February 29, 2008

NENO LA LEO

“[A song of ascents.] I call on the LORD in my distress, and he answers me.”- Psalm 120:1

NYUMBA ZA MABALOZI

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA NSSF ZIMETILIANA SAINI MKATABA WA UJENZI WA NYUMBA ZA MABALOZI NJE YA NCHI AMBAPO NSSF NDIO ITAGHARIMIA UJENZI HUO.

February 28, 2008

MUAFAKA HATIMAYE

HATIMAYE MUAFAKA WA KENYA UMESAINIWA LEO KATI YA PANDE MBILI ZILIZOHASIMIANA TOKA UCHAGUZI MKUU.

PRAY IT DAILY

Dear Lord, I thank you for this day. I thank You for my being able to see and to hear this morning. I'm blessed because You are a forgiving God and an understanding God. You have done so much for me and You keep on blessing me. Forgive me this day for everything I have done, said or thought that was not pleasing to you. I ask now for Your forgiveness. Please keep me safe from all danger and harm. Help me to start this day with a new attitude and plenty of gratitude. Let me make the best of each and every day to clear my mind so tha t I can hear from You.Please broaden my mind that I can accept all things. Let me not whine and whimper over things I have no control over. Let me continue to see sin through God's eyes and acknowledge it as evil. And when I sin, let me repent, and confess with my mouth my wrongdoing, and receive the forgiveness of God. And when this world closes in on me, let me remember Jesus' example -- to slip away and find a quiet place to pray. It's the best response when I'm pushed beyond my limits. I know that when I can't pray, You listen to my heart. Continue to use me to do Your will. Continue to bless me that I may be a blessing to others. Keep me strong that I may help the weak. Keep me uplifted that I may have words of encouragement for others. I pray for those who are lost and can't find their way. I pray for those who are misjudged and misunderstood. I pray for those who don't know You intimately. I pray for those who will delete this without sharing it w ith others. I pray for those who don't believe. But I thank you that I believe.I believe that God changes people and God changes things. I pray for all my sisters and brothers.I pray for my childrens and my parents. For each and every family member in their households. I pray for peace, love and joy in their homes that they are out of debt and all their needs are met.I pray that every eye that reads this knows there is no problem, circumstance, or situation greater than God. Every battle is in Your hands for You to fight. I pray that these words be received into the hearts of every eye that sees them and every mouth that confesses them willingly..This is my prayer. In Jesus' Name, Amen.

KENYA KUZACHA

WAPATANISHI WA MGOGORO WA KENYA BADO HAWAJAKATA TAMAA WANGALI NA MATUMAINI MAKUBWA KUWA MUAFAKA UTAFIKIWA TU. HONGERENI SANA WAHESHIMIWA DUNIA INAWAANGALIA NINYI KATIKA JUHUDI ZENU HIZO, MUNGU AWAPE NGUVU, IMANI NA UWEZO WA KUMALIZA KAZI HII MLIOIANZA.
"HERI WAPATANISHI MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU"
"Blessed are the peacemakers, for they will be called sons of God." Mathew 5:9

NENO LA LEO

“For God did not give us a spirit of timidity, but a spirit of power, of love and of self-discipline.”- 2 Timothy 1:7

February 27, 2008

ICT

Waziri wa Mawasiliano na ICT Shukuru Kawambwa, Naibu Maua Daftari na Katibu Mkuu Naomi Katunzi pamoja na baadhi ya maafisa wazarani hapo walitembelea ofisi za Celtel ktk ziara ya kufaamiana.

NENO LA LEO

“Dear children, let us not love with words or tongue but with actions and in truth.”- 1 John 3:18

