September 26, 2011

Zanzibar UPDATES - Meli tano zapigwa marufuku

Ajari ya Mv Spice Islander 1 yazindua Mamlaka toka usingizini, yazipiga marufuku meli tano kwamba hazina sifa ya kubeba abiria. 

MAMLAKA ya vyombo vya baharini Zanzibar, zimesimamisha huduma za meli tano kutokana na meli hizo kutokidhi viwango vinavyotakiwa kusafirisha abiria na mizigo.

 Meli zilizositishwa safari ni Mv Serengeti, Nura, Buraq One, Buraq Two pamoja na Mubarak kutokana na usajili wa meli hizo ulikuwa ni kusaidia kuvuta meli baharini (tagi) na siyo kubeba abiria.

 Akitoa taarifa hizo kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Mamlaka wa Vyombo vya Bahari Zanzibar, Haji Vuai Ussi alisema kukatishwa kwa safari kwa vyombo hivyo kumetokana na kukosa usalama wa uhakika kwa abiria wake.

 Aidha, alisema ingawa meli hizo zilianza kazi za kuchukua abiria kwa muda mrefu, lakini zilishindwa kujisajili kwa kazi hiyo, jambo ambalo limekuwa likienda kinyume cha taratibu za vyombo vya bahari.

 Vuai alisema meli hizo pia zilikuwa zikihudumiwa na wafanyakazi wasiokuwa na sifa wala taaluma ya ubaharia pamoja na kushindwa kutoa taarifa za usalama kwa wasafiri wakati wanapokuwa safarini.

 Alisema Mamlaka imebaini tatizo kubwa katika meli hizo baada ya kufanya ukaguzi na kugundua kuwa meli zote hizo zimekosa mfumo mzuri wa mawasiliano pale linapotokea tatizo la kiufundi.

 Akizungumzia kuhusu usalama wa vyombo vya baharini kwa ujumla, alisema mamlaka imegundua pia matatizo lukuki kwa manahodha wa meli hizo kwa kuondoa meli bila kujua taarifa za usalama wa abiria wao.

 Mkurugenzi huyo alisema mamlaka yake imejipanga upya kuhakikisha kuwa wanachukua hatua za kisheria kwa nahodha ye yote ambaye atabainika kuondoa meli bila ya kuwa na taarifa sahihi za abiria.

 Hivyo amewataka wamiliki wa vyombo vya baharini kutoa ushirikiano kwa mamlaka.

Source: Habari Leo

WINNERS Boulevard.: ARE YOU BUILDING PIPELINES OR HAULING BUCKETS?

WINNERS Boulevard.: ARE YOU BUILDING PIPELINES OR HAULING BUCKETS?: Hapo zamani za kale kulikuwa na kijiji Fulani, kilikuwa kizuri sana kwa kuishi isipokuwa tatizo hakukuwa na majim ya uhakika mpaka mvua in...

NEC WEBSITE KULIKONI?

Hii ni screen shot ya Wavuti ya Tume ya Uchaguzi iliyopigwa saa 12:03 jioni hii, nilitarajia kukuta updates zozote kuhusiana na yale yanayojiri yanayowahusu, lakini iki ndicho kilicho hapo.
]
Update pekee inayoonekana baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana ni sentensi hii yenye maneno yapatayo 19:- "Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yatangaza Ratiba ya Uchaguzi wa JImbo la Igunga pamoja na Chaguzi Ndogo za Madiwani"



Hata kwa sentensi hii mtu alitarajia kupata hiyo ratiba inayosemwa, lakini sivyo ilivyo. Mtu anajiuliza kulikoni huko NEC? yaani toka mwaka jana hakuna lolote lililotokea kuhusiana nanyi litupasalo wanachi kuhabarishwa? mtu aliyeikumbuka website hii na kupost hako ka-update ka maneno 19 ilimchukua muda gani hata kushindwa kuweka taarifa kamili?

  Hii yasikitisha kwa kweli, karne hii ya 21 na Zama hizi za Taarifa (Information Age) bado asasi muhimu kama hii inashindwa kuitumia ipaswavyo, mtu alitarajia loe hii kuwe si tu na ratiba bali majina, picha za wagombea na vyama na pengine taarifa kuhusu idadi halisi ya wapiga kura, vituo, na mambo mengine kama hayo.

Shule za Kata hazifai!


Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa, amesema haungi mkono shule za sekondari za kata nchini kwa sababu hazijaandaliwa vizuri kuwawezesha watoto kukomaa na kupata elimu iliyo bora.

Aliyasema hayo jana katika mahubiri yake kwenye kanisa kuu la Anglikana Mbeya ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya kutembelea Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini ya kanisa hilo. Dk. Mokiwa alisema shule nyingi za kata zimejengwa kisiasa na ndiyo maana hata elimu inayotolewa katika shule hizo haikidhi mahitaji ya ushindani wa kielimu. 

