September 16, 2011

Maajabu ya Dunia- Kutana na kucha zenye umri wa miaka 18!


Impressive. Chris "The Duchess" Walton demonstrates how she texts with her Guinness world record holding fingernails inside the New York Public Library in New York 14 September. Her nails measure 10 feet 2 inches on her left hand and 9 feet 7 inches on her right hand that she has been growing for 18 years.


Wakuu wa Mikoa waapishwa!

 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dr Gharib Bilali na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa mikoa mara baada ya kuwaapisha leo Ikulu.
Dr Christine Ishengoma akila kiapo

Joel Bendera akipokea zana za kazi. 

Makamu wa Rais Dr Bilali akimpongeza Mwantumu Mahiza

Kanali Massawe akitia saini hati ya kiapo. 
More pix here

Zanzibar accident UPDATES, Mmiliki wa Mv Spice Islanders 1.

Wakati huu ambapo visiwa vya Zanzibar vingali katika simanzi kuu huku hakuna idadi rasmi ya watu waliokufa na kuzikwa ama (300, 1696 au 2000!) katika meli  Mv Spice Islanders 1 baharini, (kama ilivyokuwa kwa Mv Bukoba 1996) na ambapo mapaka sasa nahodha hajulikani alipo ikiwa ni miongoni mwa waliokufa au la, angalau Mmiliki au wamiliki wamejitokeza na kutangaza kulipa fidia.
Mmiliki huyo ni Visiwani Shipping Cooperation, kampuni inayomilikiwa na:


  1. Salum Said Mohamed (Batashi) hisa asilimia 73 (Mkurugenzi)
  2. Makame Hasnuu Makame 15,
  3. Yussuf Issa Suleiman 12, 
Kwenye mitandao, hasa wikipedia mmiliki pekee anayeonekana ni Makame Hasnuu na si Visiwani Shipping Cooperation. 
Read more:Abiria waliokufa na wale waliosalimika katika ajali ya ya Spice Islander I watalipwa fidia na Kampuni iliyokuwa ikimiliki meli hiyo ya Visiwani Shipping Cooperation ya mjini Zanzibar.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Salum Said Mohammed (Batashi), amesema fidia hiyo itatatokana na malipo ya bima kati ya kampuni hiyo na Shirika la Bima la Alliance Insurance ya jijini Dar es Salaam.Alisema kampuni yake ilikata bima ya abiria yenye thamani ya Dola za Marekani 300,000, lakini alisema watu watakaonufaika na bima hiyo ni wale tu ambao wameathirika katika tukio hilo, “Abiria watalipwa bima walioathirika na wale ambao wamepoteza ndugu zao watanufaika kwa niaba yao,” alisema.Hata hivyo, alisema watu waliopoteza mizigo hawatalipwa fidia kwa sababu sheria za kimataifa bima ya mzigo inayosafirishwa kwa meli hutakiwa kukatwa na muhusika wa mzigo huo.Alisema meli hiyo ilikuwa imekatiwa bima na Kampuni iliyokuwa ikimiliki ndiyo itakayonufaika na bima hiyo, lakini hakutaja ilikuwa imekatiwa kiwango gani cha bima meli hiyo.Alisemameli iliyozama ina umri wa miaka 37 tangu ilipotengenezwa kiwandani mwaka 1974 nchini Salamis- Ugiriki na kampuni ya Goumas Shipyard. Aidha, alisema meli hiyo ilisajiliwa Zanzibar Oktoba 10, 2007 na ilikuwa ikitoa huduma kati ya visiwa vya Unguja, Pemba na Tanzania Bara. Alisema kwa mara ya mwisho meli hiyo imefanyiwa ukaguzi na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA) Disemba, 2010 na ilipelekwa Chelezoni Mombasa Julai 20 hadi Agosti 8, mwaka jana na matengenezo yote yalifanywana Kampuni ya Africa Marine ya Mombasa, “Ripoti baada ya kutoka Chelezoni Mombasa inaonyesha meli ilikuwa na uwezo wa kuendelea na kazi kama kawaida na haikuwa na matatizo yoyote,” alisema Mkurugenzi huyo.Alisema meli hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukua tani 425 za mizigo na abiria 600 na wakati ajali hiyo inatokea ilikuwa na mzigo wa tani 97 na abiria 610.

  
source: Nipashe

Mv Spice Islanders 1, Nahodha anasakwa.


JESHI la Polisi nchini limeanza kumtafuta nahodha wa meli ya mv Spice Islander iliyozama baharini katika eneo la Nungwi, Kaskazini Unguja usiku wa kuamkia Jumamosi. 

Taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa jana na Mkuu wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, ilimtaja nahodha huyo kwa jina la Said Kinyanyite, ambaye ni mkazi wa Nzasa Mbagala, Charambe, Temeke, Dar es Salaam. 

Mussa alisema nahodha huyo, ambaye hakuonekana baada ya ajali hiyo ni mzaliwa wa kijiji cha Mbwemkuru, Pande, Kilwa mkoani Lindi. 

