September 30, 2006

Wameondoka kisraarabu pasi na purukushani yoyote, ombi lao ni Serikali kuwapatia huduma muhimu na ulinzi, lakini pia twaomba kuhakikisha pasiwepo na zoezi lingine kama hili hapo siku za usoni, au hii isiwe nguvu za soda.
Wengi walio kuwa mtaa wa kongo wamehaia mchikichini kuanza maisha upya....
Mtaa wa Msimbazi ukiwa tupu.
Kwa amani kabisa wamachinga wametii mamlaka na kuamua kuondoka maeneo yasiyo ruhusiwa kwende wanakopaswa, kinyume na matarajio ya wachache waliodhani au kuomba damu imwagike. Tz ni nchi ya amani kweli.
Japo siku 180 zaweza onekana nyingi lakini si nyingi hata kidogo kwa jambo lolote kufanyika kama ilivyokuwa kwa wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga. kwa aliye pita Mtaa wa kongo au kariakoo wiki moja iliyopita hawezi amini macho yake akipita leo.

September 20, 2006

....ni ajabu na kweri kabanda haka ndo kamemuhifadhi Shabani Kissu wa TVT wakti akirusha matangazo moja kwa moja hii ndo hali halisi ya Ukumbi wetu mpya.
....hata uwezi ona kinachoendelea waliko wabunge, kwa sisi wapiga picha ndo kabisa ......ndo maana jamaa sometime wanaamua kuchat tu.
Naendelea kuwaletea kwa njia ya picha ukumbi mpya wa bunge letu tukufu Tanzania, pamoja na uzuri wote kasoro hazikosi, moja ni upande wa waandishi ni kama hatukutakiwa kuwepo, mbali na lango letu la kuingilia kufichwa uani (kwani kila kada ina lango lake), pia.............

September 17, 2006

Watoto wa Dom ushinda wakishangalia kwa nje wakitamani bila shaka kuingia lakini hili jipya halina nafasi kwao, hata wananchi wanaotaka kufatilia bunge..... no way.
Hii ni dhahabu au? JK aoneka aamini,,,,,,
Ndani ni mduara na viti vya kunesanesa......
Pengine ni Bahati kwa Tz na hasa kinamama kwani mgeni wa kwanza toka nje kutembelea ni Mwanamama Rais wa Ireland Bi Mary McAleese. Hapa pamoja na JK wakati wa gwaride la heshima.
Kwa jinsi mandhali ya inavyovutia kila afikae ataka apete kumbukumbu.
Manthali ni ya kuvutia maua chekwaaaaa.
Ni wachache hadi sasa wamepata bahati ya kuona au kuvinjari Jengo la Bunge Tukufu la Bongo na kwa mlio ughaibuni ndo kabisa, kwa kupitia picha mtavinjari japo kiduchu. Hili ni lango la kuingilia Waheshimiwa tu.
Pamoja na utandawazi na salon za kisasa bado mzee huyu anapeta na wembe chini ya mti katikati ya jiji la Dar.
Elimu ni muhimu sana na ni uridhi pekee anaochiwa mtu na usipotee, binti akipitia masomo wakti akielekea shule.

September 14, 2006

Bongo Pix Blog 1st Post

Picha hii ilipigwa siku moja kabla kifo cha Pope John wa Pili. Nachukua nafasi kuwakaribisha wote ktk blog hii ya Bongo pix. Kama jina linavyojieleza ni ya picha za wabongo ambazo zimepigwa kiubunifu na utaalmu.Naomba ushirikiano wa kila mmoja wenu, mliotanguli ktk blog na watoa maoni pamwe na wasomaji. una huhuru kutoa mawazo yako kwa picha yoyote kwa lugha nzuri na ustaarabu na si lugha chafu. kwa wanaojua kusoma picha karibuni mshauri, kukosoa, na kuelimisha picha kama imefanikiwa au haikufanikiwa kufikisha ujumbe tarajiwa.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...