October 28, 2009

Mchakamchaka, mazingaombwe yangalipo shuleni siku hizi??

"Jua lilee literemke mamaaa, mwezi naoo utelemkee mamaaa haiyahiyaa hiyaa hiyaaa mamaaaa.............." Je wakumbuka nyimbo gani za mchakamchaka za enzi zile? au ni nini wakumbuka katika miaka ya sabini na themanini shule za msingi na sekondari? Wakti ule tulikuwa ukifika shule tu mwakimbia mchakamchaka na kuimba nyimbo kibao hivi bado yafanyika hayo?? Nakumbuka wakti tuko Sekondari Jite Best kulikuwa na mwalimu mmoja anaitwa GB alikuwa anakuja saa kumi na nusu na kugonga kengere na kiboko mkononi, ole wako ubakie bwenini ujifanye ujasikia, hizo bakora zake ni balaa, hivi vingalipo hivi?? Mazingaombwe mwayakumbuka??? wale wakongo walikuwa wanajifanya wanatengeneza pesa, vitambaa, kalamu, NK na ilikuwa unalipa kiingilio na mwatangaziwa shule nzima siku hiyo HAKUNA MASOMA, hivi waliishiaga wapi wale?? Mdau ni kitu gani wakumbuka???

Hongera Tamila & Sarah

Bwana Harusi Emmanuel Makene Tamila na Bi Harusi Sarah Mgaya wakipozi mara baadaya kufunga pingu za maisha Jumamosi iliyopita. Tamila ni Mwanasheria Kitaaluma na Mmiliki wa Kampuni ya Sheria ya Kings Law Chembers na Pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, mwenyeji wa Mwanza na Bi Harusi Sara ni Mwanafunzi wa Udaktari wa Madawa katika Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki na mwenyeji wa Ludewa Iringa.

Wabongo wanakimbia ARV?????

TANZANIA: Low uptake of ARVs hampering universal access
HIV-positive Tanzanians are not taking advantage of the availability of life-prolonging anti-retroviral medication in hospitals around the country, says a senior government official. "We have an adequate supply of ARVs in our hospitals and other outlets, but there are few people who are turning out for this important service," David Mwakyusa, Health and Social Welfare Minister, told IRIN/PlusNews. An estimated 250,000 people are taking ARVs, while another 190,000 who need them are not accessing them. In 2008, the government re-affirmed its commitment to achieving universal access to ARVs by 2010. "We are working hard to encourage people to check their HIV status and those infected to go for further medical attention and when necessary start taking ARVs, which are in good supply," the minister said. Mwakyusa also bemoaned the fact that few pregnant women made use of prevention of mother-to-child transmission (PMTCT) services available at antenatal clinics; just 33 percent of pregnant women who require PMTCT services access them, according to UNAIDS. Research has found that although HIV-positive Tanzanians welcome anti-retroviral therapy, transportation, supplementary food costs, ill-treatment at hospitals and difficulties in sustaining long-term treatment all act as barriers to accessing treatment. Fear of stigma as well as HIV denial, which often led patients to seek treatment from alternative healers, and inadequate numbers of trained medical personnel, also prevented patients from accessing healthcare. "Multi-faceted interventions are required to promote regular HIV clinic attendance, including ongoing education, counselling and support in both clinic and community settings," authors of a recent study by the Centre for Population Studies and the London School of Hygiene and Tropical Medicine recommended. Mwakyusa noted that Tanzania was planning to cut the cost of ARVs by producing them locally. He said it was important for the country to become more self-sufficient, especially in the face of the global economic downturn. "We are praying that despite the global financial crisis, donors will continue supporting our efforts," he said. "The financial crisis is clearly affecting the capacity of donors to fund international programmes on AIDS." icheki hapa

October 26, 2009

Tanzaniaaa, Tanzaniaaaaaa nakupenda kwa ...........

SIKIA SHUHUDA ZA WALIOTEMBELEA BONGO JINSI WANAVYOISIFU!
This has been an amazing trip for us. We've met incredible people and the kids have had the experience of a lifetime. I hope they remember this for the rest of their lives. How could they not, right?
Two years ago I could not have imagined a trip like this would be possible. When a friend asked me what a dream-come-true would look like for me, I had to say it had something to do with taking my children to faraway lands for experiences that would change them forever. Since that time, my life has realigned to make this dream and many more possible. All because one friend asked.
What are you dreaming for for your kids?

