April 29, 2010

Utafit REDET wapondwa ama wapendwa???

Baadhi wakataa matokeo ya utafiti wa Redet
UTAFITI uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet) kuhusu uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu, umewasha moto miongoni mwa wabunge na wanasiasa, wengi wao wakiuponda huku wabunge wengi wakijiamini kushinda katika majimbo.
Wabunge na wanasiasa hao walizungumza jana na HABARILEO kwa nyakati tofauti, wengi wao wakionesha wasiwasi juu ya utafiti huo, huku wanasiasa wa vyama vya upinzani wakisema utafiti huo umetengenezwa kwa manufaa ya CCM.
source: HABARILEO
REDET poll wins applause
THE publication of the REDET opinion poll yesterday which gave the highest ranking to President Kikwete at the expense of his rivals was welcomed by both the ruling and opposition political parties’ leaders alike.
The ruling CCM which got the highest ranking in the poll ranking expressed optimism that the party will win the forthcoming general elections with flying colours. Opposition leaders also saw hope for their prospects in the poll findings which indicated that two thirds of the sitting MPs will lose their seats.
SOURCE: DAILYNEWS WADAU, MAGAZETI YOTE HAYO YANAMILIKIWA NA SERIKALI LAKINI MITAZAMO NDO TOFAUTI The CCM Deputy Chairman (Mainland), Mr Pius Msekwa, told the ‘Daily News’ in Dar es Salaam yesterday that the party respects scientific studies and that basing on the findings, he regards CCM as the obvious winner in this year’s general elections.

Yes I know!

“I know that my Redeemer lives, and that in the end he will stand upon the earth.”- Job 19:25

April 22, 2010

Snap toka Mjengoni

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wananchi kutoka jimbo la uchaguzi la Kondoa Kaskazini, ambao walitembelea Bunge, Aprli 22, 2010 kwa mwaliko wa Mbunge wao, Zabein Muhaji Mhita (wapili kushoto). Walikuwa kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

Mh Karamagi na Mh Kingunge Ngombale Mwiru wakichat.

Yalojili Makao Makuu leo..

Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi nchini balozi Athmani Mhina akimkaribisha makamu wa Rais Dk Ali Mohamed shein katika ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma ambapo Dk Shein alifungua mkutano Mkuu maalum wa Jumuia ya wazazi leo.

TTB Mpooooo? Tanzania, Botswana Top Africa Travel Destinations

Wakati Rais JK akimteua Mfanyabiashara wa Marekani na Ndugu wa Mwigiuzaji maarufu Brad Pitt, Doug Pitt kuwa Balozi wa Heshima wa Utalii Tanzania, Mtandao mmoja unaojihusisha na mambo ya utalii yaitangaza Tanzania kuwa Kinara kwa Utalii Africa. Wow hizi ni habari njema sana kwa Bongo na asa kwa ujio wa fainali za Kombe La Dunia huko Bondeni Mwezi Juni. TTB Changamkieni taarifa hizi na kuziuza kwa nguvu zote.

The results are in. The Fazendin Portfolio, a travel representation firm specializing in marketing African safari camps, lodges and safari outfitters, released the results of its first quarter 2010 African Travel industry survey.

What did they find? The selection of Tanzania and Botswana as top African travel destinations in 2010, a growth in online/social media in marketing African travel in 2010 and beyond, and a continued challenge in keeping up with and qualifying inquiries.

The results were gathered from surveys taken by travel agents and tour operators, over two-thirds of whom travel to Africa. The other top leaders include South Africa (tied with Botswana), Kenya and Zambia.

The most important factors for clients were camp guides/hosting and value for money. Green/eco-friendly operations did not appear to be particularly important.

When asked the greatest business challenge of 2010 thus far, respondents mentioned keeping up with the volume of inquiries. However they added that not all inquiries are serious and it makes it difficult to qualify and make the sale while being time efficient.

Visit www.fazendinportfolio.com.

