September 9, 2011

Website ya Taifa kunani?????


Nilikuwa najaribu kufungua website ya Taifa ktk www.tanzania.go.tz  lakini hilo ndilo linaloonekana baadaya kufunguka kwa sekunde ka moja hivi, Je wataalamu wetu wamaligundua hili?

Watuhumiwa wa Mihadarati ya Bilion 4 wafikishwa kwa pirato

Raia wa Iran, Ali Mirzaei Pirbaksh (kushoto) na Watanzania wanne, Abdul Mtumwa (wa pili kushoto) akifuatiwa na Aziz Juma, Said Mashaka na Hamidu Kitwana wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kusomewa mashitaka ya kukutwa na Kilo 97 za dawa za kulevya aina ya Heroine eneo la Africana Mbuyuni Dar es Salaam. 

Richard Masatu - kwanini aliuwawa kinyama?

Marehem Richard Masatu

Na Mwandishi Wetu.


Agosti 10, 2011, zilipatikana taarifa za kifo cha mwandishi wa habari Richard Masatu, kilichodaiwa kusababishwa na ajali ya gari. Hata hivyo uchunguzi wa daktari kuhusu kifo hicho ulibainisha kuwa Marehemu aliuawawa kinyama. Tangu kupatikana kwa taarifa hizo, Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limekuwa likificha ukweli kuhusiana na kifo hicho. Kwa sababu ya umuhimu wa tukio hilo la kusikitisha, gazeti hili limeanza kufanya uchunguzi ha hii ni taarifa yake ndogo ya awali. Endelea.

 SIKU chache baada ya jeshi la polisi mkioani Mwanza kushindwa kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa kifo cha mwandishi wa habari Richard Masatu (39) uchunguzi umebaini kuwa aliuawa kutokana na kufuatilia biashara ya madawa ya kulevya na sakata la noti bandia.

 Jinsi alivyouawa: Uchunguzi wa kina uliofanywa umebaini marehemu hakufa kwa ajali ya gari bali kwa kipigo ambapo inadhihirishwa na taarifa maalum ya uchunguzi wa Kitabibu iliyotolewa na daktari katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza, akitokea katika viwanjwa vya Nane nane Nyamhongolo akiwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Luninga cha Star TV (James George) alipitia katika Baa maarufu Igoma (Cross Park) na kukaa hapo kwa muda wa saba.

 Katika baa hiyo, pamoja na mwandishi wa habari ambaye alikuwa ameambatana na marehemu, pia alikuwa akinywa na watu mbalimbali wakiwamo maofisa usalama wa Taifa wilaya ya Ilemela (DSO Mugoma), mkuu wa kituo cha polisi wilaya Ilemela (OCD Allan Bukwimba), mkuu wa kituo cha Mwatex (OCS Abubakar).

 Imebainika kuwa Marehemu wakati akitoka katika baa hiyo majira ya saa 3: 35 alitekwa na wauaji hao kwa kuanza kushambuliwa na kitu kizito kichwani upande wa kulia ambapo kutokana na ulevi aliokuwa nao alishindwa kujimudu na hivyo kubebwa na wauaji hao ambapo walimkokoto hadi katika misitu ya Ndama kando kidogo ya barabara ya Mwanza Musoma na kuanza kushambuliwa na kudi la wauaji.

 Vituko baada ya kufariki: SIMU ya Mke wa Marehemu: Licha ya taarifa kusambaa kuwa marehemu alikuwa amepata ajali, wa kwanza kupingana na taarifa hizo alikuwa mwandishi wa Gazeti la Msanii na rafiki mkubwa wa Marehemu, George Nteminyanda ambaye baada ya kufika hospitalini na kumwangalia marehemu, alianza kumkagua kama anavyoeleza.

 “Nilipata mashaka, kwani mwili wake ulivyokuwa ukionekana na jinsi taarifa zilivyo elezwa nilipata wasiwasi, niliamua kumkagua kuona anamajeraha ya aina gani, nilianza kumgeuza Kichwa, upande kuangalia kichwani, hapa ndipo nilistuka kwani kitendo hicho kilimfanya kutokwa damu iliyoganda mdomoni” alieleza.

 Alisema baada ya kuona damu alilazimika kumfuata daktari wa wadi ambaye alimhoji ni kwanini marehemu hawakumrufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi kutokana na hali aliyokuwa nayo, lakini alidai kujibiwa kuwa alikuwa akiendelea vyema.

