May 31, 2009

Amin, Usiamini huu ndo ukweli - dawasco ina wateja 70, 000 tu.

Mamlaka ya Maji safi na maji taka DAWASCO inayohudumia wakazi wa Jiji la Dar na Mkoa wa Pwani ina wateja halali 70, 900 tu kati ya jumla ya wakazi wapatao Millioni Nne na Ushee hivi. 
Hayo yamebainishwa na Afisa Biashara Mkuu Bw Raymond Mndolwa leo wakti akitangaza kuanza kwa operesheni kata maji kwa wadaiwa sugu inayotarajiwa kuanza next wiki. 
Naomba kuwasilisha. 

Mbunge Aloyce Kimaro apata ajali

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro amenusurika kufa baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kuparamia mawe yaliyopangwa barabarani na kupata ajali usiku wa kuamkia jana.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Kimaro na polisi zinasema kuwa, ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mikongeni kata ya Lembeni wilayani Mwanga, Kilimanjaro kwenye barabara kuu ya Moshi-Tanga, akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda jimboni kwake.

Kwa mujibu wa habari hizo, wakati ajali hiyo inatokea, Kimaro alikuwa na rafiki yake Joseph Temu ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari hilo aina ya Mercedes Benz akiwa na mkewe na watoto wake watatu. Katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa.

May 30, 2009

Meneja Mtoto

Meneja YANK wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akivalisha viatu mtoto Neema Ramadhani wa Asasi ya Good News Social Welfare cha vingunguti katika hafla ambayo Tigo ilitoa msaada wa magodoro, viatu, sare za shule, vifaa vya shule na misaada  mingine ya kibinadamu kituoni hapo jijini hivi karibuni.

May 29, 2009

KELELE, the African Bloggers conference, coming soon

August 13-16th, 2009 in Nairobi, Kenya. Kelele is an annual African bloggers’ conference held in a different African city each year and run by an organising committee in that city.

Date : August 13-16th, 2009

Venue : Nairobi, Kenya

Organizer : Kelele organising committee

Kelele is the Kiswahili word for noise.

This gathering of African bloggers is organised in the tradition of historical African societies where everyone has a voice. With too many voices marginalised or simply ignored in Africa society today for a variety of reasons, the organizers believe that the internet in general and grassroots media tools such as blogs in particular represent the most powerful way in which to give Africans back their voice. They will be gathering to make a powerful, positive, inspirational noise that will be heard across the continent and beyond.

The theme of Kelele ’09 Nairobi is Beat Your Drum – we want to connect the traditional Africa method of getting your message across vast distances – the talking drums – to the 21st century and the tools we use today to get our message across, blogs and the Internet. We anticipate that this conference will continue to be called Kelele wherever it is held. For example Kelele Nairobi ’09, Kelele Accra ’10, Kelele Cairo ’11 and so on.

Uchumi kukua kwa kasi 2010 - BOT

Tanzania's central bank sees growth rebound in 2010.

Tanzania's economic growth could rebound in 2010 to more than 6 percent if the world overcomes the economic downturn, the central bank governor said on Friday.

Tanzania, the second largest economy in the five-nation East African Community bloc, expects growth of 5-6 percent this year, down from 7.4 percent in 2008, due to the effects of the global economic slowdown.

"We are expecting 2010 to start moving up again, the global recovery should certainly push us, maybe towards 6 (percent) and above," Benno Ndulu told Reuters on the sidelines of a regional meeting of central bank chiefs.

He said the downturn had hurt demand for the country's coffee, cotton, tourism and gemstones.

Tanzania, whose relative macroeconomic stability has made it popular among foreign investors, has suspended plans to raise funds through a Eurobond, but is hoping to get support from the International Monetary Fund to boost the economy. Source reuters

May 28, 2009

Mwakyembe Asikitishwa na taarifa ya Polisi..

BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA KYELA S.L.P. 44, S.L.P. 20797 Kyela Dar Es Salaam 28/05/2009
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Nimesikitishwa na kufedhesheshwa na taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa Iringa Jumatatu iliyopita na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini James Kombe na kutangazwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mazingira ya ajali ya gari niliyopata tarehe 21, Mei 2009, saa 1 na dakika 10 eneo la Ifunda, mkoani Iringa. Taarifa hiyo ya Polisi inakanusha maelezo yangu yote na ya dereva wangu kuhusu ajali ilivyotokea na kunitaka nijiepushe kutoa matamshi kuhusiana na ajali hiyo kwa madai kwamba sina utaalamu na masuala ya ajali. Taarifa hiyo nimeipata kupitia gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 26, 2009 na kwa kuwa uwasilishwaji wake haujalalamikiwa na Jeshi la Polisi, naichukulia taarifa hiyo kuwa sahihi.
Pamoja na kwamba bado naumwa na niko nyumbani nikipumzika kwa ushauri wa madaktari, nimelazimika kuvunja ukimya na kutoa taarifa hii fupi kuzuia upotoshaji wa makusudi unaofanywa na magazeti, hususan gazeti la Tanzania Daima, na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi kwa sababu wanazozijua wenyewe kuhusu suala hili. Aidha nataka kuelezea masikitiko yangu kuhusu hatua hiyo ya Jeshi la Polisi ambayo ina mwelekeo zaidi wa kisiasa kuliko utaalamu wa upelelezi na uendeshaji mashitaka kama ifuatavyo:

Tujikumbushe - Idd Amin Dadaa alikuwa ajiitaje?

Wengi wetu twaweza kuwa tumesahau au hatujui kwa kuwa hatukuwai sikia mahala popote kutokana labda na umri wetu, au tu kutofuatilia yanayoendelea au yaliyokuwa yakiendelea kwa wakti uliopita, lakini huyu anaweza kuwa ni mmoja (kama si yeye pekee) ya kiongozi pekee aliyewai kujipa majina na nyadhifa nyingi tu jina.
Alikuwa akijiita “His Excellency, President for Life, Field Marshal Al Hadji Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, and Conqueror of the British Empire.”