April 21, 2010

Pamoja na nyongeza 100% Mgomo uko palepale - TUCTA

SERIKALI imepandisha kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi kwa asilimia 100, huku wafanyakazi wa Serikali na sekta ya umma, wakitakiwa kuvuta subira hadi Jumapili ijayo wadau watakapokaa kujadili.
Hata hivyo, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), limesema tamko hilo la Serikali ni siasa na msimamo wao hautarudisha nyuma nia ya wafanyakazi kugoma Mei tano mwaka huu, endapo madai yao makuu matatu hayatatekelezwa kabla ya Mei Mosi.
Katika madai hayo makubwa, Tucta wanaitaka Serikali iongeze kima cha chini cha mshahara, ipunguze kodi inayokatwa katika mishahara (PAYE) na kuongeza malipo yanayotolewa na mifuko ya pensheni.
Hata hivyo, msimamo huo wa Serikali na wa Tucta umetolewa wakati taarifa za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), zikionesha kuwa kiwango cha chini cha mshahara wa Tanzania ni kikubwa kuliko Kenya na Uganda.
SOURCE: Habarileo

Bunge larekebisha Sheria Gharama za Uchaguzi- JE KWATOSHA

Bunge limepitisha kwa kauli moja marekebisho ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya Mwaka 2010, baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, kuwasilisha bungeni muswada wa sheria unaopendekeza marekebisho ya sheria 16, ikiwamo sheria hiyo.

Hatua hiyo ilifikiwa jana na Bunge, zikiwa zimepita wiki chache tangu Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, kukaririwa na vyombo vya habari akilalamikia kitendo cha serikali kuingiza vifungu ndani ya sheria hiyo kinyemela.

Vifungu vilivyolalamikiwa na Dk. Slaa kwamba, viliingizwa katika sheria hiyo nje ya utaratibu wa Bunge, ni pamoja na vifungu vidogo vya 1, 2 na 3.

Dk. Slaa, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema, alisema vifungu hivyo viliingizwa katika Kifungu cha 7 baada ya sheria hiyo kujadiliwa na kupitishwa na Bunge, kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.

Kutokana na hilo, Dk Slaa, alitaka sheria hiyo irudishwe bungeni ili vifungu hivyo viondolewe mara moja.

swali!!

Wadau je kuingiza vifungu kinyemela na baadaye kushtukiwa lakini pamoja na kushtukiwa huko wakana na sasa waamua kuondoa vifungu ama kurekebisha tu kwatosha? hakuna makosa mahali fulani hapo? Je Mkuu wa Nchi hakudanganywa ama kuuziwa mbuzi kwenye gunia?

source:Nipashe

"they shall never perish"

Siku inakuwa njema sana uhamkapo na kupata ujumbe mzuri kama huu. ASANTE YESU.

“I give them eternal life, and they shall never perish; no one can snatch them out of my hand. My Father, who has given them to me, is greater than all; no one can snatch them out of my Father's hand. I and the Father are one.- John 10:28-30

April 20, 2010

Shy Rose uso kwa macho na Mtoto wa Mkulima

Mtoto wa Mkulima Mizengo Pinda akichat na Afisa Habari wa NMB na Mjumbe wa UWT DSM Shy Rose Bhanji ktk viwanja vya Bunge Dodoma hii leo.

Ray C akana kutapeli ughaibuni

Fuatilia mahojiano yake na Bongo5 hapa.

JK appoints Tourism Goodwill Ambassador

President Jakaya Mrisho Kikwete presents a Makonde carving to the newly appointed Tanzanian goodwill ambassador for tourism Mr.Doug Pitt during a special recognition ceremony held in New York.

April 19, 2010

JK akutana na boss wa ICC, Luis Moreno-Ocampo

President J Kikwete chats with The International Criminal Court Prosecutor Mr.Luis Moreno-Ocampo in New York when the later paid courtesy call on him this morning.

TAUSI BADO YUKO JUUUUU

Tausi Likokola lawezekana kuwa jina geni miongoni mwa watu lakini si geni kwa wengi wetu na hasa wanaofuatilia kwa karibu masuala ya mitindo na ulimwende hapa Bongo na Duniani kwa ujumla.
Tausi ni Mwanamitindo mzaliwa wa Tanzania ambaye amepiga hatua kubwa sana katika fani hii kimataifa kwa muda mrefu sana, pamoja na kuwa sasa ni mama wa watoto wawili lakini bado anapata mikataba na makampuni mbalimbali duniani kama vile Gucci, Christian Dior, Tommy Hilfger, Escada, NK.
waweza kumtembelea hapa au katika facebook ujionee zaidi.

