October 30, 2008

UKISTAAJABU YA MUSA.........................................

AMA KWELI UKISTAAJABU YA MUSA UTAONA YA FILAUNI, Akitoa maoni yake kuhusu hoja hiyo, Zitto ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Rais, alisema anaunga mkono pendekezo hilo la Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini la kutaka ufanyike uchunguzi huo, akieleza kuwa uuzwaji wa Buhemba unatia shaka kwani umeikosesha serikali fedha nyingi.
Alidai kuwa mgodi huo ulinunuliwa na mwekezaji kwa Dola za Marekani milioni 20, lakini mwekezaji akauuza kwa Dola za Marekani milioni 348 huku serikali ya Tanzania ikiambulia patupu.
Kuhusu mgodi wa Buhemba, alitaka uchunguzi wa ufanyike kwani mwekezaji aliyekuwa akiumiliki ameondoka katika mazingira yasiyojulikana tena bila ya kuwalipa wafanyakazi haki zao na kukiuka makubaliano mengi ya mkataba na baadaye kuuza kinyemela mgodi huo kwa kampuni ya Maremeta.

OIC, MEMBE AENDA KUMWONA PENGO

Waziri Membe jana alikutana na Kardinali Pengo juu ya sakata la Bongo kujiunga na jumuiya ya Kiislamu OIC kikao hichi kilikuwa cha siri yalozungumzwa ni wenyewe wanajua ni hadi pale watakapo yabainisha na nina imani si siku nyingi tutayajua.

October 29, 2008

"MENE MENE TEKEL PERES"

Nachelea na kweli nisingependa kudhani au kuwaza au hata kufikili kuwa yanayoendelea hapa Bongo siku hizi yaweza kuwa sawa na msemo huu wa Kibiblia kwa wale nilowaacha basi waende ktk kitabu cha Daniel 5:1-31. yajulikana sana kama THE WRITING ON THE WALL.
5In the same hour came forth fingers of a man's hand, and wrote over against the candlestick upon the plaister of the wall of the king's palace: and the king saw the part of the hand that wrote.

October 28, 2008

Hii imekaaje wadau?????

Tukiachana na maandamano ya wahariri, je hii nayo imekaaje wadau? imekaa njema kweli? askari hawa ambao hawakuona utambulisho wote huu alionao Mroki al maarufu "Father Kidevu" na kuamua kumjebu bila huruma kulikoni? Picha: Mpochi

Wahariri waandamana BONGO

Maandamano yikiwasili kwa Mkuchika. Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo
Mhariri na Mkurugenzi wa gazeti lililotiwa lupango na serikali Mwanahalisi akimfunga mdomo mmoja wa waandamanaji.
Wahariri Kibanda na Mapinduzi
Mwenyekiti wa MISA TAN na Mhadhiri wa UDSM IJMC Ayoub Riyoba (kushoto) na baadhi ya wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali wakiwa mbele ya wizara ya habari baada ya maandamano yaliyoitiswa na bongo Editors forum kupeleka malalamiko kupinga kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi miezi mitatu na serikali.
Hata hivyo hawakuweza kuonana na waziri wala naibu wake kutokana na kuwa wako Dodoma ambako bunge ndio linaanza leo hii.

October 27, 2008

Odemba ang'ara Miss Earth 2008

Miriam Odemba mwakilishi wa Tanzania ktk Miss Earth 2008 huko ktk Jiji la Puerto Princesa magharibi mwa visiwa vya Philippine ni mmoja wa warembo wachache wanaopewa nafasi ya kufanya vyema ktk fainali zitakazo fanyika tarehe 9, Novemba mwaka huu. Picha: afp

October 22, 2008

Maisha Bora....

Mjane Agnes Jeremiah amekuwa akiishi kwa kutegemea kugonga kokoto huko Kunduchi tangu kufiwa na mumewe yapata miaka saba sasa, kwa siku nzuri uingiza kiasi cha Shs 1000 au chini ya US$ 1, kiasi hiki ndicho anachotegemea kulisha na kusaidia familia yake ya watoto wanne wa kwanza akiwa ndo kwanza amemaliza darasa la saba.

Lakini mama huyu hatoweza kufanya kazi hii ya kipato kidogo hivi kwa muda zaidi kutokana na kuwa serikali imewaamulu wote wanaoishi kwenye maeneo ya machimbo ya kokoto huko Kunduchi kuondoka mara moja na siku yoyote tingatinga litaingia kufanya kazi yake. Je ni wapi kina mama kama huyu wataelekea?

