September 28, 2011

Chips Mayai hatari kwa afya yako!?


WATAALAMU wa Kilimo na Afya wamesema kuwa vifo vingi husababishwa na ulaji hafifu wa matunda na mboga za majani huku wakihadharishwa kuwa ulaji wa chipsi mayai unachangia unene unaosababisha vifo vya ghafla.

 Katika mkutano wa kwanza wa uhamasishaji matumizi ya bidhaa za matunda na mboga unaofanyika mjini Arusha, wataalamu hao walisema inapotokea vifo vya namna hiyo, baadhi ya watu kusingizia sababu mbalimbali hususani uchawi.

 Wamebainisha kwamba watu wengi wanakula matunda na mboga chini ya kiwango cha gramu 400 kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), jambo ambalo ni hatari kwa afya.
 

Mtaalamu kutoka WHO, Godfrey Xuereb alisema jana kwamba takribani watu milioni mbili hufa kila mwaka kutokana na maradhi yanayosababishwa ukosefu wa lishe za matunda na mboga.

 Mwenyekiti wa Baraza la kuendeleza Kilimo cha Matunda na Mboga (Hodect), Felix Mosha alisema viazi vilivyochomwa kwenye mafuta na kuchanganywa na mayai ya kukaanga maarufu kama Chipsi Mayai unaonesha kushika hatamu katika lishe za wakazi wa mijini hasa vijana na wanawake.

 Akielezea chakula hicho kama mlo ‘mchafu’, Mosha Alisema: “Matokeo yake taifa sasa limekumbwa na tatizo la unene uliokithiri hasa miongoni mwa watoto na akina mama na kuchangia vifo vingi isivyotarajiwa.” Ofisa kutoka Wizara ya Kilimo na Chakula, Geoffrey Kirenga Alisema:

 “Na mara nyingi mtu akionekana mnene huchukuliwa kuwa na afya lakini ukweli wengi huwa na utapiamlo na wanapofariki ghafla wanakuwa chanzo cha uvumi, tetesi na hisia za ajabu wakati chanzo hasa huwa ni ukosefu wa vitamini na madini yatokanayo na matunda na mboga”.
 

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akifungua mkutano huo, alisema wastani wa mtanzania mmoja hula gramu 80 pekee za matunda na mboga kwa siku.

 “Hii ni asilimia 20 tu ya kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambacho ni gramu 400 kwa mtu mmoja kwa siku.”

 Alisema Maghembe na kuongeza kuwa asilimia kubwa ya Watanzania humaliza hadi miezi miwili bila kugusa hata tunda moja.

 “Na hii ni aibu maana hapa nchini kuna matunda ya kila aina ambayo pia hupatikana kwa bei ya chini sana, lakini bado watu hawana mwamko wa kuyatumia kiafya na hata katika mila zingine matunda na mboga huonekana kuwa ni vyakula vya watoto,” alisema Waziri Maghembe.

Source: Habari Leo

Kibaki atangaza siku mbili za maombolezo


Rais Mwai Kibaki ametangaza siku mbili za maombolezo ya kifo cha Mwanaharakati Prof Wangari Maathai, pia kesho itakuwa siku ya mapumziko nchini Kenya ili kutoa nafasi kwa wakenya kushiriki Mazishi ya Mwanaharakati huyo. 

Newzzzz Alert. Tanesco yabwagwa, Dowans Kulipwa Mabilioni yake.

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamiz lililoweka na Tanesco dhidi ya Dowans Tanzania ya kusajiliwa kwa tuzo ya Billion 94 iliyotolewa na ICC.


Kusajiliwa kwa tuzo hiyo kutaipa nguvu kisheria Dowans kulipwa Mabilion hayo ambayo bila shaka yatakuwa yameongezeka kutokana na riba iliyokuwa inaendana nayo toka kutolewa tuzo hiyo na ICC November Mwaka jana.

Nimeombwa na Michelle Obama!

Bernard --

I see the day-to-day challenges my husband faces, and the difficult decisions he has to make.

I know that everyone supporting the campaign now has stood with Barack even during the hardest times, just like I always do. It gives him strength to know that we have his back.

Will you let Barack know you're with him by making a $3 donation today?

https://donate.barackobama.com/Friday-Deadline

Thank you,

Michelle


Thank You First Lady,
I will make sure I donate before the dead lineDowans kulipwa yale mabilioni leo??
KITENDAWILI cha iwapo Kampuni ya kufua umeme ya Dowans inastahili kulipwa tuzo ya Sh94 bilioni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) au la kinatarajiwa kuteguliwa leo wakati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itakapotoa uamuzi wake wa kisheria.

 Dowans iliwasilisha maombi katika mahakama hiyo ikiomba tuzo ya kiasi hicho cha fedha dhidi ya Tanesco, baada ya kuamriwa na jopo la majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) ya Paris, Ufaransa Novemba mwaka jana.

 Jopo hilo liliketi chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen akisaidiwa na  wasuluhishi Swithin Munyantwali na Jonathan Parke na kutoa uamuzi huo wa kuitaka Tanesco ilipe tuzo hiyo ya mabilioni.