TFF, WIZARA YA HAB.... MICHEZO MPO?

"The current indoor stadium is in an advanced state of disrepair, reflecting the inability of Tanzania to maintain a sports infrastructure on its own"

October 23, 2009

WAPIGA KURA HEWA MAMILIONI UGANDA WAGUNDULIKA

Having examined all general election results from the Movement system to present day (1996-2006), we have found un-refuted indications of rigging in all three elections. The group also found among others;
The “Buzaaya County” effect of 1996 where polling stations were counted twice by Electoral Commission. The persistence of “Buzaaya” especially in Kampala needs to be addressed. Subsequently, we have downgraded the Presidential candidate score of Mr Yoweri Museveni from 4.4 million to 4.3 million to reflect the right score. After adjustment, Yoweri K. Museveni scored 75 per cent in 1996. The “Ayivu effect” 2006 where the NRM failed to prevent internal rigging in NRM elections and caused the NRM Presidential candidate to lose a former NRM stronghold (protest vote for opposition).
The “Mushanje effect” – Rubanda County West, Kabale 2006, where the NRM (Museveni) candidate’s victory declared at the polling station was altered and recorded as a Besigye victory at National Electoral Commission. This was done by the presiding officer who probably signed a new declaration sheet after polling. We have no way of authenticating signatures or a citizens’ register from which to compare and cross match.
Conclusions
NRM must unreservedly lead the way to remove all “ghosts” as they are more likely to damage the party in 2011 and will work into FDC plan to bring the NRM candidate below 50 per cent as we shall demonstrate.
Whereas external forces compromise the election results, this report shows that internal non-adherence to the party laws and selective application thereof also undermines the Party’s performance probably to a greater extent.
In order for NRM to succeed in 2011, the Party leadership must ensure internal cohesion and discipline, and adherence to the party constitution. This must apply across the organisation from top Party Leadership to the Branch executive.
We therefore advocate for all NRM to lead by example in ensuring discipline and adherence to the Party laws. This will ultimately ensure 80 Per cent victory for NRM Presidential candidate and all other candidates competing at various levels. We also recommend an early strategic plan from top leadership.

Kiwira kurejeshwa, je ni mwanzo au mwisho wa picha????