JONGWEEEEEEEE

Kwa Komredi Mugabe sasa kumekucha, maana watu woete ni Mabilionea, Noti ya Zim Dolla Million 500 ilotolewa karibuni yatosha kununua Lager tu au tumboga gengeni. Mhhh

TANGAZOOOOO

October 20, 2008

Mogae anyakua kitita cha Bilion 5

Botswana's former President Festus Mogae has won a $5m (£2.8m) prize to encourage good governance in Africa. He stepped down in April after serving two terms in office. Botswana is one of Africa's most stable countries - it has never had a coup and has had regular multi-party elections since independence in 1966.
Announcing the prize, ex-UN Secretary General Kofi Annnan also commended Mr Mogae for his action to tackle the Aids pandemic which has ravaged the country.
The Ibrahim Prize - the most valuable individual annual prize in the world - was set up by Sudan-born telecoms entrepreneur Mo Ibrahim. As well as the $5m prize, Mr Mogae, 69, gets $200,000 a year for the rest of his life

TUDURUSU kiduchu yalojili TARIME

Vumbi la Uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime limetuwama kwa sasa na mshindi na mshindwa ameshajulikana, si vibaya kudurusu kwa chati yaliyojili huko na mstakbali wa Jimbo au Nchi yetu kwa upande mmoja na siasa za vyama kwa upande mwingine.
Kwa hakika yaliyojili huko ktk kipindi chote cha kampeni hata siku ya uchaguzi yenyewe, gharama na maelkopta yaliyotumika kwa jimbo hilo tu si madogo hata kidogo kiasi cha kuyaacha yapite tu.
Huu nadhani waweza kuwa uchaguzi mdogo uliowahi kutumia gharama kubwa kuliko mwingine wowote ktk historia ya taifa letu changa (nasema nadhani kama sivyo naomba kukumbushwa) na masikini ambalo wapo wenzetu wanaopata japo mlo mmoja tu kwa siku na kwa taabu sana tena ndani ya Tarime yenyewe lakini kwa kipindi kifupi tu wameshuhudia matumizi ya kukidhili ya fedha mbele ya macho yao huku wakiambulia vumbi tu.
Mbali na gharama jambo lingine ni siasa za chuki zilizo kidhiri jimboni humo, kwa hakika hili lilikuwa ni tatizo kubwa sana si tu kwa wanatarime wenyewe bali hata sie tulioenda kuripoti habari hizi hatukuwa na amani kabisa, kwa macho yetu tulishuhudia unyama wa kutisha ukitendeka, mtu kukatwa mapanga mbele ya adhala pasi na kujali lolote kwa mkataji, tumeshuhudia damu ikimwagika mbele ya macho yetu, pengie kwa wanatarime wanaweza wasishangazwe sana na hilo kulingana na historia yao na hasa yale ambayo yamekuwa yakijili hapo, lakini kwetu sie hilo lilikuwa la kuogofya sana.
Hali hii ilituwakati mgumu sana kutekeleza majukumu yetu na kwa kweli ilitutia woga mno, pengine ndo maana baadhi yetu wengine waliamua kuegemea moja mbali na mwingine pengine ni ktk kutafuta ulinzi lakini kwetu sie tuliokuwa kati kwa kati hali ilikuwa ngumu sana na hata utendaji wetu uliadhiriwa kwa kiwango kikubwa sana.
Hizi zilikuwa ni siasa za chuki ambazo sikupata kuzishuudia wakati mwingine wowote hapa Bongo, za kushindwa kuvumilia kusikia mtu akitoa kile ambacho pengine kwa mtazamo wako ni utumbo au upuuzi na kuamua ama kumpiga mawe (kama yalomkuta Mch Mtikila na Mbowe) au kumchalnga kwa mapanga kama wale majeruhi wanne au hata kumzuia Mh Waziri kuona majeruhi tu.
Kwa hakika hizi si aina ya saisa ambazo tungependa tuwe nazo Watanzania na zaidi ya yote tufanye kila tuwezalo siasa hizi zisijirejee tena jimboni humo au penginepo popote nchini mwetu kwa hazitufai na si utamaduni wetu hata kidogo.
MUNGU BARIKI TANZANIA

October 13, 2008

Mwaloni kama kawa

Biashara katika soko la Samaki la Kirumba AU Soko la Kimataifa Mwaloni zililejea jana baada ya mgomo uliodumu kwa siku tisa wa wafanyabiashara kupinga kupandishwa kwa ushuru maradufu na kampuni iliyokuwa imepewa kandarasi ya kukusanya ushuru sokoni humo ya Upeo Vijana jana. Kampuni hiyo imesitishwa utoaji huduma hiyo na sasa Halmashauri ya Jiji ndio inakusanya kwa muda Yasemekana kulikuwa na vituo vitatu vya kuchukua ushuru ndani ya mkoa na wilaya moja, na kila kituo gunia moja lalipiwa 300 au 500, kulingana na ujazo na gari likiingia kupakia mzigo lalipiwa paking, hawa jamaa wa UPEO VIJANA wakapandisha toka 300 kwenda 600 kila kituo na 500 kwenda 1,500 ndo kasheshe ilipoanzia hapo.

