August 14, 2009

Fidia ya mabomu ni balaa tupu.

MAANDALIZI ya kuwalipa fidia wakazi wa Mbagala walioathiriwa na mabomu yameingia dosari baada ya baadhi ya majina ya watu kukosekana kwenye orodha ya malipo, huku majina mengine yakitofautiana na namba za nyumba zilizoathiriwa.
Jumla ya Sh8.5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wakazi ambao nyumba zao ziliathiriwa na milipuko ya mabomu iliyotokea Aprili 29 kwenye ghala la silaha la kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) iliyo Mbagala na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 29. Fedha hizo zitatumika kulipa fidia nyumba 9,259 zilizoharibiwa na mabomu hayo na ambazo zilihakikiwa na serikali.
Lakini uchunguzi wa gazeti hili jana umebaini kuwa mchakato wa malipo hayo umeanza kuingia dosari baada ya watu kadhaa waliofika ofisi ya afisa mtendaji kata ya Mbagala Kuu, kugundua kuwa majina yao hayapo kwenye orodha iliyobandikwa ukutani na wengine kukuta tofauti ya majina na namba za nyumba.
Afisa mtendaji wa kata hiyo, Basil David alisema kuwa zaidi ya watu 50 waliofika ofisini kwake kuangalia majina yao, walikuta aidha yamekosewa au hayaendani na namba za nyumba zao. "Ni kweli zimejitokeza kasoro kwenye mchakato huu. Zipo namba za nyumba zilizokosewa na majina mengine yanatofautiana na namba za nyumba hizo,” alisema.
"Kutokana na hali hii tumeziagiza ofisi za serikali za mitaa kuorodhesha majina ya watu ambao majina yao au namba zao zimekosewa, ili ayapeleke kwa mkuu wa mkoa kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho kabla ya kuandaliwa kwa hundi za malipo," alisema.

Katoliki- Kingunge amepwelea,

MALUIMBANO kuhusu waraka wa Kanisa Katoliki (RC) yanaendelea kuwa makali, baada ya waumini wa kanisa hilo kumuelezea mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru kuwa amepwelea. Mbali na kauli hiyo iliyotolewa jana na Baraza la Walei, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Valentino Mokiwa amemtaka Kingunge kuliomba radhi kanisa badala ya kuombwa radhi kama alivyotaka. Matamko hayo mazito yalitolewa kwa nyakati tofauti jana wakati wahusika hao walipokuwa wakizungumza na gazeti hili kuhusu utashi wa Kingunge kuwa Kanisa Katoliki limuombe radhi na kuungama kutokana na kumwita kuwa ni mkongwe. Mwenyekiti wa Baraza la Walei, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Balozi Nicholas Kuhanga alisema baraza limewataka maaskofu wa kanisa hilo, kutoendelea kujibishana na Kingunge badala yake kazi hiyo sasa itafanywa na baraza hilo. Kuhanga, ambaye amewahi kuwa waziri, alisema wamefikia uamuzi huo kwa kuwa baraza linamjua kwa undani mwanasiasa huyo kwa kuwa wanaishi naye.
Balozi Kuhanga alisema anamshangaa Kingunge kuupinga waraka huo wakati unawasisitizia wananchi kuwachagua viongozi waadilifu na wanaojali maslahi ya wananchi. Alisema kanisa haliwezi kumwomba radhi Kingunge kwa kuwa hana tofauti na mafisadi kutokana na kitendo chake cha kupinga waraka unaowapinga mafisadi.
"Yeye anaingia katika kundi hilo, (Mafisadi) kutokana na msimamo wake wa kuupinga waraka huo unaopinga ufisadi nchini," alisema Kuhanga. "Wale ambao hawana hulka za kifisadi wanaunga mkono waraka wakati wale ambao wana hulka za kifisadi wanaupinga, kwa sababu unatishia maslahi yao." Alifafanua kuwa waraka huo umetolewa kama somo la uraia ambalo limeonekana kufifia na kusababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii.
source: Mwananchi

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...