Kamishna Mussa aliwaomba wananchi kupitia mpango wa Polisi Shirikishi Jamii, kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi endapo watapata taarifa za alikojificha, ili akamatwe na kutoa maelezo ya jinsi ajali hiyo ilivyotokea. 

Taarifa hiyo ilisema tangu kuzama kwa mv Spice Islander, hajapatikana hali ambayo imewalazimu polisi kutafuta picha yake kwa lengo la kurahisisha utambuzi kwa watu wasiomfahamu wamwonapo. 

Katika hatua nyingine, kazi ya kuopoa miili ya walionasa kwenye mabaki ya meli hiyo iliyokuwa ikifanywa kwa ushirikiano wa wapiga mbizi wa Afrika Kusini na majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, imeshindikana. 

Ofisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, alisema kushindikana huko kumesababishwa na hali mbaya ya bahari na kina iliko meli hiyo tofauti na uwezo wa wazamiaji hao. 

Igunga, CCM kwachafuka

HALI ya  siasa katika jimbo la Igunga mkoani Tabora imechafuka baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Fatuma Kimario kudaiwa kukutwa na viongozi wa
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akifanya mikutano ya ndani na viongozi wa matawi, vijiji na kata kinyume cha utaratibu.
 
Tukio hilo la aina yake liliibuliwa kwa viongozi wa
 
Chadema baada ya kuonyeshwa alama ya chama chao na kijana mmoja,  Juma Gwala ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kitongoji cha Zahanati, kuonyesha alama inayoonyesha  matusi dhidi ya msafara wa viongozi wa Chadema.
 
Hali hiyo ilisababisha walinzi wa Chadema  na Mbunge wa Maswa Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Sylvester Kasulumbayi na Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Kiwanga kumkimbiza.
 
Lakini aliwazidi mbio na kutokomea kusikojulikana.
 
Baada ya hapo, viongozi na walinzi wa Chadema walirudi kuendelea na mkutano wao ambao ulikuwa umbali wa mita zipatazo 60 kutoka mkutanoni.
 
Wakati mkutano huo ukiendelea, ghafla kijana mmoja ambaye hakufamika, alipaza sauti na kusema DC yuko kwenye ofisi za kijiji, huku akidai kuwa anagawa fedha kwa viongozi wa vijiji.
 
 
 
Hali hiyo  ilizua mtafaruku na kusababisha watu wengi kukimbilia kwenye ofisi hizo na kumkuta DC Kimario akiwa na viongozi  na wazee  maarufu wa eneo hilo.
 
Walimtia misukosuko ya hapa na pale, huku wakimpiga makofi hadi wakamtoa nje ya ofisi.
 
Baada ya watu mbalimbali kuingia ndani ya ofisi, walimkuta DC Kimario akiwa na msaidizi wake ambaye ji a lake halikutambulika, wakiwa na nyaraka mbalimbali zinazoonyesha ajenda za kikao hicho.
 
Miongoni wa ajenda hizo  ni uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Igunga, kuhakikisha wageni wanaoingia kijijini au kitongojini taarifa zinatolewa kwa mtendaji wa kijiji.
TIMU ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeingia katika msukosuko mkubwa wa chini kwa chini baada ya kiongozi mmoja mwandamizi anayeongoza kampeni hizo (jina tunalihifadhi) kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu, Tanzania Daima limebaini.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika katika Ofisi Ndogo za CCM Makao Makuu jijini Dar es Salaam na kutoka Igunga zinaeleza kuwa tukio hilo limesababisha kujeruhiwa vibaya kwa mwanamke huyo.

Ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini alisema sakata hilo lilianza baada ya mume wa mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo anayeongoza kampeni za chama hicho kuvamia chumba ambacho watuhumiwa hao walikuwamo na kuanza kumwadhibu mkewe kwa kipigo.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, wakati vuta nikuvute kati ya mke na mume ikiendelea chumbani, kigogo huyo wa CCM alifanikiwa kutoroka na kuwaacha wanandoa hao ambao wote wawili ni makada wa CCM wakiendelea kupambana.

Habari zinaeleza kwamba mtafaruku huo ulimsababishia mwanamke huyo aliyekuwa miongoni mwa kundi la mabinti wapatao 10 wanaotumika kuhamasisha kwenye kampeni hizo majeraha makubwa yaliyomlazimisha apelekwe hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Chanzo kingine cha kuaminika cha habari kililieleza gazeti hili kwamba kabla ya kwenda hospitalini, mwanamke huyo alilazimika kupita katika kituo cha polisi cha Igunga ili akapatiwe fomu maalum ya idhini ya matibabu (PF3).

Inaelezwa kwamba mara baada ya kufikishwa kituoni hapo na wasamaria wema, mwanamke huyo (jina tunalo) alitakiwa kwanza kulitaja jina la mtu aliyemsababishia majeraha hayo na akajikuta akipata wakati mgumu kumtaja mumewe.

Habari zinaeleza kwamba taarifa za tukio hilo zilipofika katika ofisi za CCM wilaya ya Igunga, maofisa wa chama hicho waliingilia kati na kuamua kulizima jambo hilo chini kwa chini ili kuepukana na hatari ya kuvuruga kampeni nzima za ubunge cha chama hicho.