JK AJITOSA KENYA

Rais JK jana alielekea Kenya kujaribu kuokoa mazungumzo ya upatanishi kati ya ODM na Serikali ya Mwai Kibaki ambayo mpatanishi wake Kofi Annan alitangaza kuwa YAMEKWAMA JANA.
Raila Odinga leo hii ametangaza kusitisha maandamano aliyokuwa ameyaita kufuatia ushauri wa Mpatanishi Kofi Annan,
Ndugu zetu wakenya ebu kaeni ktk meza ya mazungumzo jaribuni kaafikiana ili kumaliza mgogoro huu kwani wanaoteseka ni raia wadogo na zaidi kinamama na watoto na si nyie wanasiasa ambao mnauwezo wa kuruka wakati wowote kwenda kokote mtakako,
jaribuni sana kuwafikilia hawa wadogo wanaoteseka legezeni misimamo yenu kwa manufaa ya wakenya wote, misimamo mikali haitasaidia ktk hali tete kama hii.
Thaminini mchango mkubwa wa wapatanishi hawa Kina Annan, Graca Machel, Ben Mkapa ambao hata kama ni wastaafu lakini wanazashghuri muhimu za kufanya ila wameziacha na kukaa nanyi kujaribu kutafuta suruhu ya jambo hili, pia michango ya viongozi mbalimbali akiwemo rais Kikwete ambaye yasemekana alilazimika kumwomba Rais wa Uturuki na ujumbe wake kuahirisha ziara na kwenda moja kwa moja Kenya kujaribu kuokoa jahazi la upatanishi.
VIONGOZI WA ODM NA SERIKALI YA KIBAKI JUKUMU LA AMANI, USTAWI NA MUSTAKABALI WA KENYA LIKO MIKONONI MWENU.

