September 30, 2010

Kila la kheri Genevive

Miss Tanzania 2010,Genevive Emmanuel, ameondoka leo hii kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya ulimbwende ya dunia (Miss World 2010) yanayotarajiwa kufanyika huko Sanya nchini China tarehe 30 Oktoba 2010.

Kura ZERO ina maana gani?

Katika pitapita zangu kule NEC nikitafuta kuona landa patakuwa pamewekwa majina ya wagombea wote wa mwaka huu japo wa urais tu bila mafanikio, katika chimbuachimbjua ndani ya mtandao huo nakutana na matokeo ya mwaka 2005, nikacheki ya Dar kwanza, si mwajua ndo Tanzania yenyewe, huko nakumbana na matokeo hayo,
Kwamba uchaguzi ule kuna watu walipata ZERO ama buyu, sielewi, yaani hata yeye mwenyewe hakujipigia kura? mbali na mkewe au jirani, ndugu ama jamaa nk..
Mhh habari ndo hiyo.

Kampeni Zanzibar

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM mkutano wa kampeni Mkoa wa kaskazini Unguja.
na Amour Nassor VPO.

September 29, 2010

Ni miaka mitatu sasa

Miaka 3 imetimia leo hii, mengi yamepita hapo lakini bado naona kama jana tu.
Asante BWANA wa Majeshi kwa kutupigania kutulinda na hata kutufikisha leo hii, hakika sisi peke yetu hatuwezi, sifa na utukufu ni kwako BWANA.

photojournalism as a career: 9 things you need? Besides A camera

You’d be wrong (and you will not be the only) if you think you just need X thousand dollars on some top professional camera equipment, and you’re on track to become a successful photojournalist. It takes a whole array of skills. So ok, what do you need? Here is a list of 9 things that are important to make it as a photojournalist – besides camera

1!. Flair for the visual

saying. You need to have some talent, be artistic and have creativity in the visual world. Some are born with a stunning visual consciousness, others need to develop it. We now live in a visually-saturated world, so it’s easy to find sources of inspiration. Go to shows, reading photography books, look in magazines, etc. Find out what style you like. Do not try to copy it but use it as inspiration to create your own visual style. Anyone can take a picture of something. Professional photojournalists have to do it with style!

second Technical know-how

You must know some basics about the technical side of photography. Not much, really, and not very difficult. You do not need an engineering degree the lens or something. But we live in a digital world and beyond camera / lens, it will be useful for you if you are handy with a computer and photo software. You must use it all the time! Knowing some basics about web design and multimedia production can also be of great benefit.

third Business savvy

Do not think that if you made a beautiful photo story, someone out there will automatically find it and pay you nicely for it. Someone, perhaps, but you can wait long for that to happen. This is where you have business savvy. Try to learn about the image industry and the market you are in. Develop negotiating skills. Be prepared to turn down a sale if you do not like the conditions. It pays in the long term! And have good business practices in general, so your customers will recommend you and get back to you again and again: Be professional. Show up prepared and on time. Deliver what you promise when you promise. There is no room for error in professional photography. Thinking ahead when it comes to business.

4th Money in the Bank

If you are just starting out as a freelance photographer / photojournalist, you will probably need to hang for a while until you have generated enough revenue sources to keep you afloat. This can be anything from 6 months to 6 years. Depending on your talent, savvy, commitment and happiness! Even if you work as a pretty established freelancer, next month’s income is not always safe. Photographic equipment is expensive, it must be maintained and replaced every now and then. So it takes a bit of capital to avoid going broke in the process of building your career.

5th A good physical shape

Oh yes, it is a physical work! You do not have to be an Olympian contestant, but you need to be prepared to stand or walk for long periods, sometimes carrying heavy equipment. In all weathers. At all times of day (and night). And sometimes in risky situations where you might have to run fast!

6th Nerves of steel

in these questionable situations or when the adrenaline kicks in for any reason, you should keep your calm, compose, and time your shots, get the right angle, focus and exposure. In less dodgy, more everyday situations, you must have nerves to break the ice, get intimate with strangers, steps away from the crowd and not to freeze when you finally face to face with the moment you’ve been waiting for.

7th Persistence

When pursuing a shot, a story or a sale, do not give up when someone says no. Look for other ways to achieve your goal. If it were easy, everyone would already have done it! Sometimes it’s just a matter of being patient. If something did not work the first time, so wait a bit and try again.