“Ni kweli tumepokea habari za kusikitisha kuhusu kiongozi wetu mmoja wa juu katika kampeni kukumbwa na kashfa ya kufumaniwa na kusababisha mwanamke aliyadaiwa kuwa na uhusiano naye kupata kipigo kikali kutoka kwa mumewe ambaye pia ni kada maarufu wa 


Soko kuu Mwanjelwa Mbeya linateketea kwa moto.

Hali hilivyo huko Mbeya leo hii baada ya moto kulipuka na kuanza kuteketeza Soko kuu la Mbeya, Mwanjelwa. Picha kwa hisani ya Rama Msangi. 


Hii ilikuwa Dec 2006 baada ya soko hilo hilo kuteketea kwa moto, aliye kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Juma Akukweti na timu yake akiwemo Mpiga picha wa Idara ya Habari Maelezo Teddy Nyantori walienda kukagua uharibifu huo, Teddy hakurudi, alifariki, Akukweti naye akukukaa sana alimfuata ni baada ya ndege waliyokuwa walimokuwamo kupata ajari. 

Igunga, Ngoma inogile

CHADEMA WAMKAMATA MKUU WA WILAYA YA IGUNGA. 

VURUGU zimezuka jana katika Kata ya Isakamaliwa, wilayani Igunga zikiwahusisha viongozi wa Chadema na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.Katika sakata hilo, wanachama wa Chadema walimkamata Mkuu huyo wa Wilaya kwa tuhuma za kuendesha mkutano wa ndani na watendaji wa serikali za vijiji, wakati akijua kuwa kulikuwa na mkutano wa kampeni za chama hicho karibu na eneo hilo.
 
Msafara wa Chadema ulifika katika eneo la kampeni saa 8.00 mchana na kabla mkutano haujaanza, Meneja Kampeni wa chama hicho, Sylivester Kasulumbai, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkuu wa wilaya ya igunga alikuwa akifanya kikao cha ndani katika eneo hilo kinyume na taratibu, hivyo wanakwenda kumshughulikia.
 
Kasulumbai ambaye ni Mbunge wa Maswa Mashariki akiwa na Mbunge wa Viti Maalum, Susan Kiwanga, baadhi ya wananchi na vijana wao, walifika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata kulikokuwa kunafanyika mkutano huo na kuanza kuhoji aliko Mkuu huyo wa Wilaya.
 
Mmoja wa wananchi alimnyooshea kidole mama ambaye alikuwa amekaa mbele na kusema; “..yule ndiye Mkuu wa Wilaya”.Kundi hilo la vijana na viongozi wa Chadema, waliingia katika ukumbi huo na kumtoa nje mama huyo huku wakimtaka aeleze kwa nini anafanya vikao vya ndani katika Kata hiyo wakati anajua kuwa chama hicho kilikuwa na mkutano katika eneo hilo.
 
Kitendo hicho kilizua purukushani na kutokuelewana kati ya waliokuwa kwenye mkutano wa ndani na viongozi wa Chadema, jambo lililovuta umati mkubwa wa watu.
 
Maelezo ya DC
Baadhi ya vijana wa Chadema walikuwa wamewashikilia watu waliokuwa wakishiriki mkutano huo huku mama huyo akitolewa nje na kuketishwa kwenye kiti alitakiwa atoe maelezo kuhusu mkutano wake.
 
Baada ya kukaa kwenye kiti huku akionekana kuchanganyikiwa, alisema yeye ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga, jina lake ni Fatma Kimario na kwamba, hakuwa na taarifa za mkutano wa kampeni za Chadema.
 
“Sina ratiba, iko katika ofisi za halmashauri, hivyo sikujua kama kuna mkutano hapa, hata hivyo watu walikuwepo niliwaruhusu waende mkutanoni na mimi nilikuwa naondoka sasa hivi,” alisema na kuongeza:
 
“Nilichokuwa nafanya ni mkutano wa viongozi wa serikali kwa ajili ya kuangalia hali ya mifugo inayoibwa sana, elimu kwa wote hasa watoto na ujenzi wa nyumba bora na masuala ya amani”.
 
Kimario aliwasihi wafuasi wa Chadema kusoma karatasi ya ajenda ili wafahamu kilichokuwa kikijadiliwa kwenye kikao hicho.
 
Karatasi aliyokuwa akiizungumzia Mkuu huyo wa Wilaya ilikuwa na ajenda tano za kikao hicho ambazo ni; Uhamishaji wa mifugo; Kuwa na choo chenye ubora na nyumba bora; Elimu;  Mipaka ya shule na ajenda ya mwisho ilikuwa Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga.
 
Hata hivyo mbunge Kiwanga alimtaka mkuu huyo wa wilaya aeleze tangu lini kikao cha viongozi wa serikali kikahudhuriwa na wazee maarufu na mabalozi wa nyumba kumi, swali ambalo lilionekana kumchanganya mkuu huyo wa wilaya kwa kutoa majibu tata.

Google+ Followers

There was an error in this gadget
There was an error in this gadget

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...