February 19, 2009

Jukwaa lakubali yaishe..

JUKWAA la Wahariri Co Limited limetangaza kumfungulia Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni George Mkuchika baada ya kugoma kuandika habari zake kwa takribani miezi minne sasa.

“Tayari gazeti liko mitaani, tunatangaza kumfungulia Mkuchuka. Lakini pia tunalaani kitendo cha kutumia sheria mbovu kuvifungia vyombo vya habari,” alisema mwenyekiti wa jukwaa hilo Sakina Datoo. Hata hivyo jukwaa hilo lilikishambulia kituo cha televisheni cha ITV kuwa kilifikia hatua ya kurusha habari za waziri huyo hasa baada ya Mkuchika mwenyewe kuzungumzia habari zinamlinda mmiliki wa kituo hicho Reginald Mengi.

Liyumba atoweka????????

Wadhamini wa mshitakiwa Amatus Liyumba, Benjamin Nguluguni (kushoto) na Otto Agaton, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo baada ya kukamatwa kwa kukosekana mshtakiwa Liyumba.
DHAMANA aliyopewa Amatus Liyumba imeingia dosari baada ya mahakama kutoa amri ya kukamatwa pamoja na wadhamini wake, lakini juzi na jana alisakwa na maafisa wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) lakini hakuonekana.

Alitakiwa apandishwe mahakamani jana, lakini badala yake maafisa wa takukuru waliambulia kuwakamata wadhamini na wakakiri mahakamani hapo kuwa Liyumba haonekani. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi ilitoa hati ya kukamatwa kwa Liyumba ikiwa ni siku moja tu baada ya kupewa dhamana na mahakama hiyo katika mazingira ambayo hayakuwaridhisha upande wa mashitaka. Hakimu Hadija Msongo jana alikiri kuwa mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamtwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake. Hata hivyo hakueleza sababu ya mahakama kutoa hati hiyo kwa kile alichodai kuwa jalada la kesi hiyo tayari limepelekwa mahakama kuu. Ifate hapa baadaye.

Dk Kitine: AZOZA.

Dk Kitine: Nchi iko hatarini

MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Makete na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), katika serikali ya awamu ya tatu, Dk Hassy Kitine ameonya kwamba, uchafu na wizi mkubwa wa rasilimali za taifa, mustakabali mbaya wa kisiasa na hali ngumu ya uchumi vinavyoikabili nchi, vinahatarisha usalama wa taifa.

Kauli ya Dk Kitine ambaye alishika wadhifa huo wa Ukurugenzi katikaIdara ya Usalama wa Taifa, wakati serikali ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imetolewa wakati nchi ikiwa imegubikwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya ufisadi na vita ya chini kwa chini ya kugombea madaraka.

Akizungumza katika mkutano maalumu na baadhi ya vyombo vya habari katika mgahawa wa Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam jana, Dk Kitine alionya kwamba, uchumi na maliasili za taifa zimeshikwa na wageni, huku Watanzania walio wengi wakifanya kazi za udereva, ufagiaji barabarani, kazi za ndani na mashambani. "Nimewaiteni kuzungumzia mustakabali wa nchi yetu, kama mnavyofahamu mimi nimeshika nafasi mbalimbali nyeti kuanzia wakati wa Mwalimu," alifahamisha. ICHEKI HAPA.

KP NA WENYE NACHO

Hakika WENYE NACHO ndipo walipoifikisha taaluma ya uandishi wa habari hapa nchini.

Je kwa stahili hii tutafika kweli????????????????????

Asante KP, Ujumbe umefika

.

Liyumba atoweka??????

Kuna taarifa kuwa Mtuhumiwa wa KESI YA Ujenzi tata wa minara miwili ya BOT A. Liyumba ametoroka na ajulikani alipo na kuwa wadhamini wake 2 wanashikiliwa na polisi kuhusiana na hilo.
Jana mawakili wanaomtetea Liyumba toka Amacus Attorneys Hudson Ndusyepo na Onesmo Kyauke (R) walithibitishia waandishi kuwa mteja wao alipewa dhamana licha ya kutotimiza masharti pamoja na kuwasilisha mahakamani hati ya kusafilia iliyopitwa muda wake(PASSPORT EXPIRED 2007).
Habari ndo hiyo wadau.

TUNGALI TUNAFUATILIA MAHAKAMANI KISUTU TUTAWAJULISHA TAARIFA KAMILI ZAIDI SI MUDA.

DEMOKRASIA

Uenyekiti wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania emekabidhiwa rasmi kwa CCM kutoka kwa UDP leo hii, Kiti hiki kitakuwa kinakaliwa kwa kupokezana kila baada ya mwaka mmoja kwa vyama vyote vyenye wabunge kwa kufuata mpangilio wa erufi.
John Cheyo alikabidhi rasmi kwa Pius Msekwa makamu wa CCM Bara.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...