May 27, 2008
CHEE NKAPA AZOZA
RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amevunja ukimya kuhusu tetesi na tuhuma kwamba alikiuka misingi na kujikita katika biashara wakati akiwa madarakani kwa kusema madai hayo si ya kweli na kwamba wanaomtuhumu wana chuki dhidi yake.
Akihutubia mwishoni mwa wiki katika Kijiji alichozaliwa cha Lupaso, Wilaya ya Masasi, Mkapa alisema wanaomtuhumu wanamchukia kwa kutowapendelea wakati wa utawala wake. Katika hotuba yake hiyo aliyoitoa wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kwa Kituo cha Afya kinachomilikiwa na Kanisa la Katoliki kijijini hapo, alisema; “Msisikilize uongo huo kwa sababu hauna msingi wowote isipokuwa ni chuki …hasa inayotokana na watu ambao walifikiri nitawapendelea … sikuwapendelea,” alisema Mkapa huku akishangiliwa na wanakijiji wenzake waliohudhuria makabidhiano hayo.
Alisema kuwa yeye si tajiri na kwamba tuhuma hizo ni za uongo na hivyo kuwataka wananchi kuzipuuza kwa kuwa hazina msingi wowote wala chembe ya ukweli. “Sina uwezo wa fedha ingawa najua mnasikia na kusoma mengi …naishi kwa pensheni yangu kutoka serikalini kutokana na kuwa kiongozi kwa miaka 10 ambayo hata Mzee Mwinyi anaishi hivyo maana sisi sote ni wastaafu. Huo (uvumi) ni uongo …uongo ….uongo ….uongo …uongo….uongo….uongo,” alisema Mkapa na kuongeza; “Mimi si tajiri, nimeomba msaada nimepewa…nimejinyima mimi na mke wangu ndiyo tukaweza kugharimia kusafirisha vifaa hivi kutoka Canada hadi Dar es Salaam, kutoka hapo hadi hapa vimesafirishwa na Serikali…..sikuwa na uwezo wa kununua vifaa kama hivi. Nitapata wapi fedha za kununua vifaa kama hivi,” alisema Mkapa.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Prof Aloysius Mwessa Hnonoli ni Mbongo wa kwanza kuwa Mkurugenzi wa Muhimbili na Mkuu wa Chuo kikuu cha Tiba. Mstaafu huyu jana alitu...
-
Nimekuta ubishi paala fulani tena kwa watu naweza sema ni waelewa kiasi fulani maana wameenda shule na wengine wako katika fani, ati ile ho...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
The Himba are an ethnic group of about 20,000 to 50,000 people living in northern Namibia, in the Kunene region (formerly K...
-
Mineral occurrence in Tanzania by TMAA UONGEZAJI WA PATO LA MTANZANIA Mheshimiwa Spika, 46. Lengo la Dir...
-
Kina dada wengi hivi sasa imekuwa ni kawaida kwenye kila shughuri hasa za usiku kukuta wamevaa nguo fupi, wengi wanasema ni fashion...
-
Ukumbi huko nyuma ya Minara miwili ukiwa ni wa mviringo. Eneoe kubwa la chai na ukaguzi pamoja na usajili kwa waalikwa. Sehemu za waa...