October 19, 2011

Je Mh Lowassa amekata kiu yako au ulitarajia nini zaidi?

Magazeti kadhaa leo yalikuwa na heading tofauti kuhusu mkutano wa Mh Edward Lowassa, Mbunge wa Monduli, wengi walidhani au kutarajia yale ya Igunga kutokea Monduli wakati Rostam Aziz alipoachia ngazi chamani kwa kile alichokiita siasa uchwara za CCM, wengine walitarajia ule msemo wa umemwaga mboga namwaga ugali, pia mambo ya Richmond/Dowans/Symbion nk. 

Sina hakika kuwa kile kilichosikika na kuripotiwa toka katika mkutano ule kimekata kiu yako au kuwa ndicho kilichotarajiwa na wengi, sina hakika, labda ndicho au sicho, kila mtu ana jibu lake. 

Buriani Maulid Hamad Maulid

Maulid Hamad Maulid


Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Maulid Hamad Maulid Wakati wa mazishi huko Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja jana leo.

Salha Izrael aelekea London


Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Izrael akipunga mkono wakati akiwa katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Oktoba 19,2011 alipokuwa akiondoka nchini kwenda London Uingereza kushiriki fainali za Miss World zitakazo fanyika mwezi ujao.

Hayati Samora Machel akumbukwa.

 Mama Maria Nyerere akiweka Shada la Maua ndani chumba maalum mahala lilipo kaburi la mwasisi wan chi ya Msumbiji wakati wa maadhimisho ya sherehe za kumbukumbu ya kifo cha mwasisi huyo zilizofanyika mjini Maputo leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Graca Machel, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo, mjini Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.

Mwezi wa 11 twaambia hakuna sababu kuondoa noti za "zamani"- BOT


Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema haujafika wakati wa kutangaza muda wa mwisho wa matumizi ya noti za zamani, kwa vile watu wanaozimiliki kwenye mzunguko bado ni wengi.
Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki na Mambo ya Sarafu wa BoT, Emmanuel Boaz, alisema hayo jijini Dar es Saalam jana alipozungumza na NIPASHE kwa niaba ya Gavana wa Benki hiyo, Profesa Benno Ndulu.

Alisema watautangazia umma utaratibu wa kurudisha noti hizo ili kuziharibu wakati zitakapobaki chache kwenye mzunguko.

Hata hivyo, hakuwa tayari kueleza kiasi cha noti hizo zilizoko mikononi mwa watu kwenye mzunguko kwa maelezo kwamba, suala hilo ni la ndani ya BoT.

“Tunajua hela yote iliyopo kwenye mzunguko na iliyopo Benki Kuu. Ikifika muda tutatangaza utaratibu wa kuzirudisha zikibaki chache bila kuwaletea wananchi usumbufu,” alisema Boaz.
Alisema baada ya kutoa noti mpya, hawakuona sababu ya kuutangazia umma kuwataka kurejesha zile za zamani kwa kuepuka msongamano wa watu, ambao ungejitokeza kwenye mabenki, hali ambayo ingewaletea wananchi usumbufu mkubwa.

Kutokana na hali hiyo, alisema noti hizo, ambazo ni za thamani ya Sh. 500, 1,000, 5,000 na 10,000, bado ni fedha halali kama walivyokwisha kutangaza huko nyuma, ambapo alisema hawakuwahi kutangaza muda wa mwisho wa kukoma matumizi yake.
source: Nipashe

Hivi sasa unaposema noti za zamani mtu anachanganyikiwa, maana zilizotolewa kabla ya hizi za Mwezi january ni mpya zaidi ya hizi zinazoitwa mpya, kwa msimammo huu Tanzania tutaendela kuwa na noti mbili mbili, lakini ambazo hazikai mifukoni mwetu, bila shaka haya ni maendeleo, na pengine ndiyo tunayoyataka. 


Mungu Ibariki Bongo Yetu.  

JK, LOWASSA MTEGONI1


DHANA ya kujivua gamba iliyoasisiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, na ambayo hivi karibuni ilimng’oa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, imeingia katika hatua ngumu ya utekelezaji wake, Tanzania Daima Jumatano, limebaini.