February 26, 2008

Wanawake na Sanaa ya UCHONGAJI

Muslim on HIV/AIDS

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE katika Uzinduzi wa Mkutano wa Kwanza wa Viongozi wa Dini ya Kiislamu juu ya mapambano dhidi ya UKIMWI 26 FebruarI, 2008 Mzee wetu Mh. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili; Naibu Mufti wa Tanzania; Kadhi Mkuu, Kenya; Kadhi Mkuu, Zanzibar; Waheshimiwa Mawaziri; Waheshimiwa Mabalozi wa Marekani na Uingereza; Viongozi na wasomi wa Dini ya Kiislamu, Mabibi na mabwana, Assalaam Alaykum, Ni faraja kubwa kwangu kujumuika nanyi katika mkutano wenu huu muhimu unaozungumzia jambo ambalo linaathiri na kuwagusa watu wetu wengi na pia maendeleo yetu kama nchi. Sina budi kuwapongeza kwa dhati kwa kuamua kulijadili tatizo hili ambalo ni muhimu kwetu sote na ufumbuzi wake unahitaji mchango wa kila mmoja wetu wakiwemo viongozi wetu wa dini. Kama mnavyofahamu hii ndiyo sera ya serikali yetu. Sote tunafahamu kwamba hali ya UKIMWI kulingana na taarifa za awali za zoezi la upimaji wa hiari nililolizindua tarehe 14 Julai, 2007 hapa Dar es Salaam na kupata muitikio nchi nzima unaonesha kuwa maaambukizi ya UKIMWI nchini ni wastani wa asilimia 5. Hadi sasa watu zaidi ya milioni 3.4 ambao ni sawa na asilimia 85 ya lengo wameshajitokeza kupima virusi vya UKIMWI kwa hiari. Mbali na mafanikio yetu katika upimaji, bado UKIMWI unaendelea kuwa tishio maana unaambukiza hasa wale waliyo katika rika tunalolitegemea kama nguvu kazi ya nchi, yaani miaka 14 hadi 45, wanawake na wanaume. UKIMWI hauchagui umri, dini, wala nafasi ya mtu katika jamii; kwa mfano watoto 1,400,000 (wenye umri wa chini ya miaka 17) wamepoteza mzazi mmoja au wote kutokana na UKIMWI. Leo hii hakuna familia hata moja katika jamii yetu na wa dini zetu zote ambao hawajaathirika na UKIMWI kwa njia moja ama nyingine. Kwa mfano, kila mwaka takriban watoto 50,000 hadi 60,000 (yaani watoto 138 kila siku; 5 hadi sita kwa kila saa moja) wanazaliwa wakiwa na virusi vya UKIMWI. Hii ni kuonyesha tu ukubwa wa tatizo hili. Wataalam wanatuambia kuwa makisio ya umri wa kuishi ya Mtanzania leo hii yanakadiriwa kupungua kutoka miaka 52 kabla ya nchi yetu kukumbwa na tatizo la UKIMWI hadi miaka 37 ifikapo mwaka 2010. Kama havitapigwa vita, UKIMWI na virusi vya UKIMWI vitakuwa tishio kubwa katika fursa za taifa za maendeleo ya kiuchumi na uhai wa watu wetu kwa jumla. Leo hii mama mwenye umri wa miaka 20 ni mjane. Watoto wa umri wa miaka 5 ni yatima. Hali hii siyo nzuri hata kidogo. Uwezo wa kukabiliana na janga hili kwa Waislamu hivi sasa ni mdogo sana kutokana na kutokuwa na msimamo na mbinu za pamoja miongoni mwa viongozi na wasomi wa Kiislamu. Pia jamii ya Kiislamu inakabiliwa na wasiwasi wa kulijadili tatizo hili, au kutolikubali tatizo. Aidha, kuna ukimya, usiri na wakati mwingine kuna taarifa potofu, unyanyapaa, kunyoosheana vidole na kutofahamika nafasi ya Uislamu katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Kwa ujumla kuna ukosekanaji wa wazi wa programu za UKIMWI zinazowahusisha waumini wa Kiislamu moja kwa moja. Nafurahi kuwa nyinyi viongozi sasa mmekubali kwa pamoja kuchukua nafasi yenu katika kupambana na janga hili. Kama mnavyofahamu dini ina nafasi kubwa na imekuwa kimbilio la mwanadamu tangu enzi za utumwa na katika majanga ya asili kama njaa, mafuriko, matetemeko, vita, na sasa UKIMWI. Dini ina nafasi sio tu katika kuzuia kuenea kwa UKIMWI bali pia katika kuwatunza yatima na kuwafariji kiimani wagonjwa wa UKIMWI. Aidha, Jumuia za Kidini Tanzania zina utamaduni wa muda mrefu na wa kipekee wa kuongoza watu katika mwanga nyakati za matatizo makubwa na kuwajali waumini wake. Pia zimejithibitishia kuwa mhamasishaji mkuu wa wanaume, wanawake na watoto. Ni matumaini yangu kuwa baada ya semina hii ya leo Misikiti itakuwa imeona mwanga na kuanza kuchukua hatua mbalimbali kufikia vijana wa rika zote na wa jinsia zote. Pia nafasi hii tuitumie kuhakikisha kuwa maadili yanadumishwa yakiwemo yale tunayofundishwa kwenye msahafu kuhusu matunzo ya yatima na wajane na hatari ya dhuluma kwa makundi haya ya watu. Nimearifiwa kwamba warsha yenu inalenga kuandaa tamko la pamoja juu ya mbinu za kukabiliana na UKIMWI, kuimarisha nia thabiti ya viongozi wa Kiislamu juu ya kupambana na UKIMWI na kujiongezea uwezo wa kuendesha programu za kupambana na UKIMWI miongoni mwa jamii zenu. Hivyo muda sasa umefika kwa viongozi wa Kiislamu hapa nchini kutambua kwa kupitia tamko mtakalolitoa kwamba ni kwa kujitolea, na kutumia nguvu za akili na uthubutu wa moyo ndipo tutakapoweza kuushinda UKIMWI. Napenda kurudia kwenu kuwa Tanzania bila UKIMWI inawezekana ikiwa kila mmoja wetu atashiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Kwa tamko lenu mtakuwa mnatangaza nia yenu ya kutekeleza yote yaliyo ndani ya uwezo wenu katika kutokomeza janga la UKIMWI, kupiga vita woga, unyanyapaa na kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya UKIMWI na virusi vya UKIMWI. Pia kwa tamko lenu mtakuwa mnaazimia kuendeleza programu za kuzuia UKIMWI kwa vijana wetu, kujenga ufahamu wa UKIMWI na mikakati ya kuuzuia kwa pamoja kwa kutoa ushauri nasaha na kupima. Ninafurahi kuona kuwa mmewaalika wenzetu kutoka nchi za jirani ambao nao wana harakati kama za kwetu za kupigana na janga hili la UKIMWI. Hilo ni jambo zuri kwani tunapobadilishana mawazo ndipo tunapopata ufumbuzi ambao pengine umeishajaribiwa na wenzetu na kuonekana unafaa. Hali kadhalika, nasi nina hakika tunayo mengi ambayo tumeyajaribu na yanafaa kwenye hali yetu hapa Tanzania. Wenzetu nao wanaweza kujifunza kutoka kwetu. Maana UKIMWI hauna mipaka. Mwisho, napenda kutumia fursa hii kuwashukuru kwa dhati Waheshimiwa Mabalozi wa Marekani na Uingereza ambao wamesaidia kufanikisha mkutano huu muhimu. Tunawashukuru sana kwa mchango wao. Kwa hayo machache, nawatakia mkutano mwema, Inshallah Mwenyezi Mungu ajaalie mkutano huu utoe matunda mema ya kuwa na kauli ya pamoja inayolenga kupunguza kasi ya maambukizi mapya na pia kupunguza makali kwa wale ambao tayari wameambukizwa virusi vya UKIMWI. Serikali inafanya jitihada zote ili kuhakikisha kuwa zoezi la upimaji linaendelea vizuri na dawa za bure kwa waathirika zinakuwepo. Baada ya kusema hayo sasa natamka kuwa mkutano huu umefunguliwa rasmi. Asanteni kwa kunisikiliza.

