August 17, 2009
JK na hadithi ya Nabii kutokukubalika kwao
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali muasisi wa TANU na CCM Mzee Omar Selemani Mwenye umri wa miaka 104 aliyelazwa katika hospitali mkoa wa Dodoma. Mzee Omar Selemani ni mweyekiti wa Umoja wa wazee Mkoani Dodoma.Wakati wa harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika Hayati Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alikuwa akifikia nyumbani kwa Mzee Omari Selemani na kufanya shughuli za siasa
Naomba kwanza nikiri hapa kuwa si kawaida yangu kumwaga ngojera ktk Bongo pix bali taswira zaidi, lakini yapo ambayo wakutana nayo na uwezi kuyaweka ktk taswira ili watu wajionee hivyo wafanyaje? watoto wa mjini wanasema unakubali yaishe.
Hivi karibuni nilipata bahati ya kutoka nje ya nchi kidogo na kwenda Jo'burg kwa Mzee Madiba katika kuongeza ama kujinoa zaidi na taaluma yetu hii ambayo yabadilika kila uchao, yapo mengi niliyaona na kuyasikia katika juma zima nililokaa huko bondeni, mazuri na mabaya pia lakini moja wapo ya ambayo nilisikia mara kwa mara ni juu Rais wetu JK na vile jinsi ya wenzetu wamwonavyo.
Siku ya kwanza ya darasa letu tulianza kwa utambulisho kama ilivyo kawaida au ustaarabu kwa sehemu zote watu wakutanapo mara ya kwanza, niliposena kuwa natoka TZ nilipata macho mia mia toka kwa washiriki ka watatu hivi, mwanzo sikufahamu kwa nini ila nilikuja jua baadaye wakti wa breki, kulikuwa na washiriki toka Cameruni, Comoro, Afrika Kusini, Sao Tome and Principle, Tanzania na Zimbabwe, wakti wa mapumziko hayo walikuja kunisalim kwa karibu zaidi washiriki toka Comoro, Zimbambwe na Afrika Kusini, walikuja si kunisalimu tu na kutaka kujua zaidi habari za Bongo na zaidi Rais wetu JK, wote (sijui kama waliambiana) walimsifu kwa namna ya pekee JK na kuonyosha kumkubali kwa jinsi vile anavyoendesha nchi, na kuonyesha wazi kuwa wanatonea wivu sana kuwa na rais kama huyu.
Mi sikuwa na la kusema kwa sababu kwa akika si kitu nilikitarajia, na labda sidhani kama WATZ nao ndivyo wamwonavyo au la sijui kwani sijawai kufanya utafiti huo, lakini pia nilidhani labda ni kutokana na kauli ya Rais Obama aliyoitoa wakti wa kuanza ziara yake ya kwanza barani Afrika, sijui, lakini kila mmoja alikuwa na sababu yake tofauti kabisa na hilo, mfano Mzimbabwe ye alisema JK alikuwa ni Rais pekee aliyethubutu kumnyooshea kidole Mugabe ktk kikao cha wakuu wa SADC na kupelekea kutoa tamko lile lililosomwa na Waziri Membe ambalo limepelekea kuwa na serikali ya umoja, anasema japo hali ya kiuchumi haijatengemaa na kuwa wanalazimika kutumia pesa za kigeni hata kununua chungwa na kuwa Zimdollar yalipia Daladala tu lakini angalau kuna utulivu wa kisiasa ambao anazani una mchango mkubwa wa JK.
Mcomoro anamwona ni kiongozi shujaa hasa kwa kuthubutu kutuma majeshi kukomboa kisiwa cha Anjuani na kumwondosha Mtawala Mohamed Bacar mbali na juhudi nyingine za upatanishi wa kidiplomasia barani Afrika na zaidi mgogoro wa Kenya.
Msauzi anamwona ni kiongozi wa mfano barani Afrika, haya ni baadhi tu ya yale niliyoyasikia au kuyakumbuka angalau kwa sasa kwani kwa siku sita nilizokaa Jo'burg ni mengi yaliongelewa ni sifa nyingi zilimiinwa kiasi cha hata washiriki wengine ambao hawakumjua JK kufanya kazi ya ziada kwenye mitandao kusaka habari zake na TZ kwa ujumla.
Siku ya kuondoka nilipata bahati ya kukutana na baadhi ya wabongo wenzangu pale uwanjani na bila kuchelewa tulijikuta tuna chati haya na yale mmoja akitokea Harare na mwingine Jo'burg na sote tukirejea Dar, mara likaibuka ktk maongezi yetu hili la JK na jinsi anavyokubalika na zaidi Wazim wanavyomkubali, ikabidi kujiuliza kulikoni JK? na kwa hakika sidhani umaarufu huu au sifa hizi wampazo watu hawa je anazipata hapa nyumbani? au ndo nabaii uwa akubaliki kwao? Haya yamewapata manabii wengi Bwana Yesu akiwamo.
Je weye mdau wasemaje?
Zim nauli ya Daladala Bilion tatu
Zimdollar ni pesa ya kulipa ktk Daladala tu, uwezi nunulia chochote huko.
HARARE, Zimbabwe – A woman pays her bus fare with 3 trillion in old Zimbabwe dollars — the equivalent of 50 U.S. cents. The collector accepts the brick of neatly folded bundles of a trillion each without bothering to count the notes.
"No one seems to worry, and it works," said the woman, Lucy Denya, a Harare secretary who says she's seen police officers using old notes to board buses.
The Zimbabwe dollar is officially dead. It was killed off in hopes of curbing record world inflation of billions of percentage points, and Zimbabwe has replaced it with the U.S. dollar and the South African rand.
Yet the role of the old Zimdollar, as it is known, remains in flux. It is still used, and has become another point of contention for the divided leadership of the country, now one of the poorest in the world.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
LONDON (Dow Jones)--U.K. defense giant BAE Systems PLC (BA.LN) Tuesday was fined GBP500,000 for improper accounting in relation to the award...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
It’s not important to hold all the good cards in life. It`s important how well you play the cards which you hold. Often, when we lose...
-
The Himba are an ethnic group of about 20,000 to 50,000 people living in northern Namibia, in the Kunene region (formerly K...
-
On Tuesday, 7th July we witnessed the peak of the Saba Saba festivities. I never go to the Dar es Salaam International Trade Fair, these day...
-
A very rare opportunity. With Outstanding Entrepreneur, Great Visionary, Motivational Speaker, Founder, Chairman and CEO of Edmark Inte...
-
Huwa nina kawaida au tabia ya kusoma kila kilichombele yangu kilichoandikwa, sijui kama kawaida/tabia hii ni mzuri au la kila mtu aweza sem...