 Vyanzo vya habari kutoka Mahakama Kuu, vilidokeza jana kwamba uamuzi wa maombi hayo ya usali wa tuzo hiyo ya Dowans unatarajiwa kutolewa leo.

 Endapo Mahakama Kuu itakubaliana na maombi ya Dowans, basi tuzo hiyo itasajiliwa na kuipa nguvu ya kisheria kulipwa mabilioni hayo.Hata hivyo, Dowans kwa kujihami, imeshafungua maombi mengine ya utekelezaji wa hukumu hiyo ya ICC katika Mahakama Kuu Uingereza kupitia kwa mwanasheria maarufu nchini.

Source: Mwananchi

Kampeni Igunga zahamia angani, CHADEMA waanza, CCM na CUF kufuata leo.WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilitikisa anga la Igunga baada ya kuanza kutumia helikopta kufanya kampeni zake, zile mbili za wapinzani wao, CCM zikishindwa kuwasili jimboni humo na kubaki Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutokana na sababu za kiufundi.Wakati Chadema ikipasua anga na mbili za CCM zikibaki KIA, helikopta ya Chama cha Wananchi (CUF) nayo imeshindwa kutua Igunga jana na sasa inatarajiwa hapa leo.

 Helikopta ya Chadema ilianza kuonekana katika anga la Igunga saa 10:40 jioni ikiwa na maandishi makubwa ya chama hicho na rangi ya bluu.Ujio wa helikopta hiyo ulivuta kwa muda idadi kubwa ya wananchi waliokuwa kwenye Viwanja vya Sabasaba wakisubiri ujio wa helikopta mbili za CCM, ambazo awali, ilielezwa kuwa zingewasili saa 8:00 mchana.

 Baadaye ilielezwa kwamba helikopta hizo za CCM zingetua Igunga saa 11:30 jioni zikiwa na makada wa chama hicho akiwamo Katibu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.

 Hata hivyo, ilipofika saa 12:00 jioni, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akitumia gari la matangazo la Bendi ya muziki ya ToT Plus alitangaza kwamba helikopta hizo zisingeweza kutua Igunga kutokana na sababu za kiufundi.

Alisema zilichelewa kupata vibali kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam na kwamba baada ya kutua KIA ilishauriwa kuwa ni vyema zilale hapo.

 Alisema kama helikopta hizo zingeondoka KIA jana jioni na kufika hapa usiku wakati tayari kungekuwa na giza kitu ambacho kisingekuwa kizuri kiusalama. Alisema helikopta hizo sasa zitawasili leo saa 4:00 asubuhi.

 Matumizi hayo ya helikopta yanawafanya wananchi wa Igunga kushuhudia kampeni nzito na za aina yake tangu kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza wa vyama hivyo mwaka 1994 na Rostam Aziz kushinda.Jimbo hilo lenye wapiga kura 170,000 katika vijiji 96, halijawahi kushuhudia kampeni nzito kiasi hicho zinazohanikizwa na magari yenye vifaa vya kisasa vya muziki.
 

Habari kutoka ndani ya CCM, zinaeleza kuwa katika kujihakikishia kura katika kipindi hiki cha lala salama, chama hicho kitawatumia makada wake, Makamba na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli wanaoelezwa kuwa na ushawishi mkubwa.

 Kulingana na vyanzo mbalimbali vya habari, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM anatarajiwa kurudi tena hapa keshokutwa.Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye aliwasili hapa jana kuongeza nguvu kwa viongozi wa chama hicho ambacho idadi kubwa ya wabunge wake wameweka kambi hapa.
soma zaidi hapa 

Source: Mwananchi

Elimu kibongo bongo, Migomo kabla ya darasa.

University students display placards as they wait for the outcome of a meeting between their leaders and the Ministry of Education and Vocational Training officials in Dar es Salaam on Tuesday, on their overdue loans which they would have collected on the 27th of this month. (Photo by Robert Okanda)Elimu ya namna hii kweli tutafika? Elimu ya msingi wasoma kwa taabu, hakuna madawati, vitabu, walimu wa kutosha.

 wafaulu kiMungu Mungu, waenda shule za kata, wakaa gheto kama si kwenda na kurudi zaidi ya kilomita ishirini kwa siku, nako darasani hakuna madawati, hakuna maabara, maktaba hazina vitabu, walimu ni kasheshe. 

Lakini nako wafanikiwa kufaulu kiaina, hatimaye waja chuo, ukidhani kuna unafuu, hali ndo kasheshe zaidi, mkopo hauupati mpaka kwanza muemdeshe mgomo, upigwe virungu na mabomu ya machozi na hii ni kipindi chote mpaka umalizapo kozi yako. Muhitimu huyu aliyepitia haya yote mwisho wa siku anakuja kuwa mtu wa namna gani? tunakuwa tumejenga taifa la aina gani kupitia mfumo huo?


 Mimi sijui, wewe je? 

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...