December 4, 2008

ALBINO sasa wawindwa na mitutu..

TAARIFA TOKA KIGOMA NA KUTHIBITSHWA NA RPC NI KUWA:

WATU WENYE SIRAHA WAMEVAMIA NA KUMPIGA RISASI

MTU MWENYE ULEMAVU WA NGOZI YAANI ALBINO

KUMUUA NA KUONDOKA NA MKONO WAKE.

WADAU HII SASA INATISHA YAANI NDUGU ZETU SASA WANATAFUTWA KWA MTUTU WA BUNDUKI? HII NI ZAIDI ATA YA PESA, HIVI KWELI SERIKALI IMESHINDWA? JE JESHI LA POLISI NIN KWELI HALIJUI WAARIFU HAWA NI WAPI WANAPELEKA VIOUNGO HIVI VYA NDUGU ZETU HAWA? JE WALE WALIOKUWA EXPOSED NA VICKY NTETEMA WA BBC WAKO WAPI HADI SASA? NI NINI JESHI LA POLISI LIMEFANYA JUU YAO? AU KUNA USHIRIKIANO USIO RASMI HAPA? MTU ANALAZIMIKA KUWAZA MENGI KUTOKANA NA UKWELI KUWA HAKUNA HATUA INAYOONEKANA KUFANYWA NA WAHUSIKA TOKA TAARIFA ILE NZURI YA UCHUNGUZI KUTOLEWA NA HADI LEO HII MAUAJI HAYA YA KINYAMA YANAPOENDELEA KUFANYIKA NCHINI. HII INASIKITISHA SANA.

JK AKUTANA NA TSVANGIRAI

MWENYEKITI WA AU RAIS JK JANA ALIKUTANA NA KIONGOZI WA MDC CHA ZIMBABWE BW. MORGAN TSVANGIRA IKULU.

Mengi adai waziri ataka kumuhujumu..

TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI.

Hivi karibuni waziri mmoja kijana anayeongoza wizara nyeti alipendekeza nibambikiziwe kodi bandia ya kiasi kikubwa nitakachoshindwa kulipa na hatimaye nifilisiwe kama njia pekee ya kuninyamazisha kabisa eti kama alivyofilisiwa tajiri mmoja mkubwa huko Urusi.

Alidai kwamba vyombo vyangu vya habari vimekuwa mno mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.

Nilitegemea waziri huyo msomi sana angefahamu jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi. Angalao angefahamu kwamba anayeamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe ni mhariri wa gazeti ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari na siyo mmiliki wa vyombo vya habari.Kama mkiristo na kama alivyoagiza Bwana Yesu namsamehe kwa vile hajui atendalo.

Baada ya kumsamehe ningetaka ajue yafuatayo.Asiyekemea maovu katika jamii, yeye ni sehemu ya maovu hayo. Waziri huyu na wale wote ambao wamekwishanitumia vitisho wakumbuke kwamba hata kama watafanikiwa kuvinyamazisha kwa hujuma zozote zile, vyombo vyangu vya habari, na hata kama mimi sitakuwepo tena, moto wa kupiga vita ufisadi uliokwishawashwa katika akili za wanajamii hauwezi kuzimika kamwe.

Ieleweke pia kwamba sauti za maskini na wanyonge katika jamii hazisikiki kwa urahisi. Vyombo vya habari husaidia kupaaza sauti na vilio vyao katika vita dhidi ya maovu. Ni wajibu wa kila mtu aliye na uwezo kusema kwa sauti kubwa kwa niaba ya wanyonge na maskini ili kutokomeza ufisadi.

Nachukua fursa hii kumpongeza sana Rais wetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuguswa na sauti na vilio vya wanyonge na maskini wa Tanzania kuhusu ufisadi na hatua za kijasiri zinazochukuliwa na Serikali yake dhidi ya ufisadi.

Sisi sote ni lazima tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azidi kumpa ujasiri, nguvu na hekima nyingi wakati huu wa majaribio makubwa.

Reginald A. Mengi
Mwenyekiti Mtendaji
IPP Limited
3 Desemba,2008

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...