February 12, 2009

Huu ni ulevi wa madaraka au????????????

DC AAMURU WALIMU WACHARAZWE VIBOKO MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali, ameacha maswali miongoni mwa walimu baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika shule tatu za msingi za kata ya Katerero na kuamuru walimu 16 kucharazwa viboko kwa kile alichodai ni utoro na uchelewaji wao.

“Nikamwita askari wangu nikamwambia Mwalimu Mkuu atoke, tukafunga mlango nikawaambia walimu kama watoto wanaochelewa mnawapa adhabu na mimi nawapa adhabu,” alisema Mnali kuthibitisha kucharazwa viboko vinne kila mmoja.

Walimu waliocharazwa ni Generosa Lwakatare, Ernestina Anatory, Jonesta Grenos, Hawa Ayubu, Rehema Baisi, Frieda Laurian, Avitus Leonald na Asirath Ndyamukama wa Katerero.

Wengine ni Amos Kamugisha, J.K. Zale, Bruno Francis, M. Mwesiga, Pulleti Rugemalila, Winfrida Kakurwa, Editha Bigilwa, Ester Mutashaba, Ludovic Bushongole, Gosbert William, Venance Philipo na Vedasto Munabi wa Kansenene.

Walimu wengine waliochapwa ni Imelda Lwegalulira, Coretha Ernest, Devotha Bushobe, Augustina Bampenja, Josephina Ndyamukama, Julius Katemana, Videlieth Yesse, Generoza Mulokozi, Sylvester Petro, Josiah Kamuhabwa na Concessa Rweyemamu wa Kanazi.

“Ni kweli tukio hilo limetokea … ni vyema DC na huyo Polisi wakapimwa afya kwa sababu hii si hali ya kawaida, kwani zipo taratibu za kinidhamu za kuchukua kwa watumishi,” alisema Naibu Waziri wa Elimu MWANTUMU Mahiza ambaye kitaaluma ni mwalimu.

WAASIA "WAUAJI" WAPANDA KIZIMBANI.

Watuhumiwa wa mauaji ya kutisha yaliyotekea jijini hivi karibuni Vinoth Praveen (23) na na mkewe Komal Bupendra (23) wamefikishwa mahakamani leo hii. Wanatuhumiwa kumuua Abdul Basit Abdallah kumkatakata na mwili kuuweka katika begi na kuutelekeza ndani ya gari katika jengo la J.M Mall, alikuwa akiwadai pesa kiasi cha dola za USA 20,000.

Ina maaana gani?????

Siku imekaribia, je ina maana gani hasa? na umejiandaaje kwa siku hiyo????????

MAGAZETI YAPEWA SIKU 7 KUJIELEZA

SERIKALI IMEYAPA SIKU SABA KUANZIA LEO MAGAZETI MATATU YA TAIFA LETU, SEMA USIKIKE NA TAIFA TANZANIA KUJIELEZA KWANINI YASICHUKULIWE HATUA KWA HABARI AMBAZO YAMEKUWA YAKIANDIKA. TAMKO LIMETOLEWA NA WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO KAPTENI MSTAAFU GEORGE MKUCHIKA LEO HII.

UMATI WASIKILIZA KESI YA ZOMBE.

Watu wengi wamekuwa wakijitokeza mahakamani kufuatilia kesi ya mauaji ya wafanyabiashra wa madini na taxi dreva inayomkabili Zombe ana wenzake ambapo leo hii mshitakiwa wa pili Christopher Bageni anaanza utetezi wake.

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...