8th Know your history

work as a photojournalist, it is also important that you have something to say. Not just take boring pictures of beautiful or ugly things. Photography for the sake of photography called art photography. Not photojournalism. Make sure you have an idea or some intent with your work.

9th Passion

As I wrote in the beginning, it is not always easy being a photojournalist. So it’s important to enjoy your work. Have fun! If you are not happy and not worry about your motives, it will show up in your images. So enjoy your work!

Good luck!

The author, Morten Svenningsen, is working as a professional photojournalist in Nepaland is also the founder and CEO of Gaia Photos, an international forum for the global photojournalism online . With a team of top photojournalists from around the world, Gaia Photos your ability to follow and comment photojournalistic work since it is produced and published! Click the link above to visit!

September 28, 2010

Orijino Komedi katika kampeni za JK

Kundi la Orijino Komedi wakiburudisha wakazi wa Shinyanga katika Uwanja wa Kambarage kabla ya JK kupanda jukwaani kuomba kura.

September 27, 2010

If thats true, you made my day! @VODACOM

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ya Intaneti ambayo itawawezesha wateja wake kuchati kwa intaneti bure.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba alisema jana kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kuchati bure kwenye tovuti za Face Book, the Grid na Vodamail.
Alisema Vodacom Tanzania inatoa huduma hiyo kwa lengo la kuwawezesha wateja wake kupata muda wa kuchati zaidi.
Alifafanua kwamba hayo yote yatawezekana kwa kutumia mtandao wa 3G ambao una kasi na nguvu kubwa.
“Tunapenda wateja wetu watumie mtandao wetu kwa kuwasiliana bure na hivyo kukata kiu yao ya mawasiliano”.
Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma hiyo ya mtandao wa Intaneti.
Aliwaomba Watanzania kujiunga na Vodacom ili kupata huduma hiyo bure na hivyo kuwasiliana zaidi.
Alisema huduma hiyo itapatikana kwa simu za mkononi na pia kwa Laptop zilizounganishwa na USB Modem.
My take:
Ki ukweli sijawai kuwa mteja wa Vodacom, (usiniulize, sijui ni kwanini) lakini kwa ofa hii na hasa kama itakuwa inapatikana katika modem ambapo itaniwezesha kutumia katika laptop yangu na si kwenye simu peke yake, na iwe UNLIMITED ACCESS, Sio siri leo hii hii na si kesho nitajiunga haraka sana.
Lakini ni nani wa kunihakikishia hilo? Bi Makamba au Bw Mafuru? gharama za internet kwa sisi wengine imekuwa kama damu maishani mwetu ktk dunia hii iliyochanganyikiwa na mtandao (ICT ERA), uwa najiuliza siku nitakayo amka na kukuta mitandao imeparaganyika, sijui itakuwaje, na kwa hakika sitaki kuota wala kujua siku iyo.
.

September 23, 2010

Hiki ndicho Raia Mwema walichoandika

Wanamtandao wampa Dk. Slaa ushindi 76%

Daily News walimkubali kwa 60%

Synovate wakana madai ya CHADEMA kumpa 45%

WAKATI kampuni ya kibiashara inayojihusisha na tafiti ya Synovate Limited ikikanusha taarifa za kubaini kwamba mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa sasa anakubalika zaidi, Watanzania wanaotumia mitandao wamempa mwanasiasa huyo asilimia kubwa ya ushindi kulinganisha na wagombea wengine.

Ufuatiliaji wa Raia Mwema, katika mitandao mbalimbali ukiwamo ule wa gazeti la Serikali la Daily News (Daily News Online Edition) na mtandao maarufu kwa mijadala wa Jamiiforums unaonyesha kwamba Dk. Slaa anakubalika zaidi katika mtandao kuliko wagombea wengine akiwamo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Hata hivyo, kumekuwa na angalizo katika mitandao kwamba si Watanzania wengi wanaotumia mitandao hata kama kuna ongezeko kubwa la matumizi ya mtandao kupitia simu za mikononi, hoja ambayo bado inaweza kutoa taswira tofauti katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, kutokana na wapiga kura wengi kuishi vijijini na wanaoishi mijini kutofahamu chochote kuhusu mtandao kama anavyosema na mchangiaji mmoja katika mtandao wa Jamiiforums:

“Ingekuwa JF (Jamiiforums) inasomwa na asimilia 50% tu ya Watanzania wote, basi, Dk. Slaa angepita kiurahisi sana. Lakini kwa kuwa wengi hawapiti humu inabidi juhudi za ziada zifanyike kushinda”.

