBAYO IMEKUWA GUMZO HATA KUSABABISHA KUSIMAMISHWA KWA MTUMISHI ALIYEMWALIKA MFANYABIASIASA HUYU. Tuliombee Taifa – Rostam Aziz Asema watu wanachukuiana na kuombeana vifo Adai wanazushiana uchawi, anapakaziwa fisadi Aomba kanisa litumike kurejesha taifa katika mstari Dar es Salaam, Julai 6, 2008 MBUNGE wa Igunga, Bw. Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu kisiasa na kujamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari ulio sahihi. Bw. Rostam alitoa mwito huo Dar es Salaam jana katika hafla ya uzinduzi na kuweka wakfu albamu ya kwaya ya Amkeni ya Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo ambapo alikuwa mgeni rasmi. Alisema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki, na kwamba licha ya kashfa za ufisadi anazozushiwa, wamepuuza hilo na wamejenga imani kwake. “Nawashukuru kwa kuamua kunialika kuwa mgeni rasmi… ni ishara kwamba mmeamua kupuuza maneno na upuuzi wa vijiweni. Nafurahi kuwa miongoni mwenu…. hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii,” alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo. Rostam alisema watu wanachukiana mpaka kufikia hatua ya kuzushiana uchawi na kuombeana vifo. “Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi,” alisema. Rostam alisema licha ya matatizo ya kisiasa, kuna matatizo ya kijamii ambayo alisema ni ndoa kuvunjika kila kukicha, watoto wa mitaani kuongezeka, madanguro na dawa za kulevya kukithiri, mambo ambayo yanasababishwa na mmomonyoko wa maadili. Katika hafla hiyo ya kuweka wakfu kanda za video, kaseti na dvd, Mbunge huyo alitoa mchango wa sh. milioni 5 kuchangia seti za vyombo vya muziki kwa kwaya ya Amkeni pamoja na jenereta yenye thamani ya sh. milioni 2.6. Hiyo ni albamu ya kwanza ya kwaya ya Amkeni iliyodumu kwa miaka 24 sasa. Mwaka 2005, Rostam pia alishiriki katika harambee ya ujenzi wa jingo la Kanisa la KKKT Kinondoni ambalo kwa sasa linatumika kama Chuo Kikuu cha Tumaini. Mwisho…
Posted by Picasa

ZITTO ARUHUSIWA MNH

Mbunge Zitto Zuberi Kabwe (Kulia) akiwa na ndugu yake mara baada ya kuruhusiwa kutoka Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku mbili.
Posted by Picasa

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...