 Ugumu wa hatua ya sasa unatajwa na wafuatiliaji wa siasa za ndani za CCM kuwa unasababishwa na mwelekeo wa dhana hiyo kuonekana ukielekea kumlenga Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

 Kuibuka upya kwa siasa zenye mwelekeo wa uhasama mkali kati ya kundi moja la viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na Katibu wa Uenezi na Itikadi wa chama hicho, Nape Nnauye, kunaelezwa kuwa ni matokeo ya mwelekeo wa sasa wa dhana hiyo.

 Viongozi hao wa vijana wanaoongozwa na Kaimu Mwenyekiti wao wa Taifa, Benno Malisa, anayeungwa mkono na Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Arusha, James Millya, wanatajwa kuwa watu ambao wamekuwa wakipinga harakati zinazopigiwa chapuo na Nape za kuendelea kwa utekelezaji wa dhana hiyo ya kujivua gamba.

 Wakati Nape na wana CCM wengine wenye msimamo kama wake wakiitaja hatua ya Benno, Millya na vijana wenzao wa Arusha kuwa inayolenga kukwamisha utekelezaji wa dhana hiyo, kundi hilo linalompinga linamtuhumu kwa kukivuruga chama chao kwa maslahi yake binafsi.
 Sakata hili jipya liliibuka baada ya Benno kuliongoza kundi kubwa la vijana wa chama hicho kufanya maandamano katika jiji la Arusha hivi karibuni yaliyomalizika kwa kauli nzito kutoka kwao ambao mbali ya kuelekezwa kwa Nape zilimtuhumu pasipo kumtaja kwa jina mtoto mmoja wa kigogo kuwa alikuwa nyuma ya mpango wa kuwazuia kutekeleza ajenda yao.

 Hatua hiyo ya Benno ambayo baadhi ya wadadisi wa mambo wanaifananisha kuwa ni kubadili mwelekeo wa mapambano ya kisiasa inamweka mwanasiasa huyo kijana katika kundi la watu wanaopinga hatua zozote za kujaribu kumng’oa Lowassa katika uongozi wa chama hicho.

source Tanzania Daima. 

JE WATAMANI AU KUTARAJI KUSIKIA NINI TOKA KWA LOWASSA?


WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa leo anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari katika mkutano ambao utazungumzia mambo makuu matatu likiwamo suala la Kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambalo lilisababisha ajiuzulu wadhifa huo, Februari 2007. 

Mkutano huo wa Lowassa unafanyika siku moja tangu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James Millya atoe matamshi makali akiwatuhumu aliowaita watoto wa vigogo kwamba wanavuruga umoja huo huku akilalamika kwamba: “Maisha yake yapo hatarini.” 

Habari zilizopatikana jana kupitia kwa watu walio karibu na Lowassa zinasema, katika mkutano huo, Mbunge huyo wa Monduli (CCM), pia atazungumzia taarifa zinazomhusu ambazo zimekuwa zikichapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini.

  Suala jingine ambalo linatarajiwa kuzungumzwa na kiongozi huyo ni kuhusu mgogoro ndani ya CCM mkoani Arusha, ambao unatokana na mgawanyiko miongoni mwa makada na viongozi wa chama hicho.  “Pia anasema kwamba ataanzia pale alipoishia, siku ile alipozungumza bungeni kuhusu Serikali kufanya uamuzi mgumu lakini hakutakuwa na kumshambulia mtu,” alisema mmoja wa watu hao na kuongeza:

  “Anasema (Lowassa) kwamba lazima aweke kumbukumbu sahihi kwa baadhi ya mambo ambayo yametamkwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na viongozi wengine kwani amebaini kuwa uongo ukisemwa sana na kwa muda mrefu hugeuka kuwa ukweli.”

Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kuitisha mkutano wa vyombo vya habari tangu alipojiuzulu kuzungumzia sakata la Richmond ambalo halikuwahi kupata hitimisho la kisiasa wala kisheria.

Source: Mwananchi.

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...