Kura za maoni zilizokuwa zikiendeshwa na Daily News zikiwa na swali: ‘Will Dr. Slaa win the presidential race? ‘ (Je, Dk. Slaa atashinda urais?) zilionyesha kwamba kati ya watu 161 wa mwanzo waliopiga kura walionyesha kumpa Dk. Slaa asilimia 60.87 na ‘Hapana’ walikuwa asilimia 28.57, kabla ya kura hizo kusitishwa, kutokana na taarifa za kuwapo hofu ya ‘uchakachuaji’ uliodaiwa kufanywa na wafuasi au wapinzani wa Dk. Slaa.

Kwa upande wa mtandao wa Jamiiforums, zaidi ya watu 6,420 wamepiga kura hizo za maoni na kuonyesha kwamba Dk. Slaa amekubalika kwa watu 4, 895 sawa na asilimia 76.25 akifuatiwa na Kikwete ambaye anaonekana kukubalika kwa watu 779 katika mtandao huo, sawa na asilimia 12.13 akifuatiwa kwa karibu zaidi na Hashim Rungwe wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 448 (6.98%) wakati mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akikubalika kwa watu 205 (3.19%) na Mutamwega Mugahywa wa TLP akikubalika kwa watu 93 (1.45%).

Mwazilishi wa mada hiyo ya kura za maoni aliweka swali “Je,Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?” Kabla hata ya majina ya wagombea kutangazwa na yeye mwenyewe kutangaza kuwania nafasi hiyo, Dk. Slaa alikuwa akitajwa kuwania nafasi hiyo na orodha ya majina kubandikwa mtandaoni badaa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza orodha ya wagombea hao.

Wachangiaji wengi katika mtandao huo wa Jamiiforums ambao baadhi ya watu wanautuhumu kupendelea wapinzani, wamekuwa wakitoa sifa kuu za mtu anayestahili kuwa Rais wa Tanzania na kumchambua Kikwete kuwa amepoteza sifa za kuendelea na nafasi hiyo kutokana na kushindwa kupambana na ufisadi kikamilifu kama alivyoahidi wakati akiingia madarakani mwaka 2005.

Miongoni mwa sifa walizoanisha katika mtandao huo ni pamoja na kuwa Rais ajaye anatakiwa awe ni msomi, mkimya, mchapa kazi, hana makundi na asiye na chembe ya ufisadi.

Kabla ya majina ya wagombea kutangazwa, wachangiaji waliwataka wagombea wa Upinzani mwaka 2000 na 2005 wasijitokeze tena mwaka huu akiwamo Freeman Mbowe wa CHADEMA, Lipumba wa CUF, Augutine Mrema wa TLP na John Cheyo wa UDP kwa maelezo kwamba matokeo ya nyuma yanaonyesha kwamba hawana jipya mwaka huu.

“Wanachotakiwa kukifanya sasa hivi ni kumchagua mtu tofauti kabisa. CCM hawawezi kubadilika. Rais ni nafasi ya Slaa sasa kwa ajili ya kusafisha na kuziba mianya ya ufisadi mkubwa. Baada ya hapo tunaweza kuchagua Rais mchumi ili ajenge uchumi wa nchi. Kwa sasa lazima tuondoe ufisadi kwanza, CCM hawawezi kuuondoa.

“Kikwete alisema anawajua wala rushwa, wauza madawa ya kulevya, wezi wa EPA waliorudisha fedha na wale wahujumu wa Bandarini lakini kashindwa kuwataja wala kuchukua hatua ilhali yeye tumempa mamlaka yote kikatiba ili ailinde nchi hii na mali zake.

“Slaa ni mzalendo wa kweli maana pamoja na kuwa hana mamlaka ya kuwafanya lolote mafisadi lakini kawataja hadharani bila woga au kuumauma maneno ingawa anajua hatari inayomkabili kupambana na watu wa aina hiyo. Huyu akipewa mamlaka ya kuongoza nchi mafisadi, wezi wa mali za umma nk, itabidi wakajichimbie makaburi wajizike wenyewe. Slaa ndio Rais anayefaa kwa wakati huu tulionao,” anasema mchangiaji mmoja wa Jamiiforums.

