September 22, 2011

Tuzo zaidi kwsa JK New York.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihudhuria mkutano wa 'Social Good Summit' anapokea tuzo kutoka United Nations Foundartion for his work in Martenal Health and Social Media Commitment kutoka kwa Makamu wa Rais wa Public Policy of United Nations Foundation Mr. Peter Yeo katika sherehe fupi iliyofanyika jijini New York jana.
 

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki- Moon kwenye Makao Makuu ya Umoja Mataifa jijini New York nchini Marekani.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amepokea Tuzo Mbili Maalum kwa mchango wake mkubwa katika Afya ya Mama Mjamzito na Watoto kwa ujumla kutoka taasisi mbili tofauti mjini New York.

Tuzo ya kwanza imetolewa na Taasisi ya Kijamii ya Umoja wa Mataifa (UN Foundation) na kukabidhiwa kwa Rais na Makamu wa Rais wake anayeshughulikia sera ya Umma Bw. Peter Yeo.

Rais amepokea Tuzo ya pili katika makao makuu ya Soko la Hisa la Marekani (National Association of Securities Dealers Automated Quotations) kwa kifupi NASDAQ ambalo ni soko la pili kwa ukubwa duniani baada ya lile la New York.  Rais amekabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa NASDAQ Bw. David Wicks.

 Mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Rais amepewa heshima maalum ya kugonga kengele kuashiria mwisho wa biashara kwa siku hiyo.

Akipokea tuzo hizo mbili maalum, Rais ameelezea changamoto zinazoikabili sekta ya Afya nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla na kuzishukuru nchi na taasisi mbalimbali ambazo zinaunga mkono juhudi za kupunguza matatizo ya afya ya mama mjamzito.

“Si sahihi kwa mama mjamzito kufariki wakati anampa uhai binadamu mwingine, uzazi unatakiwa kuwa shughuli ya furaha na sio huzuni na ndiyo maana tumetoa kipaumbele kwenye afya ya mama mjamzito kwenye ajenda yetu ya Afya” Rais amesema.

Rais amewaeleza wageni waalikwa ambao katika hadhara zote mbili wametoka katika nchi na taasisi mbalimbali kuwa kati ya vitu ambavyo serikali ya Awamu ya Nne imeamua kutoa kipaumbele katika kuongeza huduma za afya ya uzazi kwa kujenga zahanati na kuzipandisha daraja zilizokuwepo.

Serikali pia inaajiri wakunga na wataalamu zaidi wa Afya na kuongeza mafunzo katika sekta hiyo.

Juhudi zingine ni pamoja na kutoa huduma za Mpango wa Uzazi bure na kutoa vifaa vya kujifungulia kwa akina mama wanaohudhuria kliniki.

“Vifaa hivi ni maalum kwa ajili ya kuwasaidia akina mama wakati wa kujifungua, na tuna amini kuwa kwa kufanya hivi wanawake wengi zaidi watahudhuria kliniki na kuwapa motisha wa kujifungulia katika taasisi zetu za afya”. Rais ameeleza.

Kutokana na juhudi hizo takwimu zinaonyesha kupungua kwa vifo vya akina mama wajawazito na  wakati wa kujifungua  kutoka 8,000 kwa mwaka 2005 hadi 6,000 mwaka jana.

“Upungufu wa vifo 2,000 ni hatua nzuri katika muda mfupi lakini bado hairidhishi sana, tunaweza kupunguza zaidi na hilo ndiyo lengo letu kwani hatutaki kuona mwanamke yeyote anakufa kutokana na ujauzito au wakati wa kujifungua”. Rais amesema.

Mbali na shughuli hizo, Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Slovenia Dr. Danilo Turk, Makamu Waziri Mkuu wa Luxembourg Bw. Jean Asselborn na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon na Waziri wa Maendeleo wa Uingereza Bw. Andrew Mitchell.

Leo tarehe 22 Septemba, 2011, Rais anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
MWISHO.
 
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
New York.
Marekani.
22 Septemba, 2011


Google+ vs Facebook, nani zaidi?


V/S

Google wameanzisha social network yao iitwayo Google+, ambayo waweza kuwashirikisha ndugu, jamaa, marafiki taarifa nyingi kwa urahisi kama vile ilivyo kwa fb. 




Google+ makes connecting on the web more like connecting in the real world. Share your thoughts, links and photos with the right circles. Use easy, spontaneous video chat to strike up conversations with as many as nine people at once. Get everyone on the same page with fast, simple group chat. We’re very excited about the new approach to sharing we’ve created through Google+, but this is really just the beginning.

Nyumba ya Katibu CCM.


Katibu mkuu wa CCM, Wilson Mukama akitoka kuangalia nyumba ya Katibu wa chama hicho kata ya Nyandekwa Jimbo la Igunga, Hamis Makala iliyochomwa moto usiku wa kuamkia juzi na watu wasiojulikana. Picha na Daniel Mjema



MATUKIO ya hujuma yanazidi kulitikisa Jimbo la Igunga safari hii watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Katibu wa CCM, Kata ya Nyandekwa usiku wa kuamkia juzi.

Tukio hilo linahusishwa na wafuasi wa Chadema kutokana na ujumbe wa maandishi uliokutwa umechomekwa katika nyumba hiyo ukisomeka: “Chadema sisi ni wajanja”.Katibu huyo, Hamis Makala alimweleza Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliyemtembelea jana kumpa pole kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na wafuasi hao wa Chadema.
 