HATIMAYE serikali imetangaza rasmi kuwa imeanza kumiliki mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira baada ya kuitaifisha kutoka kwa wamiliki wake.
Hatua hiyo ilitangazwa jana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, katika ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam, wakati alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa lengo la kutoa taarifa ya serikali kwa kamati hiyo jinsi ilivyoshughulikia suala la Kiwira baada ya kuahidi kulifanyia kazi wakati wa mkutano wa 16 wa Bunge mjini Dodoma. “Kimsingi serikali imeshauchukua mgodi huo na inaumiliki kama tulivyoliahidi Bunge, kuanzia sasa ni mali ya serikali na hakuna mtu mwenye mkono pale,” alisema Waziri Ngeleja.
Alisema baada ya kuuchukua mgodi huo, hatua ambayo inafuata ni kuwalipa wafanyakazi wake ambao walikuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu bila kulipwa kutokana na waliokuwa wamiliki kusimamisha uzalishaji.
“Tunawataka wafanyakazi wote wa Kiwira watuelewe kuwa tunaanza kuwalipa kuanzia wiki hii. Kabla ya Novemba mosi, mwaka huu, wanatakiwa wawe wamelipwa fedha zao zote za malimbikizo,” alisema Waziri Ngeleja.
Alisema fedha zitakazolipwa kwa wafanyakazi hao ni mishahara ya miezi 15, ambayo ilikuwa haijalipwa kwa kipindi chote ambacho mgodi huo ulisimama.
Alipotakiwa kueleza kama waliokuwa wamiliki wa mgodi huo, wameshalipwa na wamelipwa kiasi, Waziri Yona alisema hilo litafahamika zaidi mjini Dodoma wakati atakapowasilisha ripoti yake katika mkutano wa 17 wa Bunge unaotarajiwa kuanza Oktoba 27.
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shellukindo, alisema wamepokea taarifa ya serikali kuhusu mgodi wa Kiwira na wataiwasilisha bungeni.
“Sisi tumewasikiliza serikali na tutakwenda kuwasilisha bungeni, mengi tutakwenda kusema huko,” alisema Shellukindo bila kufafanua zaidi.
Pia alisema kamati hiyo imefurahishwa na uamuzi wa serikali kuumiliki rasmi mgodi wa Kiwira na kuamua kuwalipa wafanyakazi malimbikizo ya mishahara yao ambayo imekuwa ikilalamikiwa kila mara.
Kamati hiyo ilisisitiza kuwa, suala la Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Daniel Yona kulipwa au kutokulipwa na wamelipwa kiasi gani, litajulikana mjini Dodoma. Hata hivyo, Shellukindo jana aliendelea kugoma kujibu maswali mengi kutoka kwa wanahabari kwa madai kuwa maelezo yaliyotolewa yanatosha.
Azma ya serikali kutaka kurejesha mgodi wa Kiwira mikononi mwake, mara ya kwanza ilitangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa mkutano wa 16 wa Bunge. Alisema serikali itachukua hisa zote za Kiwira ili kuondoa lawama zinazomkabili kiongozi huyo wa serikali ya awamu ya tatu.
“Mimi nilichoamua... kama issue ya Kiwira ndiyo kitu kikubwa, nitahakikisha zile hisa zote zinarudi serikalini.
“Nitachukua zote, nitazirudisha serikalini tuanze upya ili tuone kuwa hiki tulichoanza nacho, pengine kitatupa tija tunayohitaji,” alisema Waziri Pinda wakati akifanya majumuisho ya hotuba ya bajeti ya ofisi yake.
Inadaiwa kuwa, familia ya Mkapa na Yona, zilitakiwa kununua mgodi huo kwa sh milioni 700, lakini walikubaliwa wakati wa kusaini mkataba walipe Sh milioni 70 na zilizosalia zilipwe katika kipindi cha miezi sita. Hata hivyo, fedha hizo hazikulipwa.
Makampuni mengine ambayo kwa pamoja yaliungana na kununua mgodi huo ni Choice Industries, ambayo wamiliki wake ni Joe Mbuna na Goodyeer Francis na Universal Technologies, ambayo inamilikiwa na Willfred Malekia na Evance Mapundi. Wabia hawa ndio waliounda Kampuni ya Tanpower Resources Ltd inayomiliki mgodi huo.
Mgodi huo umejengwa na Serikali ya China na kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania kabla ya kuuzwa kwa wawekezaji wapya Kampuni ya Tanpower, Machi 2007.
source: Tanzania Daima

October 22, 2009

Dr Shein @ NIMR

Daktari wa Utafiti wa magonjwa ya Binaadamu katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binaadamu NIMR Dk. Ester Ngadaya (kushoto) akimueleza Makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Shein juu ya kazi mbalimbali za utafiti wanazozifanya katika Taasisi hiyo, wakati Makamu wa Rais alipotembelea kwenye Ofisi za Tasisi hizo zilizopo Mtaa wa Luthuli Dar es salaam leo. Wa pili kushoto Naibu Waziri wa Afya Dk. Aisha O. Kigoda, kushoto Kaimu Meneja Mkuu wa Taasisi hiyo Dk. Mwele Malechela.