Baadhi ya vyombo vya habari wiki hii vilimnukuu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akisema kuwa CHADEMA ina matokeo ya kura za maoni za Synovate yanayoonyesha kuwa Dk. Slaa anakubalika kwa asilimia 45 akifuatiwa na Rais Kikwete mwenye asilimia 41, kauli iliyowalazimu Synovate kukanusha.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Jumatatu, Meneja wa Synovate Limited, Aggrey Oriwo alisema taarifa hizo ni za kughushi, hazina ukweli wowote na zinaupotosha umma kwa kuwa hawajawahi kufanya utafiti wowote unaohusu kukubalika kwa wagombea wa urais.

Oriwo alisema kwa kawaida kampuni yao hufanya utafiti wa hali ya kisiasa kila baada ya miezi mitatu na kwamba wanatarajia kufanya hivyo kabla ya Oktoba 31 na kutoa taarifa yao, kauli iliyotolewa pia na Taasisi ya Mpango wa Utafiti na Elimu Demokrasia Tanzania (Redet), ambao nao wanatarajia kufanya utafiti wa mgombea anayekubalika.

Leave Daily News out of that hopeless adventurism, please - Editor

A vividly pro-Willibrod Slaa weekly tabloid has used our name in a shameful attempt to prop up the Chadema presidential candidate’s campaign, suggesting that he was being backed by three quarters of local internet surfers.
In its lead story on Tuesday, the September 22-28 edition of the tabloid deliberately misused an online poll involving a mere 161 visitors to purport that the whole nation was behind Slaa. While noting the tabloid editors’ virtual confession that they cannot be believed without quoting the Daily News, we abhor the unprofessional decision to use our name to lend credence to their wildly hopeless adventure.
The editors of the tabloid know that the figures they used are quoted out of context and are absolutely unrealistic. That is why they confess in the fabricated report that very few Tanzanians have access to the internet and that the purported poll results do not reflect
what will come out of the October 31 ballot.
So why would they venture out with old poll results today? Vicious anti-establishment fervor at best and malicious conspiracy to settle old scores at worst. That is typical activist journalism practiced by a section of the media, which has openly identified with the opposition and plays down any positive achievement of President Kikwete’s government while orchestrating purported failures, mostly made up ones.
The attempt to enlist the support of the Daily News was apparently meant to save another tabloid blushes after carrying an equally wild fabrication to the effect that Synovate had censored results of a poll showing Slaa leading president Kikwete by four points in popularity. The pollster has publicly derided the tabloid and lodged a complaint with the Media Council.
It is high time that section of the media learnt its lessons and returned to professional practice. We think there is nothing particularly wrong in covering presidential aspirants favourably, but the reports must at least be true. And the truth is that DrWillibrod
Slaa will not be the fifth president of Tanzania.
The Chadema candidate has a lot of issues to settle, beginning at family level, from which he will need to practice leadership upwards. He will, indeed, garner some votes in October, just like Augustine Mrema in 1995, but that will be it, and the media behind the former priest can quote us on that.

Mh akiomba kula!!

September 21, 2010

Ati Tangazo hili limekatazwa kuoneshwa luningani????

Photojournalism in Tanzania: More Zenji images

Photojournalism in Tanzania: More Zenji images: "Tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana, wake kwa waume na hasa mijini ni kubwa sana kwa Zanzibar na Tanzania kwa uju..."

Photojournalism in Tanzania: More Zenji images

Photojournalism in Tanzania: More Zenji images: "Tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana, wake kwa waume na hasa mijini ni kubwa sana kwa Zanzibar na Tanzania kwa uju..."

Fashion hizi zitatumaliza

Mwanamuziki Lady Gaga katika vazi la nyama, (sijui ni kitimoto, mbuzi au ngombe?)

Kumbe tukiamua, tunaweza kuondokana na adha hii!

