November 22, 2011

TAQWA ACCIDENT UPDATES: Picha za wanafunzi 6 wa UDSM waliofariki

Kassim Dadi - Tanzania

Josephine Kaleso  - Malawi 

Nshaija Muganyizi - Tanzania

Mubiru Patrick  - Uganda

Chimuka Hamajata  - Zambia

Chikondi Chasowa - Malawi

WANAFUNZI sita waliokuwa wakisoma Shahada ya Uzamili, Hisabati katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni miongoni mwa watu 18 waliokufa Jumamosi katika ajali ya basi la Taqwa lililogongana na lori mkoani Kagera.

 Kwa mujibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, marehemu hao ni miongoni mwa wanafunzi 10 wa UDSM waliokuwa wakienda Kigali nchini Rwanda kwa ajili ya ziara ya kimasomo katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Kigali.

 Kwa mujibu wa taarifa ya Profesa Mukandala kwa vyombo vya habari, wanafunzi waliokuwa katika safari hiyo ni wa kimataifa waliokuwa wakisoma shahada ya uzamili kupitia Programu ya Hisabati katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki.
 Miongoni mwa waliokufa katika ajali hiyo, wawili ni raia wa Malawi, Watanzania wawili, Mganda na Mzambia.
 Watanzania waliokufa ni Nshaija Muganyizi, na Kassim Dadi, Wamalawi ni Chikondi Chasowa na Josephine Kaleso, Mganda ni Mubiru Patrick na Mzambia ni Chimuka Hamajata.
 

 Basi la Taqwa lenye namba za usajili T 635 ABC aina ya Nissan Diesel lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Bujumbura Burundi liligongana na lori la Kampuni ya Bakhresa lenye namba za usajili RAB 255ACT lililokuwa likitoka Ngara kwenda Dar es Salaam.

 Magari hayo yaligongana Jumamosi saa nne asubuhi katika eneo la Lusahunga wilayani Biharamulo.

Tutarajie nini toka WHITE HOUSE Dodoma?????

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete wa pili kutoka kushoto akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo Novemba 21, 2-011 ukumbi wa 'White House' wa makao makuu ya chama hicho tawala mjini Dodoma. kulia katika picha na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama na kutoka kushoto ni Rais Mstaafu William Benjamin Mkapa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Zanziba Aman Abeid Karume

Vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi, CC na NEC vinaendelea mjini Dodoma china ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, ambapo wengi wanatarajia uenda maaumuzi magumu na hasa ya kujivua gamba ama kuvuliwa Gamba yatatolewa.



Wakati akihahirisha NEC mwezi wa Aprili mwaka huu Rais Jakaya kikwete aliongea na vyombo vya habari na kunukuliwa akitoa kauli hii 

" Tumekubaliana hatua zetu mbili, ya kwanza kuwabana wa..wa.. waji..wawaamue kuwajibika, lakini wanapokataa tusicheleee kuwawajibisha" JK.


Haikuleza ni kina nani na wanapaswa kuwajibikaje, tusubiri tuone labda sasa tutawajua hao WANAOPASWA KUWAJIBIKA/KUWAJIBISHWA. 

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...