October 27, 2011

Ukistaajabu ya Musa....


Hizi ni picha mbili halisi ambazo zimepitishwa photoshop kuhifadhi maadili, niliwai kupost hiyo ya chini hapa na kule facebook, nimekuwa nikipata maoni mbalimbali, lakini wengi wakitaka kujua kama hii ni picha halisi, hivyo nimeamua kuweka picha halisi ambayo sikutaka kuiweka kabla, huyu mdudu amewekwa hapo kuhifadhi maadili tu, lakini akiruka ni balaaa, 


Maswali kadhaa wachangiaji wamekuwa wakioji,
- je ni nani dada huyu? 
- Je kupanda jukwaani akiwa hivyo ni masharti ya mmiliki wa bendi au ni matakwa binafsi? 
- Je ni nchi gani na hii ni bendi gani? 
- Mamlaka husika zinasemaje juu ya hili? NK.


Kwa hakika mimi sina majibu, isipokuwa picha hii ilitoka kule Jamii Forum ambako nako kulikuwa na mjadala wake mkubwa, tena iliwekwa pasipo hako kanzi. 


Wapo wasomaji waliojaribu kubashiri ama kusema kuwa hii ni Uganda lakini wakapishana kuwa ni bendi gani. 


Mimi sijui, iwapo kuna mdau yeyote mwenye kuweza kutujuza zaidi juu ya binti huyu na maswali yoote hapo juu itakuwa vyema. Karibuni wadau. 

Msaada kwenye TUTA!!!!

Picha kwa hisani ya Bukoba Wadau Blog.

Zitto Kabwe - Hali mbaya,HALI ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan, ilibadilika ghafla jana jioni kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Zitto alilazwa Aga Khan juzi jioni baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa kabla ya kuruhusiwa na kisha kurudishwa baada ya maumivu hayo kuendelea.

Kaka wa mbunge huyo, Salum Mohamed alisema jana jioni kwamba hali ya mdogo wake ilikuwa ikiendelea vyema lakini ilibadilika ghafla na kuanza kutetemeka.

“Hali yake ya Zitto imegeuka kuwa mbaya, anatetemeka mwili mzima na sasa tunampeleka Muhimbili kwa uangalizi zaidi,” alisema Mohamed.

Jana jioni, mwandishi wa gazeti hili alimtembelea Zitto Aga Khan jana majira ya saa kumi jioni na kumkuta akiwa anaendelea vyema. Zitto, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alisema maeneo mengine katika mwili wake yalikuwa yamepona isipokuwa maumivu ya kichwa.

Awali, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Erasto Tumbo alisema Zitto anasumbuliwa na ugonjwa wa kipanda uso.

Aliwataka wanachama wake chama hicho, kumuombea kiongozi huyo ili apate nafuu na kushiriki kikamilifu kwenye vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza Oktoba 8, mwaka huu.

Source: Mwananchi.

Ajari ya Deluxe Coach - Miili 12 kuzikwa na Serikali


Picha naYassin Nicas Mtei


MIILI ya watu 12 walioteketea kwa moto katika ajali ya basi la Deluxe Coach iliyotokea Misugusugu mkoani Pwani juzi, watazikwa leo na Serikali kwa heshima zote katika kaburi moja katika eneo la Air Msae mjini Kibaha.

Eneo hilo ndipo walipozikwa watu waliopata ajali ya basi la Air Msae lililokuwa likitokea Arusha kuja Dar es Salaam miaka ya 1990.

Uamuzi huo umefikiwa jana katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani, iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mwantumu Mahiza kutokana na miili hiyo kuharibika vibaya na kushindwa kutambulika.

Akizungumzia mazishi hayo jana, Mahiza alisema kabla ya maziko, miili ya watu hao itachukuliwa sampuli kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (DNA) ili vifanikishe utambuzi wao.

Taarifa kutoka Hosptali Teule ya Tumbi, zilieleza kuwa hata wananchi waliokwenda kujaribu kutambua ndugu zao, walishindwa kufanya hivyo kutokana na kuharibika kwa miili hiyo ambayo baadhi imekuwa majivu.

Kutokana na hali hiyo, Mahiza aliwataka wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha kuwatambua ndugu zao, kwa kupeleka vitu kama nguo ambazo ndugu zao walizitumia siku chache kabla ya ajali hiyo.

Habari Leo, 


JK akutana na Jumuiya ya Watanzania Australia.

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa Watanzania waishio  Australia, Asimwe Kabunga katika mkutano huo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia) akipokea maua kutoka kwa Mweka Hazina wa Jumuia ya Watanzania waishio Australia, Maryam Powell walipokutana na wanajumuia  mjini Perth Australia.


 Rais Jakaya Kikwete alikutana  na wanajumuia  kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo na kijamii. Rais yupo nchini Australia kuhudhuria  mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuia ya madola ( Commonwealth Heads of Government meeting- CHOGM 2011,utakaoanza Oktober 28-30,2011. PICHA ZOTE/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO

Fibroids: Supplements provide permanent cure —Dr. Fadeyi

Fibroids: Supplements provide permanent cure —Dr. Fadeyi:

Definition according to Wikipedia. 

A uterine fibroid (also uterine leiomyoma, myoma, fibromyoma, leiofibromyoma, fibroleiomyoma, and fibroma) (the plural of myoma is myomas or myomata) is a benign (non-cancerous) tumor that originates from the smooth muscle layer (myometrium) and the accompanying connective tissue of the uterus.

Fibroids are the most common benign tumors in females and typically found during the middle and later reproductive years. While most fibroids are asymptomatic, they can grow and cause heavy and painful menstruation, painful sexual intercourse, and urinary frequency and urgency. Some fibroids may interfere with pregnancy although this appears to be very rare.

In the US, symptoms caused by uterine fibroids are a very frequent indication for hysterectomy. Fibroids are often multiple and if the uterus contains too many leiomyomata to count, it is referred to as diffuse uterine leiomyomatosis. The malignant version of a fibroid is extremely uncommon and termed a leiomyosarcoma
Read More HERE


Bahati njema ni kuwa Supplements hizi zilizomponya mama huyo zinapatikana hapa Tanzania pia, ikiwa kuna kina mama wenye matatizo hayo wanaweza kuwaona wasambazaji binafsi wa FLP na watawapatia hizo supplements, ikiwa haumfahamu msambazaji yeyote binafsi wa FLP, Nitwangie 0716927070, 0764927070, 0784475576 au nitumie email hapo juu, nitakuunganisha na aliye karibu yako, ili tuokoe kina mama wanaosumbuliwa na matatizo hayo. 

Google+ Followers

There was an error in this gadget
There was an error in this gadget

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...