April 16, 2010

NEC yatangaza majimbo mapya na ratiba ya uchaguzi 2010

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

“TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UGAWAJI WA MAJIMBO NA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU WA 2010”

1.Ugawaji wa Majimbo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ,Kwa mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,inawatangazia wadau wa Uchaguzi na Wananchi kwa ujumla kuwa itagawa Majimbo ya Uchaguzi yafuatayo.

i.Nkasi

ii.Tunduru

iii.Maswa

iv.Kasulu Mashariki

v.Bukombe

vi.Singida Kusini

vii.Ukonga

Taarifa zaidi kuhusu Majimbo hayo mapya yatakayoanzishwa itatolewa baada ya Tume kukutana na wadau wa Majimbo husika.

2. Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 Kwa mujibu wa Vifungu vya 37(1)(a) na 46(1) vya Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Vifungu vya 41(1) na 48(1) vya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ,Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawatangazia Wananchi wote kuwa Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 kwa Uchaguzi wa Rais, Bunge na Madiwani itakuwa kama ifuatavyo;

1. UTEUZI WA WAGOMBEA - 19 AGOSTI,2010

2, KAMPENI ZA UCHAGUZI -20 AGOSTI, HADI 30 OKTOBA,2010

3. UPIGAJI KURA 31 OKTOBA, 2010

Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi, Tume itawatangazia Wananchi rasmi, tarehe ya kutoa Fomu za Uteuzi kwa wagombea.

JAJI MSTAAFU LEWIS M.MAKAME MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

MKUKUTA DOM

Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo(R) akichat Katibu Mkuu wake Ramadhan Khijjah (c) pamoja na Naibu Katibu Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Clifford Tandari mara baada ya uzinduzi wa mchakato wa majadiliano ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania(MKUKUTA) ambazo zoezi hilo limeanza jana na linaendelea nchini kote.

April 15, 2010

JK yuko UN.

President Kikwete welcomes the Executive Director for the United Nations Population Fund(UNFPA) Dr.Thoraya Obaid in New York for official talks.

UN Secretary General Ban Ki Moon welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete for joint Press Conference shorlt after the conclusion of a special UN closed door meeting on improving Maternal Health Held at the UN Headqarters in New York this morning.

Mama Salma ziarani Kilimanjaro

Matukio mbalimbali ya ziara ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mkoani Kilimanjaro, pamoja na kuongea na wananchi alizindua miradi kadhaa na kukabidhi misaada kwa kituo cha afya pia.

Buriani mkutanoni Nairobi.

MKUTANO WA PILI WA MAWAZIRI KUHUSU UDHIBITI WA MAAFA KATIKA BARA LA AFRIKA, 14-16 APRILI 2010, NAIROBI, KENYA

Mhe. Dkt. Batilda S. Burian Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Mawaziri kuhusu Udhibiti wa Maafa katika Bara la Afrika, uliofanyika jijini Nairobi.

April 14, 2010

Tanzania Kids Soccer


Kids Soccer
Originally uploaded by Rwebangira
Love for soccer in Bongo is passionately followed from the very tender age, kids love it and enjoy playing at any open space available mostly with ball made of used plastic bags, papers string wrapped around it.

April 12, 2010

Rais na Msafara unapotekea kwa ghafla.- KINGA NI BORA ...

Waliondoka na furaha sana wakiwa na matumaini ya kurejea tena Poland, lakini haikuwa hivyo.
Rais wa Poland na Mkewe pamoja na msafara wake wote umeteketea katika ajari ya ndege iliyotokea mwishoni mwa wiki.
Rais Lech Kaczynski na Mkewe Maria pamoja na mkuu wa Majeshi, wabunge kadhaa pamoja na wanahistoria wote wameteketea ktk ajari hiyo, huu ni msiba mkubwa sana kwa taifa hilo.
Lakini je twajifunza nini kwa ajari hii? kuna somo lolote kwa viongozi wetu hapa??
Natumaini kuwa lipo jambo kubwa tu la kujifunza hapa, na kama lipo basi "Kinga ni bora kuliko tiba"

Kumbukumbu ya kifo cha SOKOINE leo

Leo ni miaka 26 toka Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Moringe Sokoine afariki kwa ajari ya gari huko Morogoro, kutakuwa na misa ya kumbukumbu ya kifo chake katika kanisa la Mt Joseph jijini leo jioni iliyoandaliwa na familia ya kiongozi huyo wa zamani mwenye kuheshimika sana nchini.
Nyote mnakaribishwa.

April 8, 2010

Mgombea Binafsi RUKSA?????