October 8, 2009

MADAKTARI WA JK WATOA TAARIFA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Mimi naitwa Dk. Peter Mfisi, ni mmoja wa madaktari wa Mhe. Rais. Nipo Ikulu. Nimekuwa na Mhe. Rais tangu wakati wa kampeni mwaka 2005 mpaka sasa. Mwenzangu ni Dk. Mohamedi Janabi ambaye ni daktari bingwa wa maradhi ya moyo katika Hospitali Kuu ya Taifa Muhimbili. Nimewaiteni waandishi wa habari kufafanua masuala muhimu kuhusu afya ya Mhe. Rais kufuatia tukio la Jumapili iliyopita, Oktoba 4, 2009, pale Mwanza. Tukio hilo limeleta mshtuko kwa watu wengi na kuendelea kuwa jambo linalozua mjadala kuhusu hali ya afya ya Mhe. Rais. Naelewa sababu ya wananchi kuwa na hofu na kuwapo kwa mjadala miongoni mwao. Rais ndiyo kiongozi wetu mkuu katika taifa na hivyo kuwa mwenye afya njema ndiyo matakwa ya kila mwananchi.
Naelewa fika kuwa kutokana na kiapo changu cha udaktari na maadili yangu ya kazi siruhusiwi kutoa hadharani undani wa habari yoyote inayohusu mgonjwa ninayemtibu bila ridhaa yake. Hata hivyo, kwa kuwa huyo ni Rais wa nchi, na suala la afya yake ni kwa maslahi ya taifa na umma wa Watanzania kwa jumla, na kwa kuwa yeye ameridhia kutolewa kwa habari za afya yake ili watu wajue ukweli na kuondoa hofu, nimeamua kufanya hivyo. Kama sote tujuavyo, Jumapili iliyopita, Oktoba 4, 2009 mwaka huu, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa anashiriki katika sherehe za miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, aliishiwa nguvu na kulazimika kwenda kwenye chumba cha mapumziko. Baada ya mapumziko ya dakika 10 hivi, Mhe. Rais alirejea kwenye shughuli hiyo na kuendelea kushirikiana na waumini wa AICT hadi mwisho wa ratiba yake. Ninapenda kusisitiza kuwa tukio la Mwanza limetokana na Mhe. Rais kuzidiwa na uchovu, na wala siyo kwa sababu nyingine yoyote ya kiafya. Wakati tukio hilo linatokea nilikuwepo, nilichukua vipimo muhimu kama daktari anavyotakiwa kufanya linapotokea tukio kama lile kwa mtu. Vipimo vyote vilithibitisha kuwa Mhe. Rais hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya ambayo yangeweza kuhusishwa kuwa chanzo cha tukio lile. Pressure yake ilikuwa 130/85mmhg ambayo ni kiwango cha kawaida kwa mtu wa umri wake. Mapigo ya moyo wake yalikuwa 76 kwa dakika ambayo pia ni ya kawaida. Sukari kwenye damu ilikuwa 5.5mmol/l ambayo nayo ilikuwa ya kiwango cha kawaida. Joto la mwili lilikuwa digrii 37.5 centigrade ambalo ni la kawaida. Mhe. Rais pia hakuwa na kiungo chochote kilichoonekana kutetereka, jambo ambalo lilithibitisha kuwa hakupata kiharusi. Kutokana na matokeo hayo, sikuona hatari yoyote ya yeye kuendelea kushiriki katika sherehe hiyo muhimu kwa wakati huo. Ndiyo maana niliruhusu aendelee kushiriki sherehe zile mpaka alipomaliza na kuondoka. Baada ya kurudi Dar es Salaam siku ile niliwasiliana na madaktari wanzangu wa hapa nchini na nje ya nchi ambao tumekuwa tunashirikiana nao katika kuchunguza na kufuatilia afya ya Mhe. Rais. Wote hao baada ya kuwasimulia kilichotokea na matokeo ya vipimo nilivyomfanyia Mhe. Rais, kwa tafakuri zao hawakuwa na wasiwasi wowote kuwa tukio hilo lilisababishwa na jambo jingine lolote, isipokuwa uchovu. Imani yao inatokana na ukweli kuwa wanaifahamu vizuri hali ya afya ya Mhe. Rais kwa kuwa wanahusika katika kuifuatilia mara kwa mara. Mmoja wao alimuona