 “Niliambiwa na daktari kuwa hali yake ilikuwa inaendelea vyema na kwamba walikuwa wakingojea kuona hali yake inaimarika vipi baada ya dripi kumalizika. Basi sikuwa na la ziada lakini kwangu mimi ilinitia shaka sana,” alieleza.

 KUPOTEA kwa PF-3: Kutokana na hali iliyoonekana kwa Marehemu na mashaka juu ya kifo chake, familia iliomba mwili wake kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua sababu ya kifo chake.

 Kutokana na maelezo ya matabibu waliompokea Hospitalini usiku, maehemu alifikishwa hospitalini akiwa na fomu namba 3 ya Polisi (PF-3), ambapo ililazimu ichukuliwe na kupelekwa Polisi kwa ajili ya kuanza utaratibu wa kumfanyia uchunguzi (Postmortem), lakini fomu hiyo haikupatikana kama anavyoeleza Gelard Robert mwandishi wa habari aliyekuwepo katika ufuatiliaji wake hospitalini.

 “Tuliomba ipatikane PF-3 lakini kila daktari na muunguzi aliyekuwa akiulizwa hakuna aliyejibu wala kutambua kuwa ilikuwa wapi, basi haikuweza kupatikana na ndipo ofisa mmoja wa polisi aliposhauri kuwa lifunguliwe jalada jipya la uchunguzi ili mwili huo ufanyiwe uchunguzi ambapo lilifunguliwa jalada jipya hivyo kufanyiwa uchunguzi huo.

 Taarifa ya Uchunguzi wa Daktari: Kwa mujibu wa Taarifa ya uchunguzi wa kifo cha Masatu uliofanywa na Daktari chini ya wanafamilia na jeshi la Polisi umebainisha kile ambacho kinadhihirisha kuwa Marehemu aliuawa.

 
Kwa mijibu wa msemaji wa Kampuni ya Sahara Media Group Ltd, Raphael Shilatu kwa aniaba ya familia ya marehemu, wakati akizungumza katika msiba mjini Mwanza na Musoma, alisema uchunguzi wa kitalaam umethibitisha kuwa mwili wake ulikuwa na majeraha ya kushambuliwa.

 “Marehemu amefariki kutokana na kupigwa na kitu kizito kichwani ambacho kilisababisha kuvujia kwa damu ndani ya ubongo, ametobolewa jicho moja na kitu chenye ncha kali, alitobolewa chini ya kidevu, alivunjwa vunjwa kifua, mguu wa kushoto ikiwa ni pamoja na kupasuliwa bandama na pafu la kushoto” alieleza Shilatu.

 Mbinu zilizotumika kumnasa: Imebainika kuwa marehemu alikuwa akifuatiliwa na mwanamke aliyeandaliwa maalum na wauaji ambapo siku hiyo, walimtaka kukutana katika katika baa hiyo huku wakiwa wamejianda kwa ajili ya kumshambulia.

 Akiwa katika eneo hilo, bila ya kujua kuwa alikuwa akifuatiliwa marehemu alikuwa na mawasiliano maalum na mmohja wa wanawake watatu (majina yao yanahifadhiwa kwa sasa) ambao mmoja alikuwa akieleza na bayana kuwa alikuwa na makubaliano naye ya kustarehe naye na ndiye inaeaminika kuwa baada ya kuondoka alimpigia simu na ndipo alipoondoka na kushambuliwa.

 Uzushi wa ajali baada ya kushambuliwa: Huku duru za uchunguzi zikieleza kuwa baada ya kutekwa huko na kushambuliwa katika Msitu wa Ndama, wauaji hao walimtoa katika eneo la shambulizi na kumpeleka hospitali ya Mkoa ya Mwanza Sekou Toure moja kwa moja.

 Uchunguzi unabainisha kuwa wauaji hao walitaka kumtupa barabarani ili ibainike kuwa aliuawa kwa ajali, lakini kutokana na eneo hilo la Igoma kando ya Baa ya Ndama kuwa na watu wengi, walilazimika kumpeleka hadi katika hospitali hiyo ya mkoa huku wakijivika jina la wasamalia wema waliojidai kumuokota ‘baada ya ajali.’

 Sababu za kumpeleka Sekou Toure: Katika mpango wao kama nilivyoeleza awali, walipanga kumtupa barabarani, lakini baada ya kukwama waliamua kumpeleka huko, na sababu kubwa ikiwa ni kwamba katika hospitali hiyo hakuna utaratibu wa kundikisha majina, namba za magari ya wagonjwa wanaoingia kama ambavyo upo Bugando jambo ambalo lilisaidia wahusika kujificha.

