October 28, 2009

Mchakamchaka, mazingaombwe yangalipo shuleni siku hizi??

"Jua lilee literemke mamaaa, mwezi naoo utelemkee mamaaa haiyahiyaa hiyaa hiyaaa mamaaaa.............." Je wakumbuka nyimbo gani za mchakamchaka za enzi zile? au ni nini wakumbuka katika miaka ya sabini na themanini shule za msingi na sekondari? Wakti ule tulikuwa ukifika shule tu mwakimbia mchakamchaka na kuimba nyimbo kibao hivi bado yafanyika hayo?? Nakumbuka wakti tuko Sekondari Jite Best kulikuwa na mwalimu mmoja anaitwa GB alikuwa anakuja saa kumi na nusu na kugonga kengere na kiboko mkononi, ole wako ubakie bwenini ujifanye ujasikia, hizo bakora zake ni balaa, hivi vingalipo hivi?? Mazingaombwe mwayakumbuka??? wale wakongo walikuwa wanajifanya wanatengeneza pesa, vitambaa, kalamu, NK na ilikuwa unalipa kiingilio na mwatangaziwa shule nzima siku hiyo HAKUNA MASOMA, hivi waliishiaga wapi wale?? Mdau ni kitu gani wakumbuka???

4 comments:

Sophiasclub said...

Imebidi nicheke maana umenikumbusha mbali,yaani huwa nikifikiria heka heka hizo za mchakamchaka na kadhalika najiuliza hivi tuliwezaje kusoma hizo shule na kuzimaliza?! Kweli jitahada na uvumilivu ni vitu muhimu!

Yasinta Ngonyani said...

Hata mimi nimecheka sana kwa kufurahi kuona bado kuna watu wanakumbuka nyimbo hizi. Ngoja nami nimekumbuka hii Iddi amin akifa mimi siwezi kulia nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba

Anonymous said...

Sio siri umenikumbusha mbali saaaana yaani hakuna kitu nilikuwa sipendi ka mchakamchaka saa kumi na moja na kiwinta cha Moshi, yaani we acha tu.

Anonymous said...

Panda mlima panda, panda.... Si mchezo ilikuwa safi lakini. Ndhani shele za mijini mchaka mchaka hakunaga tangu siku hizo

Google+ Followers

There was an error in this gadget
There was an error in this gadget

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...