Kufuli mpya kwa kinadada

Wazungu kwa ubunifu tu ni kiboko, Kina Dada hii ni aina mpya ya kufuli jionee 

May 27, 2009

Masikini Liyumba!

Aliyekuwqa Mkurugenzi wa utumishi wa BoT, Amatus Liyumba na Meneja mradi wa benki hiyo Deogratias Kweka wameachiwa huru na Mahakama ya Kisutu leo saa 5:20 baada ya kubaini kuwa hati ya mashitaka ina makosa ya kisheria.
Uamuzi huo ulitolewa leo na Hakimu Mkazi Wariyalwande Lema anayesikiliza kesi hiyo. Baada ya kutolewa uamuzi huo washitakiwa walishuka kizimbani tayari kurejea mahome kabla ya kudakwa tena na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi.
Yaonekana ngoma bado mbichi hapa.

Kero ya Daladala BONGO sasa Bye bye

"Nimerikuta maeneo ya Ubungo likielekea Posta, yasemekana yameletwa ka 200 hivi na mengine 1000 yako njiani kutatua shida ya usafiri na kero zinazoletwa na Daladala"

WAWEKEZAJI WETU

Mwekezaji akipeleka mzigo kwa mteja wake. Wawekezaji wakisubiri wateja.

May 25, 2009

JK AREJEA

Rais JK akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliojitokeza kumraki uwanja wa Ndege akitokea US kwa safari ya kikazi ya wiki moja.  

CCM yaibuka kidedea Busanda

Mbunge mpya wa Jimbo la Busanda Lolensia Bukwimba,
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukwimba Dan Mollel ametangaza matokeo rasmi ambapo mgombea wa CCM ameibuka kidedea
matokeo ni kama ifuatavyo:
Waliojiandikisha kupiga kura ni 135,000 na ushee
Waliojitokeza kupiga kura  55,000 na ushee
CCM wamepata kura...............29,242
CHADEMA..................22,000 na ushee..
UDP.......................607
CUF......................... 271. 
HAH HAH HABARI NDO HIYO

Busanda, Nani Kucheka???

Mgombe wa CHADEMA Finias Magessa Mgombea wa CCM Lolesia Bukwimba
Matokeo yasiyorasmi yanaonyesha kuwa CCM inaongoza kwa kura 30,000 huku CHADEMA ikiwa na kura 21,000 na vyama vya UDP na CUF vikiwa na pungufu ya kura 1000 kila kimoja, muda si mrefu tutapata matokeo rasmi nasi tutawajulisha kama kawa. 

May 23, 2009

KWIKWI!

WADAU NIWIENI RADHI KWANI BLOG IMEPATA KA KWIKWI KIDOGO KUNA KARUSI KARITUPA KOMBORA KUTAKA KUIBOMOA BAADA YA KUPONA YALE YA MBAGALA LAKINI KAMECHEMKA HIVYO WATAALAMU WANAIJENGA UZURI MUDA MREFU MTAFURAHIA BLOG HII.
WASALAM
Bongpix

May 21, 2009

Mwakyembe alazwa MOI.

Dr H Mwakyembe akishushwa toka ktk ndege ya kukodi na kupelekwa moja kwa moja MOI kwa Matibabu zaidi, 
Dr Mwakyembe alipata ajali ya gari mapema leo asubui huko mkoani Iringa akielekea Dar toka kuwaona wapiga kula wake.
Mungu akujalie upone haraka. 

NEWS BREAK!!!..... MWAKYEMBE APATA AJALI MBAYA

Habari zilizotufikia muda c mrefu ni kuwa Mbunge wa Kyera Harrison Mwakyembe amepata ajari akiwa jimboni kwake Mkoani Mbeya na yasemekana ameumia vibaya na uenda akaletwa MNH kwa matibabu zaidi.
TUTAENDELEA KUWEPASHA ZAIDI YATAKAYOJILI KADRI TUTAKAPOKUWA TUNAPATA TAARIFA. 
TAARIAFA ZILIZOTUFIKIA NI KUWA NDEGE YA KUKODI TOKA IRINGA IKIWA NA DR MWAKYEMBE ITAWASILI SAA 9:30 

May 20, 2009

Bongo mswano tu

Wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Maendeleo huko Mbagala Kuu karibu na mabomu wakifanya mtihani wa moko leo hii

May 19, 2009

Hichi KIJIJI CHA KILEO KI WAPI BONGO??

WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. 
HIKI ni kijiji kipo hapa bongo, Je kuna ajuaye wapi kilipo? ni cha nani au kinafanya nini?
Aka ni kamtihani kidogo yeyote atakayepata zawadi nono itatolewa. 
KAZI KWENU.

May 18, 2009

Kondomu ATMs Hizoooo

Hatua nne za kupata kitendea kazi aka Kavwero Bonyeza radha uitakayo.
Ikishawaka taa tumbukiza koini or mia.
Kavwero katadondoka kwa chini hapo
Ni kamoja tu, kwa hiyo kama unaraundi kibao rudia steps hizo upate zaidi kulingana na mahitaji yenu.
Meneja wa Program ya HIV wa PSI Dr Alex Ngaiza akionesha namna ya kupata huduma hii pale Jolly Club wakti wa uzinduzi.

May 15, 2009

Musyoka atua Bongo

Makamu wa Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka amewasili jioni kuanza ziara ya siku nne nchini, alilakiwa na mwenyeji wake Dr Shein. Karibu sana Bongo Bw Musyoka.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...