Flaviana ndani ya Denmark

Miss Universe Flaviana MATATA yuko Denmark kujaribu bahati yake na makampuni mbalimbali ya urembo nchini humo, Bongo pixs inakutakia kila la kheri dada Matata. picha kwa hisani ya BC.

Mambo ya PWANI

Najua wengine wenu mate/udenda wawatoka hasa mlo masafa huko ambao mlishazoea mambo ya forodhani au pale Ntwara nn'jini mambo ya mwengo hayooooooo.

VERSE OF THE DAY

“This is how God showed his love among us: He sent his one and only Son into the world that we might live through him.”- 1 John 4:9

Ziara ya Rais yaahirishwa

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS UNITED REPUBLIC OF TANZANIA Telephone: 255-22-2114512, 2116898 Fax: 255-22-2113425 PRESIDENT¢S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Ziara ya Rais wa Uturuki yaahirishwa Na mwandishi maalum, `Ziara ya Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Abdullah Gul katika Tanzania, iliyokuwa ianze leo, imeahirishwa.. Rais Gul alitarajiwa kuwasili nchini leo, kwa ziara rasmi ya siku mbili kwa mwaliko wa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Rais Gul alitarajiwa kuwasili nchini na kundi kubwa la wafanyabiashara wapatao 160 kutoka Uturuki. Wakati wa ziara yake, mbali na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Kikwete, Rais Gul pia alitarajiwa kuhutubia mkutano wa pamoja wa wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki. Tanzania na Uturuki pia zilitarajiwa kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kiufundi, kisayansi na kiuchumi katika eneo la kilimo. Imetolewa Na Bw. Salvator Rweyemamu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Habari, Ikulu, DAR ES SALAAM. 26 Februari, 2008

February 25, 2008

VERSE OF THE DAY

“Jesus replied: " 'Love the Lord your God with all your heart and with all your soul and with all your mind.' This is the first and greatest commandment. And the second is like it: 'Love your neighbor as yourself.”- Matthew 22:37-39

February 22, 2008

Pinda na Askofu

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akibusu pete ya askofu, Isac Amani wa Jimbo katoliki la Moshi baada ya askofu huyo kusimikwa na Askofu Mkuu, Mwadhama Kardianli Polycarp Pengo kwenye kanisa kuu la Moshi jana.

Semfuko, Kilonzo wastaafu Jeshi

Wastaafu wa TPDF Afande Semfuko na Kilonzo wakipongezana jana

Uwekezaji Kilimo

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mkutano wa tano wa EU-SADC Agro Industry 2008 May, mkutano huu walenga kilimo, chakula na mambo yote yahusuyo sekta hii ya kilimo kwa nchi wanachama wa SADC, kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yao http://www.agro-ind2008.com/ Above, the team leader Flor Healy flanked by Tanzania Women Chambers of Commerce Chairperson Dina Bina gestures during press briefing on the coming Agro Industry 2008 in Dar es Salaam yesterday.