 Kutambulikwa kwa kushambuliwa Masatu: Majira ya saa nne mkewe aliamua kumpigia simu mumuwe ili kujua angerudi saa ngapi nyumbani, lakini simu yake ilikatwa na baada ya muda aliapigiwa simu yake na watu ambao walijieleza kuwa wao ni wasamalia wema ambao walikuwa wamemuokota Marehemu katika maeneo ya Ndama akiwa amepata ajali ya gari.

 “Walinieleza kuwa wanampeleka Hospitali ya mkoa, ambapo nilijiandaa name kufika baadaye huko, nilikuta marehemu akiwa amelazwa na kuwekewa drip, hakuwa anaonyesha kuibiwa, kwani alikuwa na kila kitu, simu yake na pochi yake ya mkononi,” alieleza mke wa Marehemu. 

Duru za uchunguzi zinaeleza kuwa kutokana na marehemu kufuatilia biashara ya mihadarati, mkakati huo wa mauaji ulipangwa ukiwahusisha maofisa wa polisi, usalama wa Taifa na wanawake waliotumika kama chambo.

 Simu ya Mke wa Marehemu yatoweka: Siku moja baada ya marehemu kufariki, hali ilizidi kuwa tete huku tetesi zikizidi kuonyesha kuwa marehemu alikuwa ameuawa, kutokana na watu kuanza kufuatilia nyendo, mke wa marehemu Edda Ikologoti Masatu alieleza kuibwa simu yake ya mkononi ambayo waliombeba kama wasamalia wema waliitumia kumpigia kumfahamisha kuwa alikuwa apata ajali.

 “Siku ya kushambuliwa mume wangu sikuwa najua lolote, niliamua kumpigia simu ilipofika majira ya saa 4:00 kujua kulikoni hajarudi nyumbani, simu yake ilipokelewa na watu ambao walinieleza wamemuokota maeneo ya Ndama akiwa kapata ajali na walikuwa wakimpeleka Hospitali.

 Simu yangu ilikata, walinipigia kwa simu nyingine na kuniuliza niko wapi name niliwaeleza kuwa niko Nyakato Buzuruga, waliniomba nifike maeneo ya Stand ili wanipitie twende naye Hospitali, niliwaomba watangulie kwa vile kutoka kwangu hadi eneo ambalo walitaka nifike lilikuwa mbali na ulikuwa usiku,” elieleza.

 Akifafanua zaidi alieleza kuwa simu hiyo iliibiwa wakati wakiwa nyumbani ambapo siku hiyo katika kumbukumbu zake, alidai kuwa alikuwa ameiweka katika pochi yake na mkoba huo kumkabidhi mdogo wake Elizabeth Ikologoti lakini alipotaka kuitumia simu hiyo haikuwepo.

 “Imenipa hofu sana, japokuwa sijui kama imepotea tu kawaida au imepotea kutokana na njama za mauajia, sijui kwa kweli labda wanajua kuwa kwa vile walitumia simu hiyo kunipigia wakati wakinialifu kuwa wamemuokota ndiyo maana imepotea, yaani hata sielwe,” alieleza.

 Ushahidi wa mazingira: Kuna taarifa za ndani kutioka kwa watu waliokuwa na marehemu siku hiyo kiziwataja maofisa hao wa polisi na usalama wa Taifa kuwa walikuwa na wahusiano na wanawake watatu waliokuwa wameandaliwa kama chambo katika eneo hilo la baa.

 Wakiwa hapo mmoja wa vijana ambaye alidaiwa kuwa ni mmoja wa wasaidizi wa karibu wa maofisa hao wa usalama, alifika na kueleza ametoka katika msitu wa Ndama kufuatilia mdeni wake jambo ambalo linaonyesha kuwa kauli hiyo ilikuwa ikimaanisha (Ishara) kuwa eneo la mauaji lilikuwa limeandaliwa na kuwa tayari kwa kazi ya uuaji.

 Moja. Ukweli, eneo la Msitu wa Ndama ni pori ambalo mchana limekuwa likitumika kwa shughili za kulisha mifugo inayouzwa mnadani hivyo usiku lisingeweza kuwa na watu hivyo kutia shaka na madai ya kuwa ‘Mtu alikuwa ameenda kumfuatilia mdeni wake’.