Mhe. Rais siku moja kabla ya kuondoka New York ambapo alipata nafasi ya kuchunguza afya yake. Mimi na mwenzangu Dk. Mohammed Janabi, ndiyo wenye dhamana ya kuiangalia afya ya Mhe. Rais Kikwete kila siku. Tumekuwa tunafanya hivyo kwa zamu na wakati mwingine kwa pamoja, inapobidi kufanya hivyo. Katika kufuatilia hali ya afya ya Mhe. Rais tumekuwa pia tukimfanyia uchunguzi wa afya yake kwa vipindi maalum hapa nchini na nje ya nchi kwa vipimo ambavyo hapa nchini havipo. Napenda kuwahakikishia wananchi wenzagu kuwa katika miaka hii minne Mhe. Rais wetu amefanyiwa uchunguzi wa kina wa afya yake. Nadiriki kusema kuwa hakuna kipimo ambacho hatujapata kukifanya katika uchunguzi wa mambo muhimu ya afya yake. Kwa sababu ya kuwatoa hofu wananchi na kwa vile mwenyewe anaridhia tufanye hivyo napenda kuwapa ufafanuzi kuhusu hali ya afya ya Mhe. Rais. Katika hali ya kawaida nisingefanya hivyo kwa sababu maadili ya kazi ya udaktari yanakataza. Naamini madaktari wenzangu wataelewa mazingira niliyokuwa nayo. Katika kufuatilia afya ya rais tumekuwa tunaangalia na kuchunguza mambo yafuatayo. (a) Blood Pressure: Tunafuatilia kwa karibu sana hali ya nguvu ya msukumo wa damu (blood pressure). Tunampima mara kwa mara na mwenyewe tumempa mashine ya kujipima kila siku na anafanya hivyo. Kwa jumla pressure yake iko kwenye viwango vya kawaida. Aidha, uzito wake wa mwili unaendena ipasavyo na urefu wake. Mhe. Rais ni mtu mwenye mazoea ya kufanya mazoezi na yuko makini katika chakula anachokula. Sisi tunahusika kwa ukamilifu na kuelekeza kuhusu chakula anachokula. Hatuna matatuzi na Mhe. Rais kwa jambo hilo. Ana nidhamu ya kujipima pamoja na mazoezi na chakula. (b) Moyo: Tumekuwa tunafuatilia kwa karibu hali ya afya ya moyo wake. Tumemfanyia vipimo kama vya ECHO, ECG na vinginevyo, na hatujabaini kuwepo tatizo lolote. (c) Ubongo: Mwaka uliopita, 2008, Mhe. Rais tulimfanyia uchunguzi wa afya ya ubongo wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hapa Dar es Salaam. Tulitumia kipimo cha CT – Scan na matokeo yameonyesha kuwa hana matatizo. (d) Ini, Figo, Bandama, Kongosho: Mhe. Rais Kikwete kila mwaka tunapomfanyia uchunguzi wa jumla wa afya yake tumekuwa tunamfanyia kuchunguza viungo vyake muhimu vya tumboni kama vile ini, figo, bandama na kongosho. Tumekuwa tunafanya hivyo kwa kutumia kipimo cha ultra sound na kwa kupima damu yake kwa kutumia vipimo muhimu. Uchunguzi huo umebaini kuwa viungo vyote hivyo ni salama na vinafanya kazi vizuri. (e) Mfumo wa njia ya Chakula: Mfumo mzima wa njia ya chakula (alimentary canal), yaani koromeo la chakula, tumbo, utumbo mdogo na utumbo mkubwa nao tumeufanyia uchunguzi wa kina kama kuna tatizo lolote katika kipindi cha miaka miwili hii. Mwaka 2007, tulimfanyia kipimo cha colonoscopy mjini Paris, Ufaransa, kuchunguza hali ya afya ya utumbo mkubwa. Matokeo ya uchunguzi yalionyesha kuwa utumbo wake mpana uko salama kabisa na hakuna matatizo yeyote. Daktari bingwa aliyemfanyia uchunguzi huo ameshauri kuwa Mhe. Rais hahitaji kufanya kipimo hicho tena mpaka baada ya miaka saba. Nakumbuka pia daktari huyo alimtania Mhe. Rais kuwa angefurahi kuazima utumbo wake. Wiki mbili zilizopita, Mhe. Rais akiwa mjini New York, Marekani, alifanyiwa kipimo cha endoscopy kuchunguza kuanzia koromeo la chakula, tumbo, na