January 22, 2008

Mikukus.. wale wapenzi wa kujichana na hasa makuku sasa watayapata ktk muonekano bora zaidi toka Interchick. Mwenyekiti wa bodi wa Interchick Kalokola Bwesha na naibu waziri wa mifugo Dr Mlingwa wakipata vikorombwezo vya vyuku toka Interchick wengi na hasa wakazi wa maeneo ya mbezi beach, kunduchi, tegeta na vitongoji kadhaa vya dar bado wakumbuka yale makuku ya wakti uleeeeeeeee sasa yamekuja tenaaaa.
KP Leo KP ni Msanii hasa, kazi zako nazikubali kaka, mi sijui weye unawaza nini hasa kwanza hata kutaka kujua bwa mkubwa kipara awazani.

Mi nalia jamani, naililia Tanzania

mafisadi waitia shakani, hatuna pakukimbilia.

BODI RUUM.. Mambo ya kushangaa ni mengi sana bongo na hasa hapo PAITWAPO BOT uwezi amini kuwa pamoja na minara yote hii miwili na jengo la kati lakini bodi room ni kiduchu kiasi kupita mpaka msuguane migongo!!! hivi hilo jengo lote ambalo naamini kuwa ni kubwa kuliko pengine jengo lolote bongo isipokuwa labda bunge ni la kazi gani hasa? au hata wafagizi wana ofisi zilinganazo na flooor nzima?
JK ndani ya BK. 1.Wazee wa mji wa Bukoba wakimpa zawadi za jadi Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Uhuru mjini humo jana.baadaye Rais Kikwete alihutubia mkutano wa hadhara. 2.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga ngoma ya mtawala wa jadi aliyokabidhiwa na wazee wa mji wa Bukoba juzi katika viwanja vya Uhuru mjini hapo. 3.Umati wa mamia wa wakazi wa mji wa Bukoba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiwahutubia juzi. 4.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mzee Paulo Kilaini mwenye umri wa miaka 80 katika kijiji cha Katoma nje kidogo ya mji wa Bukoba juzi.Mzee Paulo Kilanini ni Baba Mzazi wa Askofu Msaidizi Jimbo kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Method Kilaini.Rais Kikwete alikwenda kijijini hapo kukagua maendeleo ya Shule ya msingi Kilaini iliypjengwa na Askofu huyo katika kiwanja alichokitoa Babu yake. Kwa wale msofahamu mila za BK VAZI la kanzu na koti ni vazi la heshima kwa Wazee wa mkoa huu na mara kijana anapooa upewa upewa kanzu, mkuki na mundu hii kutambua kwamba kijana sasa kawa mtu mzima na anaweza kuongea na kukaa na wazee wa kijiji na kutoa mchango wake, kama ujaoa hata kama utakuwa na miaka mia we ni mtoto tu huwezi ongea mbele za wazee.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...