 Mbili. Mmoja wa watu waliokuwa hapo aliamuaga afisa usalama akitaka kutumia nafasi hiyo kumsindikiza marehemu kutokana na kuona amelewa alizuiliwa na afisa huyo kwa madai ya kuwa amwache kwa maana ya kwamba ‘Huyu atasafilishwa na serikali leo kwani yuko kazini’. Kutokana na hali hiyo inaonyesha wazi kuwa mpango wa mauaji ulikuwa ukitambulika. 

Tatu: PF-3 iliyopotea ilifunguliwa katika kituo cha Polisi cha Mwatex na mkuu wake wa kituo ni mmoja wa maofisa usalama ambaye alikuwa akinywa pale baa na mwandishi huyo, hii inatia shaka mazingira haya.

 Wauaji wakodiwa toka Bariadi: Ingawa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja lakini duru za uchunguzi zimebainisha kuwa wauaji hao ambao idadi yao inaaminika kuwa ni kundi la watu wasiopungua 6, inasemekana kuwa baada ya kukamilisha shambulio lao waliondoka wakiwa katika gari la polisi hali ambayo ilwafanya kupita kwa urahisi bila ya kujulikana.

 Uchunguzi huru: Kulingana na mambo haya jeshi la polisi halitoweza kufanikiwa katika uchunguzi huu kutokana na bnaadhi ya maofisa wake kuonekana kujihusisha na mauaji hayo.

 Kukwama kwa uchunguzi wa jeshi la polisi mkoani Mwanza kunadhirishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Liberatus Baro kutoa taarifa kuwa jeshi lake bado halijafanikiwa kunasa wahusika wa mkasa huo hatua ambayo inakwenda sambamba na kuachiwa kwa baadhi ya watu wawili ambao walishikiliwa siku moja baada ya mauaji hayo pia kuachiwa huru.

 Kutokana na polisi kutuhumiwa na kuhusika njia pekee ya kufanikisha uchunguzi huo ni kuwa na timu huru ya uchunguzi ambayo inaweza kusaidia kufichua mauaji hayo ya mwandishi wa habari.

From Swahili time Blog, 
Source: Dira ya Mtanzania (Jumatatu Septemba 5-7, 2011)

Mwisho wa Tanesco umekaribia???


Serikali yaridhia sekta binafsi kwenye umeme


KATIKA  kukabiliana na tatizo la ukosefu wa umeme wa uhakika nchini, serikali imekusudia kufanyia marekebisho sheria ili kuwaruhusu watu na taasisi binafsi kuzalisha na kuzambaza umeme bila kuupitishia Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO).

 Hayo yalisemwa jana jijini Arusha na Waziri wa Fedha na Uchumi , Mustafa Mkulo, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Bilali, kufungua mkutano wa 20 wa magavana wa nchi za Afrika, unaojadili tatizo la ajira kwa vijana na matumizi ya fedha za maendeleo zinazotolewa na wafadhili.

 Alisema kuwa sheria hiyo itapelekwa bungeni kwenye kikao cha Novemba ambapo kama wabunge wataridhia mabadiliko hayo, yatawezesha  umeme kusambazwa maeneo mengi hasa ya vijijini  jambo litakalosaidia kupunguza wimbi la vijana kukimbilia mijini kutafuta ajira kwani wataweza kuendesha shughuli za kujiajiri.

 “Kuna taasisi na kampuni ambazo zinazalisha umeme wao na mwingine mwingi wa ziada  unabaki lakini wanashindwa kuusambaza hata kwa majirani zao kutokana na sheria ya sasa hairuhusu  lakini tukibadilisha sheria ya sasa, wengine watajitokeza kuzalisha na kusambaza kwa wananchi hivyo kupunguza tatizo, ” alisema Waziri Mkulo.

 Alisema kuwa tatizo la ajira kwa vijana lililopo barani Afrika na hapa nchini linaweza kutatuliwa endapo kutakuwa na mkakati wa pamoja kuhakikisha kuwa vijana hao wanapatiwa elimu ya kuwawezesha kujiajiri mara baada ya kumaliza masomo, badala ya kusubiri kuajiriwa, hivyo alivitaka vyuo vikuu kuhakikisha vinabadili mtazamo na kutoa elimu itakayowawezesha vijana kujiajiri  mara baada ya kuhitimu mafunzo.
“Kwenye bajeti ya mwaka huu tumeitengea fedha nyingi  Wizara ya Elimu na Mafunzo ili iweze kuboresha vyuo vya ufundi  stadi (VETA) pamoja na  SIDO (Shirika la Viwanda Vidogo) ili kutoa mafunzo ya ufundi  kwa vijana yatakayowawezesha kujiajiri,” alisema Waziri Mkulo.