utumbo mdogo. Matokeo ya uchunguzi huo yametoa majibu mazuri kuwa yako salama. Makusudio ya kufanya vipimo hivi viwili ni kuchunguza maradhi ya kansa na viashiria vya ugonjwa huo. Bahati nzuri hana maradhi hayo na wala hakuna dalili yoyote iliyoonyesha kuwapo viashiria vya kansa. (f) Tezi la Shingo (Thyroid Glands): Aidha, wakati wa safari yake hivi karibuni majuzi mjini New York, Marekani, Mhe. Rais tulimfanyia uchunguzi wa afya ya tezi la shingo pamoja na kiwango chake cha utoaji wa homoni. Matokeo ya vipimo vyote vilivyofanyika yameonyesha kuwa hakuna matatizo yoyote. (g) Tezi la Kibofu (Prostate): Septemba, mwaka huu, 2009, tulifanya uchunguzi wa hali ya afya ya tezi la kibofu (prostate) kwa kutumia mashine maalum na kwa kuchunguza damu yake. Vipimo vyote hivyo vimeonyesha hali si mbaya. Tezi lake lina ukubwa wa kawaida na hata vipimo vya viashiria vya kansa ya tezi hilo (PSA) tunavyofanya kwenye damu vilikuwa katika kiwango cha kawaida. Mhe. Rais hana matatizo ya prostate. (h) Macho, Masikio na Pua: Tumeshamfanyia vipimo vya macho, masikio na pua na vyote viko salama. Mhe. Rais anavaa mawani lakini hayo si maradhi. Watu wengi baada ya kufikia umri wa miaka 40 si ajabu huhitaji mawani. Tunapofanya uchunguzi wa macho, ukiacha ile ya kuchunguza uwezo wa kuona, tunaangalia pressure ya macho na hali ya viungo vya nje na ndani ya jicho. Mhe. Rais hana matatizo yoyote. (i) Damu: Tumekuwa tunamfanyia Mhe. Rais uchunguzi wa damu yake kwa vipimo mbalimbali vinavyotumika kutambua maradhi mbalimbali yahusuyo damu yenyewe na mwili mzima wa mwanadamu. Tumekuwa tunafanya hivyo kila baada ya miezi sita au panapojitokeza ulazima wa kufanya hivyo. Tumekuwa tunafanya hivyo hapa nchini na hata nchi za nje kwa nia ya kulinganisha matokeo yetu na kwa vipimo ambavyo sisi hatunavyo. Matokeo ya uchunguzi wetu yameonyesha kuwa Mhe. Rais yuko salama. Hana maradhi ya damu au kisukari, wala ukimwi, au ya wingi wa mafuta (cholesterol), ama ya kiwango cha madini, au ya tezi la kibofu, wala ya tezi la shingo, au ya ini, au ya homoni mbalimbali zilizoko mwilini na mengine n.k. Jambo pekee linalojitokeza ni kwamba Mhe. Rais ana damu nyingi. Hivyo, tumekuwa tunamshauri kupunguza damu kwa kuchangia Benki ya Damu. Tunashukuru amekuwa anafanya hivyo karibu kila baada ya miezi sita. Damu nyingi inaweza kuwa na madhara mwilini lakini Mhe. Rais hajafikia kiwango cha kuwa ni tatizo la kiafya. Pia tunamshukuru kwa kuwa mwepesi kukubali kupunguza damu ambayo tunaitumia kuokoa maisha ya watu wengine. Hakuna hofu yoyote. Napenda kusema wazi watu wote wasikie na kwa ukweli kwamba mimi na daktari mwenzangu yaani Dr. Mohamed Janabi hali ya afya ya Rais silo jambo linalotutia shaka wala kutusumbua au kutunyima usingizi. Tatizo pekee ambalo limekuwa likimsumbua Mhe. Rais mara kwa mara ni maumivu ya shingo yanayotokana na kuumia zamani utotoni na wakati wa ujana. Kuumia huko ni kwa baadhi ya pingili za uti wa mgongo, sehemu ya shingo (cervical spine), kuathirika na kumsababishia maumivu. Mara nyingi matatizo ya namna hiyo huwapata wanamichezo na wanajeshi. Kutokana na shughuli wazifanyazo. Kuumia siyo jambo la kustaajabisha. Tutakumbuka kuwa Mhe. Rais amekuwa mwana michezo hususan mchezaji wa basketball, mpira wa miguu na hata riadha wakati wa ujana wake. Pia