Alisema kutokana na shule hizo kujengwa kwa manufaa ya kisiasa, wanafunzi wake wamekuwa wakisoma kwa mtindo wa kinadharia na kukaririshwa, alisema hali ambayo haimfanyi mwanafunzi kuelewa vizuri. “Vijana wa siku hizi mnafundishwa maswali yote mnapewa majibu ya kuchagua, mnapofundishwa suala la ufahamu mnashindwa kuelewa,” alisema Dk. Mokiwa.

 Askofu Dk. Mokiwa alisema ili kurudisha elimu katika kiwango bora, serikali irejeshe shule za  zilizokuwa zikimilikiwa na taasisi za dini ili wao waziendeleze kwa sababu shule hizo zilimjenga mwanafunzi kiroho na kiakili. 

Alisema serikali ilizichukua shule hizo  kama majengo na kuacha msingi ambao ulikuwa umewekwa na shule hizo ambao ulikuwa na mfumo mzuri wa ufundishaji uliozingatia maadili ya mwalimu na mwanafunzi. “Shule za misheni zirudi ni mali ya kanisa, na zitarudi zenyewe au kwa kurudishwa na waliozichukua,” alisisitiza Dk. Mokiwa. 

Akizungumzia suala la ufisadi, Dk. Mokiwa alisema ufisadi ni roho na tabia mbaya ambayo ipo katika kada mbalimbali kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa. 

Alisema ufisadi unapaswa kukemewa kuanzia ngazi ya familia kwani ikiachwa  baadaye unaharibu taifa katika sekta za bararabara na umeme na hivyo kuzua malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania.


SOURCE: NIPASHE

CCM WATWANGA MWANDISHI WA HABARI


MAKADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walio katika timu ya kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga, wameendelea kuandamwa na kashfa za matukio ya vurugu baada ya walinzi wa chama hicho (mabaunsa) kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Mussa Mukama, na kunyang’anywa vifaa vya kazi na fedha. 

Akizungumzia tukio hilo, Mukama alisema alikwenda katika Hoteli ya Peak saa moja jioni walikofikia viongozi wa CCM kufanya mahojiano na Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya, kuhusu tukio la juzi la kurushiana risasi na kusababisha gari lake kuvunjwa vioo.

 Mukama alisema akiwa ameambatana na mwandishi wa kujitegemea, George Maziku, alizuiwa na walinzi wa CCM kuingia ndani, hali iliyowalazimu kuwasiliana na Bulaya kwa njia ya simu. 

“Tulimpigia simu Bulaya, ambaye alikuja langoni na kuwataka walinzi waturuhusu kuingia ndani,” alisema mwandishi huyo.

 Hata hivyo, alisema, ilipofika saa 3 usiku, waliagana na Bulaya lakini walipofika langoni yeye aliitwa na mlinzi mmoja ambaye baada ya kumfikia, alishangaa akimkaba na baadaye watu wengine wakajitokeza na kumshambulia kwa mateke, ngumi na makofi na kumnyang’anya fedha sh 423,000, modem na flash.

 Aliongeza watu hao wapatao wanane waliokuwa na sare za CCM na wengine nguo za kawaida waliendelea kumshambulia hadi walipozuiwa na mtu mmoja aliyetoka ndani ya hoteli hiyo. 

“Jamaa walipokuwa wakinipiga walitaka kuninyang’anya laptop yangu; nilipojaribu kumpigia simu Bulaya kumjulisha kilichonipata langoni, simu yake iliita bila kupokelewa,” alisema. 

Aliongeza kuwa baada ya hapo alipata msaada kutoka kwa mwandishi mwenzake, Maziku, aliyekwenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi Igunga na kupewa PF3 ya kutibiwa hospitali ya wilaya. 

Alisema polisi walimpa RB namba 1673/2011 na kisha alipata matibabu na kuruhusiwa. Maziku alisema wakati wanatoka ndani ya hoteli alikuwa ametangulia mbele na Mukama akiwa nyuma; na mwenzake alipoitwa na mlinzi hakuwa na wasiwasi, lakini ghafla aliona wakimshambulia na alishindwa kutokana na wingi wa mabaunsa. 

Akizungumzia tukio hilo, Bulaya alisema amesikitishwa na kitendo ambacho ametendewa mwandishi huyo. 

Alisema kuwa baada ya mahojiano hayo aliingia katika kikao ambacho aliamua kuondoa mlio kwenye simu yake, hivyo hakusikia alipopigiwa na Mukama kuomba msaada.

Source: Tanzania Daima.
Ndipo siasa za Bongo zilipofikia sasa hivi. Hii ni hatari hatua za dharura zisipochukuliwa.  

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...