June 3, 2009

JK kuzindua rasmi Mv Magogoni

Nahodha Silvanus Lucas.  Gunter Trojahn Engineer wa Meli wa NRSW ndiye aliyesimamia ujenzi wa Ferry hii. 
Rais JK kesho anatarajiwa kuzindua rasmi Ferry ya Mv Magogoni iliyo kubwa ktk kanda ya Africa mashariki na kati ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 2000, magari zaidi ya 60 na mizigo tani kadhaa.

Kamati ya Bunge yaonya ajali ya Mwakyembe

KAMATI ya Bunge ya Ulinzi na Usalama imeeleza kutofurahishwa na kauli tata zinazotolewa kuhusu ajali ya gari aliyopata mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, ikisema zinaweza kuvuruga amani na utulivu wa nchi.

Onyo hilo lilitolewa wakati kamati hiyo ikipokea taarifa ya matukio ya ajali mbalimbali nchini, ikiwemo ya mbunge huyo liyotokea mkoani Iringa wakati akisafiri kutoka Mbeya kuja Dar es salaam katikati ya mwezi uliopita.

Tahadhari hiyo ya kamati ya bunge imekuja wakati tayari kumekuwepo na mvutano kuhusu mazingira halisi ya ajali hiyo iliyotokea Makambako, Iringa.

Mkanganyiko uliopo hadi sasa ni kuhusu kauli mbili tofauti za Jeshi la Polisi, moja ikiwa imetolewa katika ripoti ya matokeo ya uchunguzi na nyingine ikisema ripoti halisi haijatoka, huku maelezo ya ajali hiyo yaliyotolewa na polisi yakitofautiana na ya Dk Mwakyembe.

Akizungumzia mkanganyiko huo jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa kamati hiyo, Wilson Masilingi, ambaye ni mbunge wa Muleba Kusini kwa tiketi ya CCM, alisema taarifa waliyopokea kutoka polisi inaonyesha ajali hiyo ni ya kawaida kama zilivyo nyingine.

"Tumepokea taarifa ya matukio ya ajali nchini, ikiwemo zinazohusiana na baadhi yetu sisi wabunge. Kuna hii ya Dk Mwakyembe ambayo polisi wanasema ni ya kawaida kama ajali nyingine tu," alisema Masilingi.

more 

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...