Alidai kuwa sababu ya kuwindwa na wafuasi hao inatokana na kukasirishwa na kampeni anazozifanya katika kata hiyo zinazoifanya CCM ikubalike kwa wananchi na kukiacha Chadema kikikosa watu kinapokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nyumba iliyoteketezwa kwa moto ilikuwa ikitumiwa na katibu huyo kwa shughuli za jiko na kuhifadhia kuku.

 
“Niliposhtuka na kutoka nje nilikuta moto mkubwa unawaka nikapiga yowe kuomba msaada. Lakini majirani walishindwa kuuzima kwa kuwa ulikuwa umesambaa… kuku 15 kati ya 21 waliokuwamo ndani wamekufa,” alisema.

 
Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala na asubuhi majirani walipofika tena kumjulia hali ndipo walipogundua karatasi ikiwa na ujumbe wa Chadema kuhusika.
 

Alidai kuwa mbali na ujumbe huo, upo mwingine wa maandishi ambao ulipenyezwa katika Ofisi ya CCM ya kata hiyo unaosisitiza kuwa Chadema hawahitaji bendera za CCM katika kata hiyo. Alisema kuwa karatasi zote hizo mbili zimechukuliwa na polisi.

Ziara ya JK New York

President Dr Jakaya Mrisho kikwete with NASDAQ's Vice Chairman David Wicks (right) and at the MarketSite at New York 4 Times Square 
Zanzibar and Tanzania Mainland Ministers for Health Mr Juma Duni Haji (right) and Dr Hadji Mponda, excvhange pleasantries with  Yvonne Chaka Chaka, Princess of Africa Foundation founder, renowned singer and Roll Back Malaria Goodwill Ambassador.


President Dr Jakaya Mrisho Kikwete with First Ladies, Health Ministers and Global Health Leaders cheer after the bell zanzibar

 President Dr Jakaya Mrisho Kikwete rings the NASDAQ Stock Market Closing Bell  at  NASDAQ MarketSite at 4 Times Square,   New York, Wednesday September 21, 2011

The Chief Medical Officer, Dr Deo Mutasiwa, greets Mr Andrew Whitman, after the meeting with President Kikwete. Others from left are Zanzibar Minister for Health Hon. Juma Duni Haji and Tanzania Mainland Minister for Health and Social Welfare Dr Hadji Mponda. Right is Ambassador Tatu Nuru, Personal Assistant to the President (Diplomatic Affairs)

Huruma, Upendo na Utu wetu vimeenda wapi???




Wakazi wa jiji la Dar ni nini kimetokea na kutufanya tusiwe na huruma, upendo na imani kwa wenzetu?

 Sijui ni kitu gani kimetokea ama kinaendelea jijini kiasi cha watu kukosa huruma kwa watu wengine, kujipenda ama ubinafsi umepitiliza kusema ukweli, hivi sasa anapanda mama mjamzito au ana mtoto pengine mlemavu au mzeee katika daladala hakuna hata mtu anajitingisha kumpa siti, wengine watajifanya hawajamuona, wapo watakaojiinamia kitini, saana akijitokeza msamaria mwema atampokea mama mtoto, basi. 

Lakini je ni nani awezaye kumpokea mama ujauzito wake ama ulemavu au umri wa mtu mwingine? kina mama ambao pengine ndio wangekuwa mfano wa huruma kwa wenzao kwa kuwa bila shaka wamepata kupitia hali hiyo, ndo kwanza ujifanya hawawaoni wenzao, mara nyingi kina mama hawa hupata msaada toka kwa kina baba zaidi kuliko kina mama. 

Wakati wa UDA, kwa wale ambao wana kumbukumbu nzuri au walikuwepo, kulikuwa na matangazo ndani ya mabasi, moja wapo, mbali na lile la pale mbele kwa dereva lisemalo “Basi hili limenunuliwa nusu millioni”, mengine yalikuwa yakiimiza heshima na utii katika basi, yapo yalokuwa yameandikwa “mpishe kiti mlemavu, mzee, mama mjamzito na mwenye mtoto”, nakumbuka kusoma haya nyakati zile, kwa wenzetu waliondelea ambao tunasema twanakiri toka kwao haya bado yapo, mabasi yao yana sehemu maalumu ya walemavu, mama wenye watoto, ujauzito na wazee pia. 

Hivi sasa kila kitu tunasingizia ufisadi, je hili nalo lina mkono wa mafisadi? kwamba wamechukua huruma yetu, imani na upendo wetu wa kale na kutuachia ubinafsi, choyo na kujipenda kupita kiasi? kwamba umetufanya tusahau utu wetu na ubinadamu wetu? hapana, siamini hilo. Japo kuna ukweli kiasi kuwa chanzo cha matatizo mengii yatupatayo sasa kiini chake utakuta ni ubinafsi, lakini kwa hili tuwe na huruma na ubinadamu japo kidogo.    

Kina mama hawa (pichani) walishika bomba kutoka Magomeni mpaka Mbezi, huku kina mama, baba na hata wanafunzi wamekaa vitini kana kwamba hawawaoni, hakuna anayejari, labda ifike mahali SUMATRA waagize daladala kutenga sehemu maalumu kwenye magari yao kwa makundi haya maalumu hili kupunguza usumbufu kwao.

Haya ni maoni yangu, je wewe una maoni gani?
  

"Wakusanyikapo Tai ndipo penye mzoga"

"Wakutanikapo Tai ndipo penye mzoga", 
Hawa jamaa "Bodaboda" sasa imekuwa tabu, wakiona basi la mkoa hawangoji lifike kituoni wataenda nalo wanzengea pasipo hata kufikiri sana juu ya usalama wao, si ajabu ajari zinazousisha pikipiki zimeongezeka sana hivi sasa. 

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...