December 28, 2009

Kitoweo kutonesha kidonda cha MUUNGANO??

Nimemsikia waziri mmoja wa Visiwani akilalamika kuwa tani 80 walizopewa Zenji si sawa na kuwa wanapaswa kupewa tani takribani 120 ya samaki wa al maarufu "Samaki wa Magufuri" ambazo ni sawa na aslimia 40% ya samaki hao waliokamatwa yapata miezi zaidi ya nane iliyopita huko bahari kuu.
Habari ndo hiyo.

MWISHO KUSAJILI SIMU SASA JUNI 30, 2010

Tanzania(TCRA) imeongeza muda wa usajili wa kadi za simu kwa muda wa miezi sita mingine ambapo sasa mwisho itakuwa ni Juni 30, mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Profesa John Mkoma, alisema wamelazimika kuongeza muda huo kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa usajili ikiwamo tatizo la umeme vijijini.
“Kutokana na tathmini iliyofanyika na kwa kuzingatia maslahi ya watumiaji pamoja na watoa huduma, TCRA imeongeza muda wa kusajili namba za simu kwa muda wa miezi sita mingine hadi Juni 30, mwakani,” alisema Profesa Mkoma.
Alisema pamoja na kwamba tangu usajili huo uanze Julai mosi, mwaka huu hadi Desemba 20, watumiaji milioni 6.3 ambao ni sawa na asilimia 43 wameshajisajili na kuingizwa kwenye data, lakini utaratibu huo umekuwa ukikabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zimekwaza usajili huo hasa vijijini.
TCRA iliamua kuanzisha utaratibu wa kusajili namba za simu Mwaka huu ili kulinda watumiaji na matumizi mabaya ya huduma hiyo ya mawasiliano , kuwezesha kutambua watumiaji wa huduma za ziada za simu kama huduma za kibenki nakadhalika, kuimarisha usalama wa taifa na kuwawezesha watoa huduma kufahamu wateja wao na kuwahudumia.

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...