September 19, 2011

Kwanjuka ya AIRTEL yafikia tamati, washindi wakabidhiwa zawadi.


Afisa Mawasiliano  wa Airtel Tanzania Bi. Dangio Kaniki akikabidhi mfano wa hundi kwa  mshindi wa promosheni ya KWANJUKA Padri Isaya Gowa wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge wakati wa droo ya mwisho ya promosheni hiyo iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar es salaam, Katikati ni Meneja Uhusiano Jackson Mmbando 

Mtoto wa Mkulima at Mwitongo

Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwa na Mama Maria Nyerere mara baada ya kufika kijijini Mwitongo, WM yuko ziara ya kikazi Mkoani Mara.

No comment!

Sijui kwanini nimeiweka hii, naomba msaada wako!

Ulinisaliti wewe au gamba??


Unataka sifa??


Igunga kumekucha, Mabalozi CCM wanaswa wakiandikisha wapiga kura.


Nghoboko Masele aliyejitambulisha kama balozi wa nyumba kumi kumi wa CCM, katika kijiji cha Mwayunge Mashariki Kata ya Igunga, akiwa chini ya ulinzi baada kukamatwa na wafuasi wa chadema akiorodhesha majina na namba za shahada za wapiga kura pamoja na namba za simu zao katika jiji hicho.jana. Picha na Fidelis FelixWAKATI joto la uchaguzi mdogo wa Jimbo a Igunga likiendelea kupanda, Chama cha Wananchi (CUF) kimekituhumu CCM kuwa kimeanza kukusanya na kuorodhesha kadi za wapiga kura na kwamba, kimemkamata mmoja wa mabalozi wa nyumba kumi wa CCM wakati akifanya kazi hiyo.
 
Tuhuma hizo dhidi ya CCM zilitolewa jana na mgombea wa CUF, Leopold Mahona, ambazo tayari zimeshapingwa na Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba.
 
Akiwa katika kijiji cha Imalilo, Kata ya Nguru, jimboni humo, Mahona alisema kazi kuorodhesha majina ya wapiga kura na kadi zao inaratibiwa na kusimamiwa na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM.
 
Mahona aliwataka wakazi wa kijiji hicho kukataa mpango huo kwa kutotoa vitambulisho vyao vya kupigia kura, kwani wakikubali kufanya hivyo watashindwa kuchagua mwakilishi mwenye uwezo wa kuwasaidia.
 
Kauli ya Mahona imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa CUF Taifa,  Profesa Ibrahimu Lipumba, kuwataka wakazi Igunga kujiandaa kukabiliana na hujuma zinazotarajiwa kufanywa na CCM kwa lengo la kulazimisha ushindi, kutokana na chama hicho kupoteza mvuto kwa wananchi.
 
"Wakija kuwaomba shahada kataeni, hata wakiwatisha msikubali, mkae kimya na msiwafanye chochote. Subirini siku ya kupiga kura na mnichague mimi nikaletee maendeleo,’’ alisema Mahona.
 
Mahona alidai kuwa, wajumbe hao wanawatisha wakazi wa jimbo hilo wanaounga mkono upinzani na kulaani kuwa, kitendo hicho kinakwamisha maendeleo na juhudi za mabadiliko ya kidemokrasia.
 
Hujuma sehemu mbalimbali
 
Wakati mgombea huyo wa CUF akilalamikia kitendo hicho, mwandishi wa habari hizi imeshuhudia tukio la uandikishaji kadi hizo ukiendelea katika maeneo mbalimbali.
 
Mwandishi alishuhudia kijana mmoja, mkazi wa kata ya Iborogero, nje kidogo ya mji wa Igunga akiorodhesha majina ya wenye vitambulisho vya mpiga kura pamoja na namba za vitambulisho vyao vya mpigakura.
 
Kijana huyo alipoulizwa na Mwananchi, huku akisita kutaja jina lake, alisema kazi hiyo amepewa na wakubwa wake ambao alikataa kuwataja na kusisitiza kuwa, anachofanya ni kuorodhesha majina ya wapiga kura na vitambulisho vyao kupigia kura kisha kuviwasilisha kwa wakubwa.
 
‘’Mimi kazi yangu kukusanya taarifa za watu wenye vitambulisho vya mpigakura. Ninaandika majina yao pamoja na namba ya kitambulisho nawasilisha kwa wakubwa, wao watatoa maelekezo na hatua za kuchukua,’’ alisema kijana huyo.
 
Mmoja watu waliotoa kadi zao, Chiristina Kaloli, mkazi wa Iborogero alipoulizwa na gazeti hili alikiri kuwa, kadi yake imeishaandikishwa mjumbe wa CCM huku kusisitiza kuwa hiki ni kipindi cha mavuno kwao.
 
Kadi hiyo ambayo mwananchi iliona kumbukumbu zake Ikiwa na namba 05262605 inaonyesha kuwa, ‘Chritina Kaloli alijiandikisha kuwa mpiga kura Desemba 26, 2004 katika Shule ya Msingi Mpogoro, Wilaya ya Igunga’.
 
CCM wakanusha
Mratibu wa kampeni wa CCM, Nchemba alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alisema ni kitu kisichoweza kufanywa na CCM.
 
