Mwanamuziki wa kizazi kipya TID au Khalid Mohamed akiwasili mahakama kuu kueleza nia yake ya kukata rufaa kifungo cha mwaka mmoja alichohukumiwa yapata miezi minne iliyopita.
Pia alisema ni vema jamii ikafahamu kuwa Msanifu wa Serikali alifanya utafiti wa jengo hilo na kubaini kuwa ni chakavu na hatari kwa maisha ya binadamu.“Pia QGL inatoa nafasi kwa serikali kufanya tathmini ya uamuzi wake ya kwamba jengo lijengwe upya, au likarabatiwe na kuachwa kama sehemu ya makumbusho ya kihistoria. “Na kama uamuzi utaridhia jengo la Salamander libomolewe, QGL inakusudia kujenga jengo jipya la ghorofa 22 katika eneo hilo. “Kwa upande wa pili, kama uamuzi wa serikali ni kuliacha jengo hilo kama lilivyo, QGL inaheshimu uamuzi huo wa serikali na kuomba kurejeshewa malipo iliyofanya pamoja na gharama nyingine,” alisema Manji.