alikuwa mwanajeshi. Ili kutambua vizuri tatizo la shingo ili tujue namna ya kumpatia tiba tumeshamfanyia vipimo vyote muhimu vya uti wa mgongo toka juu mpaka chini. Tumetumia x-ray, CT – Scan na MRI-Scan. Pia ameshaonwa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu hapa nchini na nje. Pamoja na kuwepo athari katika shingo, madaktari hao kwa dhati wameshauri kuwa kwa sasa maumivu yake hayahitaji upasuaji isipokuwa mazoezi ya viungo. Mhe. Rais amefundishwa mazoezi anayotakiwa kuyafanya na amekuwa anayafanya kwa nidhamu ya hali ya juu. Matokeo yake ni kupata nafuu kubwa. Ndiyo maana siku hizo haonekani kunyoosha shingo mara kwa mara kama ilivyokuwa zamani kwa wale wanaokumbuka. Tunafuatilia kwa karibu sana hali ya shingo yake. Tunamfanyia vipimo vya MRI na kuonana na madaktari bingwa mara kwa mara. Mwisho Napenda kabla ya kumalizia nisisitize tena kwa kusema kuwa mimi na daktari mwenzangu hatuna mashaka na hali ya afya ya Mhe. Rais. Afya yake ni nzuri, hana maradhi yanayotishia maisha yake au kupunguza uwezo wake wa kulitumikia taifa na watu wake. Pia maoni yetu hayo ndiyo maoni ya madaktari wa ndani na wa nje waliowahi kuhusika na uchunguzi wa afya yake. Napenda pia kuwahakikishia kuwa, sisi madaktari wake, hatutachoka kufuatilia kwa karibu na kwa umakini mwenendo wa afya ya Mhe. Rais ili tujue mapema kama kuna jambo la kushughulikia. Kwa hili lililotokea, tutaendelea kuchunguza kama jambo lolote lililojificha ambalo hatujalibaini. Kwa sasa napenda kurudia kusema kuwa hakuna ushahidi wa kitaalamu wa kusema kuwa kulikuwa na sababu nyingine zaidi ya uchovu. Rais aliondoka New York Septemba tarehe 30 saa nane ya usiku kwa saa ya hapa Dar es Salaam kuanza safari ya kurudi nyumbani. Aliwasili nyumbani saa saba ya usiku wa tarehe 1 Oktoba. Njiani alisimama London na Nairobi kuunganisha ndege. Hivyo basi, alisafiri saa 24 bila ya kulala vizuri. Isitoshe hata kwenye ndege alitumia muda mwingi akifanya kazi. Asubuhi na mapema siku ya Oktoba 2, aliondoka Dar es Salaam kwenda Arusha kufungua mkutano wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola saa nne asubuhi. Baadae jioni yake alishiriki kwenye hafla ya chakula cha jioni alichowaandalia wabunge. Rais aliondoka saa sita usiku kwenda kulala. Hatuna hakika alilala saa ngapi kwani najua akiwa na kazi huchelewa sana kulala. Tarehe 3 Oktoba, 2009 alikuwa na mikutano mfululizo na viongozi na wananchi pale Arusha kabla ya kuondoka majira ya alasiri kwenda Mwanza. Alipofika Mwanza alikuwa na mazungumzo na wenyeji wake usiku ule mpaka saa nne ya usiku. Tulipofuatilia tuligundua kuwa hata siku hiyo nayo alichelewa sana kulala kwani walipondoka wageni wake yeye aliendelea kushughulikia hotuba yake mpaka karibu na alfajiri. Katika mazingira hayo kupata matatizo ya mwili kuchoka sana, na hata kukataa kuendelea kutumika, na kutaka kupumzika kama ilivyotokea si jambo la ajabu. Mwisho kabisa napenda kuwahakikishia kuwa Rais yuko salama. Afya yake ni nzuri na haina shaka yoyote. Uchovu uliokithiri ndicho chanzo cha yaliyotokea Mwanza siku ile ya tarehe 4 Oktoba, 2009. Mimi na wenzangu katika Ofisi Binafsi ya Rais (OBR) tumejifunza na tumeazimia kuwa waangalifu zaidi katika kupanga ratiba ya kazi ya Rais. Dr. Peter Mfisi Ikulu, Dar es Salaam Daktari wa Rais 08 Oktoba, 2009