 Katika kuwahakikishia soko la bidhaa zinazozalishwa na vijana kupitia ufundi, alisema kuwa serikali ilishapiga marufuku  watendaji wake kuagiza  samani kutoka nje ya nchi na badala yake wanunue zile zinazotengenezwa hapa nchini lakini wanunue zilizo na ubora unaokubalika.

 Aidha aliwataka wananchi  wenye uwezo kujitokeza kuliendesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ubia na serikali katika kutekeleza sera ya ushirikiano wa sekta binafsi na umma (PPP)  ili kuongeza ajira  hasa kwa vijana, huku akisisitiza kuwa jina halitabadilishwa.Uenda hii ikawa faraja kwa walio wengi. tusubiri tuone. 

Darasa letu katika karne ya 21 na miaka 50 ya kujitawalaTafakari na Mjengwa
- Hiyo ni shule ya msingi katika Tanzania yetu ya leo.
- Huyo ni  mwanafunzi anayeingia darasani na mbele ni walimu wa shule wanaoingia darasani kufundisha.
- Hao ni wanafunzi darasani
- Na shule ina tundu moja la choo.
Ni miaka 50 baada ya Uhuru wetu. Tafakari.


Mkapa awasili Igunga


 Msafara wa Rais Mstaafu Ben Mkapa ukikatiza katika mji wa Igunga
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amewasili Igunga tayari kwa uzinduzi wa Kampeni kumnadi mgombea wa CCM Bw Kafumu.

CHADEMA yazindua kampeni Igunga Mgombe ubunge kupitia CHADEMA Joseph Kashindye akimwaga sera


KATIKA siku ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga, jana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitikisa mitaa na vitongoji vyote, huku mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, akitangaza rasmi kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) ni janga la kitaifa.

 Uzinduzi huo ulianza kwa maandamano yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa wafuasi wa CHADEMA walioupamba kwa vifijo na nderemo, kuanzia saa 9.20 alasiri, wakiongozwa na magari, baiskeli na pikipiki zilizopambwa na rangi za bendera ya CHADEMA.

 Viongozi wakuu wa chama hicho, akiwamo Mbowe, Dk. Willibrod Slaa, na wabunge wa CHADEMA walipokelewa na umati wa wana Igunga na kuongoza maandamano yaliyoanzia kijiji cha Hanihani hadi Uwanja wa Sokoine, ulikofanyikia mkutano mkubwa wa hadhara.

 Msafara wa CHADEMA ulisababisha baadhi ya wananchi kuacha shughuli zao kwa muda wakajiunga na maandamano hayo huku wakikishangilia chama hicho.

 Baada ya uwanjani, zilianza dua kutoka kwa viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, kabla ya viongozi kuanza kusalimia wananchi.

 Mbunge wa Mbeya Vijijini, Joseph Mbilinyi (Sugu), alikuwa kivutio kikubwa jukwaani na kushangiliwa kwa nguvu alipokuwa akitoa salamu kwa wananchi.

 Katika hotuba yake, Slaa aliwaambia wananchi kwamba CCM imewadharau wananchi wa Igunga kwa kumtuma Rais mstaafu Benjamin Mkapa kuzindua kampeni zake, kwani naye ni gamba ambalo CCM inapaswa kuachana nalo kama ilivyofanya kwa Rostam Aziz aliyejiuzulu ubunge wa Igunga kwa shinikizo la makundi ndani ya chama chake.
 

Alisema Mkapa naye ni fisadi, kwani alipokuwa Ikulu alifanya biashara katika ofisi hiyo ya umma bila kulipia pango na alishiriki ufisadi mkubwa unaowafanya wananchi waishi maisha ya shida.

 Aliwataka wana Igunga kumchagua mgombea wa CHADEMA, Joseph Kashindye, na kumpuuza wa CCM, Dk. Peter Kafumu, kwani huyu wa CCM hawezi kuwatetea, maana anaogopa kuanika udhaifu wa serikali yake inayotafuna mabilioni ya fedha kwa manufaa ya wachache.

 Dk. Slaa alisema Rais Mkapa ni miongoni mwa vyanzo vya uhaba wa umeme uliopo hivi sasa, maisha magumu kwa wananchi na matatizo lukuki yanayowakabili Watanzania; akawataka wananchi wambane kwa maswali magumu atakapopanda jukwaani leo kumnadi mgombea wa chama hicho tawala....

Source  Tanzania Daima
Picha kwa hisani ya Mitandao

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...