October 3, 2011

IGUNGA UPDATES - CCM yatetea jimbo

Chama cha Mapinduzi kimeweza kutetea Jimbo la Igunga baada ya Msimamizi wa Uchaguzi jimboni humo kumtantaza mgombea wake kuwa mshindi kwa kura 26,484 dhidi ya kura 23 260  za mshindani wa karibu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. vyama ninane vilisimamisha wagombea tofauti na vyama viwili tu miezi 11 iliyopita.   • Jumla wa wapiga kura walioandikishwa ni 174, 077 
  • Wapiga kura waliojitokeza ni                        53,672
  • kura halali ni                                                    52,487, 

kuna tofauti kubwa sana ya waliopaswa kupiga kura na waliojitokeza kupiga kura, katika posti ya asubui nilisema kuwa kulingana na matokeo yalivyokuwa yakilipotiwa wapiga kura hawataweza kufikia nusu ya waliojiandikisha, hali halisi ndio hiyo watu zaidi ya 120, 405 hawakujikeza, hii ni takribani asilimia 70% KULIKONI?

Igunga hali tete!

Wakati matokea rasmi hayajatangazwa ama yakichelewa kutolewa hali imezidi kuwa tete wilayani Igunga, kwa muijibu wa radio one na clouds fm kumekuwa na vurugu za hapa na pale, watu kukamatwa ama kutawanywa, maduka na migahawa yote imefungwa kwa kuhofia hali hiyo wakati zoezi la kujumlisha kura likiendelea. 

Kuchelewa kutangazwa kwa matokeo kunelezwa kuwa kunachangiwa na kuchelewa kufika kwa masanduku ya kura kutoka baadhi ya vituo kulikosababishwa na miundombinu mibovu wilayani humo. 

IGUNGA UPDATES: Mshindi ni......

Mpaka jana usiku mchuano mkali ulikuwa kati ya CCM na CHADEMA huku CUF na vyama vingine vikifuatia kwa mbaali kwa mujibu wa matangazo yaliyokuwa yakirishwa moja kwa moja na ITV na Radio One. Mitandaoo mbalimbali imekuwa kitoa ubashiri wao ama matokeo yasiyo rasmi, wapo waliosema kuwa CCM imeshinda huku wengine wakisema CHADEMA imeshinda, CUF iliyokuwa ikidai kuwa ina mtaji wa kura zaidi ya 10,000 zinaonekana kuyeyuka, je ni nini kimeyeyusha kura zao miezi 11 tu baada ya uchaguzi ule?  bila shaka kuna somo hapo.Matokeo rasmi tunayatarajia muda wowote kwani watu wamekesha pale ofisi ya halmashauri ya Igunga kusubiri ujumlishaji wa matokeo toka kwenye vituo mbalimbali. 

Kwa mijubu wa Tume ya Uchaguzi watu waliojiandikisha na hivyo kuwa na sifa ya kupiga kura ni 174, 077 lakini kwa mujibu wa matokeo yanavyopokelewa na kuripotiwa kuna hati hati ya wapiga kura kufika ama kukaribia nusu ya wapiga kura wote halali, je hii inasababishwa na nini? kwanini watu zaidi ya nusu hawajajitokeza kupiga kura? je kuna walakini katika Daftari la Kudumu la wapiga kura? Itakumbukwa kuwa Uchaguzi mkuu uliopita ulikuwa na tatizo hili pia. 

Kila la kheri Kidato cha nne

Tanawatakia kila la kheri wanafunzi wa Sekondari wanaofanya mitihani kumaliza kidato cha nne kuanzia leo nchini kote, kumaliza kidato cha nne ni mwanzo tu wa safari ndefu ya masomo, hivyo hongezeni bidii katika mitihani yenu ili muweze kufaulu na hatimaye kuendelea na elimu ya juu zaidi. Special salamu kwa mwanangu Jacquile pale Madibila Secondary, jitahidi ili ufaulu mtihani huu kwa msingi mwema wa maisha yako ya baadaye. 

WINNERS Boulevard.

WINNERS Boulevard.: 'via Blog this'


Google+ Followers

There was an error in this gadget
There was an error in this gadget

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...