October 7, 2009

inakuwa vipi mchumba anapokuwa changudoa??

KAMPALA-Patrons at a hotel in Bakuli, Kampala were last Monday amused when a sex worker turned out to be the client’s girlfriend.
Kakooza, a student at Mbarara University, was in Kampala for a workshop. He said his girlfriend, a student at Makerere University, told him she was with her parents.
When Kakooza asked for a prostitute, the attendant brought him a lady whom he identified as Hellen. Kakooza was in shock and said the lady was his girlfriend and Hellen was not her real name.
When she realised that Kakooza was the client, she fled.
source: New Vision.
DUH! KUMBE WOTE UTULIVU SIFURI????
INGEKUWA NI WEYE MDAU UNGEFANYAJE??

.........Prof Mukandala awatwangia

Mukandala ataka wabunge wasilipwe.
Makamu mkuu wa UDSM amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari wakati akitoa mada katika mkutano wa hali ya siasa unaoandaliwa na REDET huko milmani akitaka Wabunge na wanasiasa wengine kutolipwa, akisema kuwa hiyo ni kazi ya kujitolea

wakti Idd Simba awabeep wabunge.........

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Idd Simba, amesema, lugha ya kiingereza imesababisha Tanzania iwe na sheria mbaya zikiwemo za madini.
Mbunge huyo wa zamani wa Ilala, Dar es Salaam, amesema, anaona aibu kwa kuwa alishiriki kupitisha sheria mbaya za madini zinazotumika kuinyonya nchi.
Mwanasiasa huyo amedai kuwa, chanzo cha ubaya wa sheria hizo ni lugha ya kiingereza kwa kuwa sheria zimeandikwa kwa lugha hiyo lakini idadi kubwa ya wabunge hawaielewi kwa ufasaha.
“Zile sheria ni mbaya na mimi naona aibu kwamba zilipitishwa wakati nikiwa kwenye lile Bunge, lakini unatarajia nini wakati sheria zile zinatungwa kwa Kiingereza, na si wabunge wengi wanaoelewa lugha hiyo,” amesema.

TANGAZO LA MKUTANO wa WABONGO SAUZI

HIGH COMMISSION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone:012- 342 4371/93

Fax: 012 – 430 43 83

822 GEORGE AVENUE,
P.O. BOX 56572,
ARCADIA 0007,
PRETORIA

TANGAZO LA MKUTANO WA RAIA WA TANZANIA TAREHE 24 OKTOBA, 2009

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI UNAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WANAOISHI KATIKA JIMBO LA GAUTENG KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA WATANZANIA WANAOISHI KATIKA JIMBO HILO UTAKAOFANYIKA TAREHE 24 OKTOBA, 2009 SAA NANE NA NUSU MCHANA HADI SAA KUMI NA MOJA JIONI KATIKA UKUMBI WA PRETORIA COUNTRY CLUB, NAMBA 241 MTAA WA SYDNEY, WATERKLOOF, PRETORIA.
MKUTANO HUO UNA LENGO LA KUANZISHA JUMUIYA YA WATANZANIA KATIKA JIMBO HILO.
TAFADHALI TUNAOMBA KUVAA NADHIFU NA KUZINGATIA MUDA.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NA WAFUATAO:
1. Jumanne Fhika 0762 909449
2. Faustine Ndugulile 0799 965120
3. Laurean Rugambwa 0835 566966
4. Lumbi na Ethel 012 344371/012 3425921
IMETOLEWA TAREHE: 3.10.2009
UBALOZI WA TANZANIA- PRETORIA

October 2, 2009

KWI KWI

WADAU KUNRADHI KITUMBUA SI ANDAZI, NIMEKUWA NA KWI KWI KIDOGO KTK KUPOST KUOTOKANA NA MAJUKUMU, NNAREKEBISHA MTANDAO WA HOME NA KUTUMIA ULE MKONGO ULOZINDULIWA HIVI KARIBUNI HIVYO KWIKWI HII YAWEZA KUENDELEA KWA MUDA KIDOGO. KUNRADHI, BONGO PIX

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...