April 15, 2009

Wenye DECI waibuka, Kakobe apigilia msumari wakamatwe,

Mwenyekiti wa DECI Jackson Mtaresi na Mkurugenzi Timoth Oleleiting'ye wakiongea na wahandishi leo hii.
Siku tu moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusema kuwa Kampuni ya Development Entrepreneurdhip For Community Initiative(DECI) ni upatu na inaendeshwa kinyume cha sheria za nchi uongozi wa juu wa kampuni hiyo umeomba kukutana na viongozi wa juu wa taifa na Benki Kuu ya Tanzania(BOT).
Meneja wa Masuala ya Ufundi na Ushauri wa Kitaalamu wa DECI, Arbogast Kipili akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari ( MAELEZO)alisema hawako kwa ajili ya kulumbana na serikali wala BOT ila wanaomba kupewa nafasi na viongozi hao ili waeleze namna gani wanaendesha kampuni yao.
“Tunaomba tualikwe tujieleze kwa rais, waziri mkuu na BOT kwa nini sisi sio upatu, DECI tuna mfumo unaoeleweka tofauti na taasisi nyingine ambazo hazijasajiliwa…tunahukumiwa sisi hivi hivi tu wakati lengo letu ni kukwamua wananchi wa chini kutoka katika umasikini,” alisema.
Kipili alisema wanaishukuru serikali na BOT kwa kutoa tangazo lake maana inaoonyesha kuwa inawatazama na inania ya kuona chombo hicho kinakaa katika utaratibu unaotakiwa pamoja na mapungufu yaliyojitokeza.
Wakti huo huo....................
ASKOFU Mkuu wa FGBF, Zachary Kakobe amewataka viongozi wa dini kutotafsiri maandiko ya biblia kwa maana nyingine kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kuleta uvunjifu wa amani na zaidi kuwachukulia hatua wote wanaovunja sheria za nchi pasi kuwabembeleza.
Aidha amewakata waliokwenda kuweka fedha na kuvuna katika Kampuni ya Development Entrepreneurship For Community Initiative (DECI) kuchukua fedha zao mapema kabla fedha hizo havijaingia kwenye viroba vya mikono ya watu walioanzisha kwa maslahi yao.

Ka WTC ketu almanusura kateketee

Jana jioni moto uliibuka ktk paking ya Ka-WTC ama BWM Towers ambayona kutishia maisha wapangaji wake.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...