August 12, 2011

EWURA YAKUNJUA MAKUCHA KWA BP!
HATUA ZINAZOCHUKULIWA


Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:
a) Kuziandikia ONYO KALI kampuni za Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd kuwaonya kutorudia tabia walioionesha ambayo ni kinyume na Sheria za Tanzania na kuwaagiza wauze mafuta kwa watu wote bila ubaguzi. Amri hii itafuatiliwa kwa ujirani na ikibainika wamekiuka hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao mara moja
b) Kusitisha leseni ya biashara kwa BP (T) Ltd kwa MIEZI MITATU KUANZIA LEO kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.

c) BP (T) Ltd ataruhusiwa kuendelea kuuza mafuta ya ndege kutokana na ukweli kwamba EWURA haidhibiti bei za mafuta ya ndege ambao ndio msingi wa mgomo kwa wafanyabiashara ya mafuta. 
d) Pia BP (T) Ltd ataruhusiwa kuuza mafuta yake yote ya petroli, dizeli na taa yaliyopo kwenye maghala yake kwa wafanyabiashara wengine wa jumla kama wanataka kwa usimamizi wa EWURA ili kuzuia kutoharibika kwa mafuta hayo katika kipindi hicho cha miezi mitatu ambapo hataruhusiwa kufanya biashara ya mafuta ya jumla.
e) Hata hivyo, vituo vyote vya rejareja (Petrol Stations) vya vyenye nembo ya BP vitaruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua mafuta kwa wafanyabiashara wengine wa jumla na si kwa BP.
f) Pia Bodi ya Wakurugenzi imeeagiza Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa BP (T) Ltd kufikishwa Mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Jinai (DPP).


USIMAMIZI WA MAFUTA

a) Kuanzia sasa EWURA itaendelea kuangalia mfumo mzima wa mafuta yanayoingia bandarini.
b) Pia EWURA itaendelea kufuatilia bei zinazouzwa kwenye vituo kama zinafanana na zile zilizotangazwa.

IMESAINIWA
Haruna Masebu
MKURUGENZI MKUU 

MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI (EWURA)

Kumbe ni rahisi kuondoa traffic jam jijini.


 Siku zile wauza mafuta walipogoma kuuza mafuta, magari na hasa binafsi yalihadimika barabarani, safari ya Mbezi mpaka katikati ya jiji ilikuwa yachukua dakika kadhaa na si masaa kadhaa kwa kutumia  usafiri wa umma ambao haukuwa na kasheshe sana kama ilivyozoeleka.

Hivi leo baada ya hali ya upatikanaji mafuta kurejea katika hali yake ya kawaida, barabara zimefungamana tena, asilimia kubwa ni magari binafsi ambayo waweza kuta kuna mtu mmoja saana wawili na usafiri wa umma umekuwa ni kasheshe tena, kwanini????????Nimejifunza jambo hapa, (though the hard way) kumbe tukiweza kudhibiti magari binafsi na kuboresha usafiri wa umma na kuwasimamia barabara watoa huduma tunaweza kuondoa foleni hizi zisizo za lazima jijini ambazo zinasemekana zinasababishia taifa hasara ya Tsh Billioni 4 kila siku! Taifa changa na masikini kama hili kupozea mahela yoote hayo kwa sababu ya kushindwa kufanya japo maamuzi madogo kama haya haiingii akilini.

 Labda tatizo kubwa hapa ni ubinafsi, maana wenye magari ni sisi wenyewe ambao ndio tunapaswa kuamua, sababu kuu ni kuwa twajifikilia sisi kwanza.  

Google+ Followers

There was an error in this gadget
There was an error in this gadget

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...