Kwa kuweza kuchangisha Billion saba kwa usiku mmoja sio siri CCM (ama Katibu MkMakamba) wanastahili pongezi za dhati kabisa, sina kumbukumbu sahihi ni harambee hipi iliwahi kuchangisha pesa zote hizi kwa usiku mmoja tena ikiongozwa na Katibu wa chama tu, lakini kwa kumbukumbu ndogo niliyonayo naamini hii imevunja rekodi (niko tayari kusahihishwa) ya harambee zote.
Nilikuwa najiuliza iwapo Makamba kaweza kuchangisha pesa zote hizo kwa ajili ya kampeni za chama kimoja tu? je ingekuwaje kama Waziri Mkuu angekuwa achangisha kwa ajili labda ya madawati kwa shule nchi nzima? na ingepatikana kiasi gani kama mchangishaji angekuwa ni Makamu wa rais labda kwa ajili ya vitanda na madawa hospitalini?
Na je ingepatikana mabilioni mangapi kama mchangishaji angekuwa ni mwenye nchi mwenyewe yaani Rais kwa labda miuondombinu ama maendeleo ya taifa kwa ujumla?
Nathani Makamba kaonesha njia kuwa kama tukiamua tunaweza kutatua matatizo yetu wenyewe kwani sisi si masikini na wala MUNGU hakuumba WaTanzania masikini ndio maana kabla hajatuumba alitundalia kila aina ya mali ardhini na baharini ili zitunufaishe sisi.
Kumbe tukiamua nasema TUKIAMUA wanafunzi hawa wa Shule ya Msingi Mahanga huko Kigoma vijijini wanaweza kusoma kwa raha, lakini ni kama kweli tuna utashi wa kuamua ama tunaguswa kweli na hali hii.

September 15, 2010

Salam toka kwa Atukuzwe, Ujiji

Mama na Mwana na Guardian Angel mpo? Atukuzwe toka UJIJI Kigoma mwisho wa Reli ana wapa Hi woooooooote.

Salam toka Kigoma aka MWISHO WA RELI

Kina mama wa Mwisho wa Reli ni waangaikaji haswaa, pamoja na kusumbuliwa na jamaa zetu lakini hawakati tamaa.

September 14, 2010

JK amtambulisha JM Bumbuli

Mgombea urais wa CCM JK akimtambulisha mgombea Ubunge January, mwana wa Makamba na aliyekuwa msaidizi wa karibu wa JK.

September 12, 2010

Miss Tanzania 2010,

Geneviva Mpangala ndiye Vodacom Miss Tanzania 2010, mshindi wa pili ni Groly Mwanga na wa tatu ni Consolata Msofe.
Kwa hisani FullShangweblogspot.

Bongo Pix: Da Chemi, waikumbuka hii?

Bongo Pix: Da Chemi, waikumbuka hii?: "Katika kusherehekea sikukuu ya Idd niliamua kutembelea mji mkongwe wa Ujiji Kigoma nilipata fursa pia ya kufika katika makumbusho ya Dr Liv..."

Bongo Pix: Da Chemi, waikumbuka hii?

Bongo Pix: Da Chemi, waikumbuka hii?: "Katika kusherehekea sikukuu ya Idd niliamua kutembelea mji mkongwe wa Ujiji Kigoma nilipata fursa pia ya kufika katika makumbusho ya Dr Liv..."

Salamu toka Ujiji

Jamaa ana andaa "New World Cinema" ya Ujiji tayari kwa movie katika kusherehekea Sikukuu ya Idd.

Da Chemi, waikumbuka hii?

Katika kusherehekea sikukuu ya Idd niliamua kutembelea mji mkongwe wa Ujiji Kigoma nilipata fursa pia ya kufika katika makumbusho ya Dr Livingston, kuna vitu vingi vya kuona na kujifunza kwa historia, kuna picha nyingi na cutting kibao, hii ya Da Chemi wakti akiwa Daily News ilinivutia, sijui ka bado wakumbuka stori hii, siku ukienda Kigoma Da Chemi fika pale Ujiji pia.

September 11, 2010

Kampeni 2010 na Fede

from artsfede.blogspot.

Mambo ya Mchina na Fede

Katuni kwa hisani ya fedeblogspot.

Miss Tanzania 2010 Live Star Tv leo

Crew Nzima ya Star Television wakiwa katika picha ya pamoja pembeni mwa OB Van yao ya kurushia laivu Shoo nzima ya Vodacom Miss Tanzania 2010 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo. Ni mrembo yupi kuibuka kudedea? tusubiri tuone hapo usiku wa manane leo. Asante mdau Full shangwe kwa photo.