CHADEMA KIDEDEA TARIME

Matokeo ya Uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime yametolewa na CHADEMA kimefanikiwa kunyakua viti vyote vya udiwani wa Tarime Mjini na Ubunge vilivyokuwa vikishikiliwa na Marehemu Chacha Wangwe.

UCHAGUZI TARIME

Msimamizi wa Uchaguzi Trasias Kagenzi alikuwa na kzi ya ziada kutuliza wapiga kura baada ya baadhi ya vituo kuwa na kasoro mbalimbali kama kutofuhuliwa hata baadhi yake kulazimisha kuvuja mlango.
Joseph Marwa mmoja wa walemavu waliojitokeza kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wao. Wacha twende tukamwite Kamanda Tossi
Uchaguzi kwa sehemu kubwa ulikuwa wa amani sana kinyume cha matarajio ya baadhi ya watu.

October 11, 2008

KAMPENI ZAITIMISHWA LEO TARIME

Kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Tarime Mkoa wa Mara kujaza nafasi ilioachwa wazi na Marehemu Chacha Wangwe zimeitimishwa leo kwa Amani na utulivu jimbo humu. Kesho mapema vituo vipatavyo 406 na sita vitafunguliwa kuanzaia saa 12 asubui ambapo wapiga kura wapatao 146, 919 wanatarajiwa kuchagua mrithi wa Wangwe. Kila La heri wananchi wa TARIME.

October 7, 2008

Happy birthday 2 u............

JK akikata keki ya birth day. Rais JK akimlisha keki mtoto Mohamed wakati wa hafla fupi ya kusherekea miaka 58 ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na wafanyakazi wa ikulu ya Dar es Salaam leo.Mtoto Mohamed ni yatima ambaye Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma wanamlea katika familia yao.
Katibu mkuu ikulu Bwana Michael Mwanda akimpa kadi ya Birthday Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa niaba ya ya wafanayakazi wa ikulu wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Kikwete kwa kutimiza miaka 58 leo.

Mtoto wa Mkulima ziarani Namibia

"Mtoto wa Mkulima" akikaribishwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Nambia, Nahas Angula na vikundi mbalimbali vya ngoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kotako nchini Namibia kwa ziara ya kikazi

Mama Salma yuko MAKETE

Mama Salma kikwete akisalimiana na watoto mapacha walioungana miili yao,maria na consolata,11,walio darasa la 5. watoto hao wanatunzwa katika hospitali ya ikonda huko makete

WANAMEREMETAAA WANA........

Mzee Mwinyi aka Ruksa akiwa na My wife wake ktk dhifa ya kitaifa jana.

Mzee Ruksa

"Huyu ndo Mzee Ruksa uliyekuwa ukisikia habari zake Mh." JK akimtambulisha Mzee Mwinyi ktk Dhifa ya kitaifa ikulu.

USHIRIKIANO

Tanzania na Madagaska jana zilitiliana saini ushirikiano ktk nyanja mbali mbali hafla iliyoudhuriwa na Marais JK na Marc Ravalomanana Ikulu, Waziri Membe na mwenzake wa MDGS Marcel walianguka saini hizo.

THE UTAMU BLOG "MARIGIO" BYE BYE

Habari zilizotufikia ainasema kwamba Ile blog iliyokuwa inawanyima watu wengi raha iitwayo theutamu IMEFUNGIWA RASMI na bado anafuatiliwa kwa karibu na mpaka sasa imeshajulikana mwanzilishi yuko Tanzania na anashirikiana na wawili mmoja akiwa UK na mwingine US. Kibaya zaidi ni kuwa wote waliotuma barua pepe kwenda kwenye email ya utamu wako recorded na wanafuatiliwa kwa ukaribu kabisa. Watanzania wametahadharishwa waache kutumia blogs kuchafuana bila ushahidi wowote,Epuka kutuma barua pepe huko ukidhani hutojulikana...! uknet.

October 4, 2008

Mkono uso kwa macho na Obama

Wakili maarufu na Mbunge wa Musoma (V) Nimrod Mkono akisalimiana na Mgombea Urais wa USA toka chama cha Democrats Barack Obama hivi karibuni majuu.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...