"Hivyo vyama vingine vinatapatapa, sisi ndio wenye wanachama wengi Igunga, tukifanya hivyo tutakuwa tunapunguza wapiga kura wetu, hatuwezi kufanya hivyo bali wao,’’ alisema.
 
Alisema kitambulisho ni mali ya mwenye nacho na kwa mujibu wa sheria za nchi, hakuna mtu anayeruhusiwa kuchukua kitambulisho cha mtu mwingine.
 
Nchemba alisisitiza kuwa, suala la kukusanya vitambulisho vya wapiga kura linaw....
ifuate hapa.

JK awasili New York.


JK akisalimiana na Maura Mwingira, mmoja ya maafisa ubalozini. 
JK akisalimiana na Dkt Rachel Mhaville ambaye ni daktari bingwa wa meno ya watoto, kwa mbaali anaonekana Mkumbwa Ali, Kaimu Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers ltd, wachapishaji wa magazeti ya serikali, Daily News na Habari leo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili amewasili New York, Marekani kuhudhuria Kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) na kushiriki katika mikutano mingine ya viongozi wa nchi na Serikali yenye maslahi kwa Tanzania na Afrika.Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, Mheshimiwa Rais Kikwete asubuhi ya leo,  Jumatatu, Septemba 19, 2011, atashiriki mkutano wa ufunguzi wa UNGA wa viongozi wa nchi na Serikali utakaojadili “Jinsi ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyokuwa ya Kuambukiza (Prevention and Control of Non-Communicable Disease) ambayo ndiyo mada kuu ya majadiliano ya Baraza Kuu la UN mwaka huu. Rais Kikwete leo  pia atakuwa Mwenyekiti wa mkutano wa waandishi wa habari kuhusu Maendeleo ya Umoja wa Viongozi wa Afrika Kupambana na Malaria (African Leaders Malaria Alliance - ALMA) ambao yeye ni mwenyekiti.Pamoja naye katika mkutano huo, miongoni mwa waalikwa wengine, watakuwa marais Paul Kagame wa Rwanda na Goodluck Jonathan wa Nigeria, na Rais wa zamani wa Marekani Mheshimiwa Bill Clinton. Rais Kikwete pia leo atashiriki katika Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Rais Clinton ya Clinton Global Initiative, na atahudhuria mkutano maalum wenye mada ya Putting Teeth into Non-Communicable Disease unaondaliwa kwa pamoja na Tanzania, Australia na Sweden.Baadaye jioni atakuwa msemaji mkuu katika hafla ya viongozi ya nchi na Serikali kusheherekea mafanikio ya muongo uliopita ya kupambana na ugonjwa wa malaria ulioandaliwa na taasisi ya Roll Back Malaria. Miongoni mwa watakaohudhuria halfa hiyo ni Naibu Katibu Mkuu wa UN, Mheshimiwa Asha Rose Migiro. Jumanne, Septemba 20, 2011, Rais Kikwete atashiriki katika mkutano wa viongozi wa nchi na Serikali kuhusu Lishe na baadaye mchana atajiunga na Katibu Mkuu wa UN, Mheshimiwa Ban Ki Moon kushiriki katika hafla ya viongozi iitwayo “Every Woman, Every Child Leaders Event”. Mchana, Mheshimiwa Rais Kikwete atashiriki katika tukio maalum la kujadili mikakati ya kimataifa kuhusu afya ya akinamama na watoto ya Global Strategy for Women’s and Children’s Health.Asubuhi ya Jumatano, Septemba 21, 2011, Rais Kikwete atashiriki katika ufunguzi wa majadiliano ya mada kuu ya UNGA mwaka huu, pia atashiriki katika mjadala kuhusu hali ya chakula wa Beyond Food Security, na vile vile atashiriki katika mkutano wa viongozi wa Social Good Summit ambako atapewa tuzo maalum kutoka Umoja wa Mataifa kwa mchango wake mkubwa wa kuimarisha afya ya akinamama na watoto.Baadaye mchana, Rais Kikwete atashiriki katika chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mheshimiwa Ban Ki Moon kwa ajili ya viongozi wote wanaoshiriki katika mkutano wa 66 wa UNGA, na pia atashiriki katika tukio jingine kuhusu afya ya akinamama lililoandaliwa na Soko la Mitaji la NASDAQ.Baadaye jioni ya siku hiyo atahudhuria hafla iliyoandaliwa na Rais Barack Obama wa Marekani kwa ajili ya viongozi wanaoshiriki mkutano wa mwaka huu wa Baraza Kuu la UN.Asubuhi ya Alhamisi, Septemba 22, 2011, Rais Kikwete atahutububia UNGA akiwa msemaji wa pili wa siku hiyo baada ya nchi ya Cyprus, shughuli ambayo itafuatiwa na shughuli nyingine nyingi za mikutano na viongozi ukiwamo ule wa kuadhimisha miaka 10 ya Azimio la Durban kuhusu ubaguzi wa rangi. Ijumaa, Septemba 23, 2022, Rais Kikwete atashiriki katika mkutano wa viongozi wa nchi na Serikali juu ya usalama wa nguvu za nyuklia wa Nuclear Safety and Security.

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...