September 4, 2010

Blogger azindua kampeni za Ubunge

Dr, Blogger and soon Mh Faustine aka Faustine Balaza amezindua rasmi kampeni za kuwani ubunge jimbo la Kigamboni hapo jana shughuri ambayo ilikuwa na baraka kiongozi wa juu kabisa wa chama ambaye pia ni Rais na Rais mtarajiwa Dr Jakaya Kikwete.
BP inakutakia kila la kheri katika mbio hizi za kuelekea mjengoni kama wengi waitavyo, hapana shaka safari yako itakuwa njema kwani vizingiti ulivyovuka (kwenye maoni) ni vikubwa kuliko vilivyobakia.
Kila la kheri.

September 2, 2010

SUPU YA MAWE RUKSA KENYA

Changaa drinking has now been legalized, but with a catch. The law will come into effect in 90 days.

This comes after President Kibaki assented to the alcoholic drinks control bill, 2009 effectively legalizing chang'aa and streamlining the licensing, manufacture and consumption of alcoholic drinks.

And as Chris Wangombe reports, Naivasha MP John Mututho who introduced the private members bill said this is a milestone, adding that the bills intention was to roll back the negative effects of illegal alcohol consumption, which has seen several hundreds of people die.

Source: Citizen TV

SIMU YA KIFO!!!!

The Ministry of Information and the police force have dismissed as rumors text messages cautioning mobile phone owners from picking calls from specific numbers in red color, which are claimed, could cause brain haemorrage and death.

Information and Communications Minister Samuel Poghisio has further cautioned those forwarding the text messages saying that he will publish their names for prosecution.

The numbers are said to originate from the Internet to specific people's phones who spread the rumor to the public causing panic

Kampeni njema JK - Ban Ki Moon

BAN KI MOON AMTAKIA KHERI JK KWENYE UCHAGUZI MKUU

NEW YORK-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amemtakia kampeni njema , Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na mafanikio mema katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Octoba.

Ban Ki Moon ametoa salamu hizo wakati wa Mazungumzo yake na Mwakilishi mpya wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue, mara baada ya Balozi huyo kumkabidhi hati zake za utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa UN, pamoja na kumtakia kila la kheri na mafanikio Rais Kikwete, pia amempongeza Rais Kikwete na Tanzania kwa ujumla kwa kuwa nchi kiongozi na ya mfano wa kuigwa Barani Afrika katika kutekeleza na kuendeleza malengo ya Umoja wa Mataifa. Hususani amani na usalama Duniani

Aidha Ban Ki Moon, ameonyesha imani kubwa kwa mwakilishi huyo wa Tanzania huku akimpongeza kwa nafasi za ubalozi alizoshika nchini Kanada na Marekani kabla ya wadhifa wake huo mpya.

Akamtaka kuendeleza msimamo wa Tanzania wa kuwa nchi kiongozi katika Afrika na ndani ya Umoja wa Mataifa kwa kudumisha na kuendeleza malengo yenye maslahi kwa Serikali ya Tanzania, Bara la Afrika na Umoja wa Mataifa kwa ujumla.

Ban Ki Moon akatumia pia nafasi hiyo kutoa shukrani zake, kwa mtangulizi wa Balozi Sefue, Balozi Augustine Mahinga ambaye katibu Mkuu alimteua kuwa mwakilishi wake maalum huko Somalia.

Katibu Mkuu akabainisha kuwa kutokana na heshima kubwa ambayo Tanzania imejijengea ndani ya Umoja wa Mataifa, anaitegemea Tanzania katika kuwasiliana na mataifa mengine hasa yale yanayoendelea.

“Tanzania mmejijengea heshima kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa, kwa hiyo usitegemee kuwa utakuwa unaisemea Tanzania peke yake, bali na mataifa mengine pia, na hilo ndio tegemeo langu kubwa kutoka kwako Mhe. Balozi” akasisitiza Ban Ki Moon.

Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu amemhakikishia Mwakilishi huyo wa Tanzania ushirikiano kutoka kwake yeye binafsi na sekretariati ya Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake, Balozi Ombeni Sefue amemwahidi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwamba atafanya juhudi zote kuendeleza maslahi ya Tanzania katika UN, kudumisha ushirikiano mzuri kati ya UN na Tanzania, na kuchangia katika kuendelelezaji wa majukumu na malengo ya Umoja wa Mataifa.

Akatumia nafasi hiyo Kumpongeza Katibu Mkuu kwa kusimamia vema utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia, huku akimwomba aendelee kuzihimiza na kuziomba nchini zenye uwezo mkubwa kiuchumi ziendelee kuzisaidia nchi zisizokuuwa na uwezo ili ziweze kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Millenia.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...