Serikali leo inatarajiwa kutoa sababu za msingi za kupinga mgombea binafsi kwenye Mahakama ya Rufaa ambako ilikata rufaa maamuzi ya Mahakama Kuu kuruhusu mgombea binafsi katika kesi iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa chama cha Democratic Party (DP) Christopher Mtikila.

Serikali ilikata rufaa Mahakama ya Rufaa mwaka jana ikipinga hukumu ya Mahakama Kuu Dar es Salaam iliyotolewa Mei 5 2006 katika kesi ya msingi namba 10 ya mwaka 2005 iliyofunguliwa mahakamani hapo na Mchungaji Mtikila Februari 17 mwaka 2005 akiiomba mahakama hiyo pamoja na mambo mengine iamuru kuwepo kwa mgombea binafsi.

Katika hukumu hiyo jopo la majaji watatu wa mahakama Kuu Dar es Salaam, jaji Amir Manento, jaji Salum Massati na jaji Thomas Mihayo, wakati huo walikubaliana na maombi ya Mchungaji Mtikila na kuruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi.

Hata hivyo serikali ilikata rufaa Mahakama ya Rufaa, ambayo ilitarajiwa kusikilizwa Februari 8 mwaka huu lakini iliahirishwa hadi leo baada ya serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali(Dag), George Masaju kuomba iahirishwe ili ipate muda zaidi wa kujiandaa katika kutoa hoja zake.

Wakati muda huo serikali ilipewa kujiandaa zaidi ukiwa ndio umemalizika na leo inakuja tena mahakamani, mahakama hiyo nayo kwa upande wake imekuwa ikichukua hatua madhubuti za kujiimarisha kujiongezea nguvu zaidi kwa kutafuta msaada zaidi wa kisheria kutoka kwa watalaamu wa mambo ya Katiba na sheria kwa jumla.

Jambo kubwa la kuvutia wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo ni kwamba leo itasikilizwa mbele makundi mawili yenye majopo ya majaji tofauti na awali kabla ya kuahirishwa.

Majopo hayo ni pamoja na jopo la majaji saba wa Mahakama ya Rufaa na jopo la wataalamu watatu wa sheria, wasio majaji wala mawakili, ambao kwa lugha ya taaluma ya sheria hujulikana kama marafiki wa mahakama (Friends of Court).

Jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa katika rufaa ya kesi hiyo hiyo ni pamoja na Jaji Mkuu mwenyewe Ramadhani ambaye ndiye kiongozi wa jopo la majaji hao akisaidiana na Jaji Eusebio Munuo, Jaji Januari Msofe, Jaji Benard Luanda, Jaji Mbarouk Mbarouk, Jaji Engela Kileo na Jaji Sauda Mjasiri.

Kwa upande wa jopo la marafiki wa mahakama ambao tayari wameitwa na mahakama hiyo kushiriki kwenye rufaa ya kesi hiyo ni pamoja na Profesa Kabudi Palamagamba na Profesa Jwani Mwaikusa ambao wote ni wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaa (UDSM).

Pamoja na maprofesa hao wawili wa UDSM, mwingine katika jopo hilo ambaye pia ameitwa na mahakama hiyo kushiriki katika usikilizwaji wa rufaa ya kesi hiyo ni Mkurugenzi wa mashtaka wa Zanzibar Othmani Masoud.

Katika barua za kuwaita kushiriki katika rufaa ya kesi hiyo Jaji Mkuu Ramadhani alisema ameamua kuwaita kushiriki katika kesi hiyo kutokana na umuhimu wa suala hilo kikatiba na kwamba kwa uzoefu wao katika mambo ya kisheria anaamini kuwa Mahakama hiyo itafaidika sana na ushauri wao kutokana na uzoefu wao katika mambo ya kikatiba.

Hoja ya kuwepo kwa mgombea binafsi imekuwa ikiungwa mkono na wadau mbalimbali wa siasa na utawala bora wakidai kuwa uamuzi huo utazidi kupanua wigo wa demokrasia nchini.

Jaji Mkuu Ramadhani pia kwa upande wake amewahi kukiri kuwa suala hilo lina umuhimu wa pekee na kwamba ni kutokana na umuhimu huo ndio maana aliamua kuteua jopo la majaji saba kusikiliza rufaa ya kesi hiyo.

SOURCE: MWANANCHI

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...