August 17, 2009

JK na hadithi ya Nabii kutokukubalika kwao

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali muasisi wa TANU na CCM Mzee Omar Selemani Mwenye umri wa miaka 104 aliyelazwa katika hospitali mkoa wa Dodoma. Mzee Omar Selemani ni mweyekiti wa Umoja wa wazee Mkoani Dodoma.Wakati wa harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika Hayati Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alikuwa akifikia nyumbani kwa Mzee Omari Selemani na kufanya shughuli za siasa
Naomba kwanza nikiri hapa kuwa si kawaida yangu kumwaga ngojera ktk Bongo pix bali taswira zaidi, lakini yapo ambayo wakutana nayo na uwezi kuyaweka ktk taswira ili watu wajionee hivyo wafanyaje? watoto wa mjini wanasema unakubali yaishe.
Hivi karibuni nilipata bahati ya kutoka nje ya nchi kidogo na kwenda Jo'burg kwa Mzee Madiba katika kuongeza ama kujinoa zaidi na taaluma yetu hii ambayo yabadilika kila uchao, yapo mengi niliyaona na kuyasikia katika juma zima nililokaa huko bondeni, mazuri na mabaya pia lakini moja wapo ya ambayo nilisikia mara kwa mara ni juu Rais wetu JK na vile jinsi ya wenzetu wamwonavyo.
Siku ya kwanza ya darasa letu tulianza kwa utambulisho kama ilivyo kawaida au ustaarabu kwa sehemu zote watu wakutanapo mara ya kwanza, niliposena kuwa natoka TZ nilipata macho mia mia toka kwa washiriki ka watatu hivi, mwanzo sikufahamu kwa nini ila nilikuja jua baadaye wakti wa breki, kulikuwa na washiriki toka Cameruni, Comoro, Afrika Kusini, Sao Tome and Principle, Tanzania na Zimbabwe, wakti wa mapumziko hayo walikuja kunisalim kwa karibu zaidi washiriki toka Comoro, Zimbambwe na Afrika Kusini, walikuja si kunisalimu tu na kutaka kujua zaidi habari za Bongo na zaidi Rais wetu JK, wote (sijui kama waliambiana) walimsifu kwa namna ya pekee JK na kuonyosha kumkubali kwa jinsi vile anavyoendesha nchi, na kuonyesha wazi kuwa wanatonea wivu sana kuwa na rais kama huyu. Mi sikuwa na la kusema kwa sababu kwa akika si kitu nilikitarajia, na labda sidhani kama WATZ nao ndivyo wamwonavyo au la sijui kwani sijawai kufanya utafiti huo, lakini pia nilidhani labda ni kutokana na kauli ya Rais Obama aliyoitoa wakti wa kuanza ziara yake ya kwanza barani Afrika, sijui, lakini kila mmoja alikuwa na sababu yake tofauti kabisa na hilo, mfano Mzimbabwe ye alisema JK alikuwa ni Rais pekee aliyethubutu kumnyooshea kidole Mugabe ktk kikao cha wakuu wa SADC na kupelekea kutoa tamko lile lililosomwa na Waziri Membe ambalo limepelekea kuwa na serikali ya umoja, anasema japo hali ya kiuchumi haijatengemaa na kuwa wanalazimika kutumia pesa za kigeni hata kununua chungwa na kuwa Zimdollar yalipia Daladala tu lakini angalau kuna utulivu wa kisiasa ambao anazani una mchango mkubwa wa JK. Mcomoro anamwona ni kiongozi shujaa hasa kwa kuthubutu kutuma majeshi kukomboa kisiwa cha Anjuani na kumwondosha Mtawala Mohamed Bacar mbali na juhudi nyingine za upatanishi wa kidiplomasia barani Afrika na zaidi mgogoro wa Kenya. Msauzi anamwona ni kiongozi wa mfano barani Afrika, haya ni baadhi tu ya yale niliyoyasikia au kuyakumbuka angalau kwa sasa kwani kwa siku sita nilizokaa Jo'burg ni mengi yaliongelewa ni sifa nyingi zilimiinwa kiasi cha hata washiriki wengine ambao hawakumjua JK kufanya kazi ya ziada kwenye mitandao kusaka habari zake na TZ kwa ujumla. Siku ya kuondoka nilipata bahati ya kukutana na baadhi ya wabongo wenzangu pale uwanjani na bila kuchelewa tulijikuta tuna chati haya na yale mmoja akitokea Harare na mwingine Jo'burg na sote tukirejea Dar, mara likaibuka ktk maongezi yetu hili la JK na jinsi anavyokubalika na zaidi Wazim wanavyomkubali, ikabidi kujiuliza kulikoni JK? na kwa hakika sidhani umaarufu huu au sifa hizi wampazo watu hawa je anazipata hapa nyumbani? au ndo nabaii uwa akubaliki kwao? Haya yamewapata manabii wengi Bwana Yesu akiwamo. Je weye mdau wasemaje?

1 comment:

BC said...

Bernard,
Inapendeza kuona Rais wetu anapewa sifa kama hizo ulizozishuhudia huko kusini.Ni kweli kwamba Rais JK ni mtu ambaye wengi tunaweza kujifananisha naye kwa kuangalia historia nzima ya maisha yake na ukaribu alionao kwa wananchi na pia jamaa zake.Huo ni ubinadamu halisi.

Pamoja na hayo,sifa za msingi zaidi zitakuja pale wananchi watakapofikiwa na maendeleo ya kweli na sio porojo za kisiasa.Huduma za jamii,uchumi na siasa safi ndio mambo ambayo yatampa sifa kamili.La sivyo itakuwa ni ile hadithi ya kale ya nabii asiyekubalika nyumbani.

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...