VERSE OF THE DAY

“There is no fear in love. But perfect love drives out fear, because fear has to do with punishment. The one who fears is not made perfect in love.”- 1 John 4:18

February 21, 2008

VERSE OF THE DAY

“The commandments, "Do not commit adultery," "Do not murder," "Do not steal," "Do not covet," and whatever other commandment there may be, are summed up in this one rule: "Love your neighbor as yourself." Love does no harm to its neighbor. Therefore love is the fulfillment of the law.”- Romans 13:9-10

Richmondzzzzzzzzzz

TANESCO yaendelea kuilipa Richmond mamiloni Licha ya Kamati ya Bunge kupendekeza kufutwa kwa mkataba wa Richmond na kutaka malipo ya Sh. milioni 152 yanayotolewa kwa Dowans kila siku yasitishwe hadi jana Shirika la Umeme(TANESCO) liliendelea kuilipa kampuni hiyo. Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bw. Daniel Mshana aliliambia gazeti hili jana katika mahojiano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kuwa shirika linasubiri maelekezo kutoka serikalini.

Mambo ya Kipanya

Wana Jambo Forum kulikoni?

Wafichua ufisadi kwenye mtandao wahojiwa Polisi. WAMILIKI wa mtandao wa kompyuta ujulikanao kama Jambo Forum ambao umekuwa mstari wa mbele wa kuendesha mjadala juu ya madai ya ufisadi serikalini, wamekamatwa na kuhojiwa na Polisi, kwa madai ya kukashifu na kufanya uchochezi. Mkuu wa Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema alithibitisha jana kuwa wanaendelea kuwahoji watuhumiwa wawili, kwa kile alichokieleza kuwa ni kujihusisha na uhalifu wa mtandao wa kompyuta. Alisema baadhi ya watu wanaojadiliwa kwenye mtandao huo ambao wanahusishwa na tuhuma za ufisadi, ndiyo walioulalamikia mtandao huo kuwa unatumika kuwakashifu na kuchochea hasira za wananchi dhidi yao. Mtandao wa Jambo Forum (JF) umekuwa maarufu nchini kutokana na watu wengi kutoa maoni yao katika matukio mbalimbali yanayotokea nchini. Masuala ya ufisadi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kashfa ya Richmond ni mambo ambayo yamekuwa yanatawala mjadala kwenye mtandao huo. Katika siku za karibuni mtandao huo umekuwa na mjadala mpana kuhusu waliojiuzulu serikalini na kutajwa bungeni baada ya kuhusishwa na kashfa ya Richmond. Mwema alikataa kuwataja watuhumiwa hao, lakini gazeti hili limebaini kuwa waliokamatwa na kuhojiwa na Polisi ni Maxence Melo na Mike Mushi, wote wakazi wa Dar es Salaam. Vijana hao ndiyo wanaomiliki mtandao huo ambao pia unachangiwa maoni na wananchi mbalimbali, wakiwamo waandishi wa habari na watu wengine maarufu. Mwema hakueleza uchochezi waliofanya au kashfa waliyoitoa watuhumiwa hao kupitia mtandao wa Jambo. “Baadhi ya taarifa zimeonekana kuwa za uhalifu, kukashifu na uchochezi. Polisi inatambua na kuheshimu uhuru wa katiba wa kila mtu kutoa maoni na mawazo yake na litaendelea kufanya hivyo. Lakini hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,” alisema. Mwema alisema uhuru huo usitumike kama kivuli cha kuhalalisha utendaji wa uhalifu. Alisema sheria za nchi zinazoruhusu utoaji wa maoni uzingatiwe na kila mtu. Alisema itakapobainika uvunjaji wa sheria unatokana na matumizi mabaya ya mitandao, watakaohusika watachukuliwa hatua za kisheria. Baadaye DCI Manumba alisema kuna baadhi ya watu wamelalamika kwamba wanakashifiwa katika mtandao huo. Alisema kuna habari nyingi kwenye tovuti hiyo, kwa sasa wanaendelea kuchambua baadhi ya habari zinazodai kuwakashfu baadhi ya watu. “Tutashirikiana na wananchi ambao wamelalamika kuona ni habari gani za kuwakashifu na za uchochezi, kwa sasa siwezi kuzitaja habari hizo,” alisema DCI Manumba alipojibu maswali ya wanahabari. Mwanasheria wa watuhumiwa hao, Tundu Lissu, aliliambia gazeti hili jana kuwa wateja wake wamehojiwa kutokana na mijadala inayoendelea ya ufisadi nchini. Mwanasheria huyo alisema kitendo cha kuwahoji wateja wake kwa mjadala huo ni kinyume cha sheria, kwa vile mtandao ni kitu kinachotumiwa na watu wengi kutoa maoni yao kuhusiana na mjadala uliopo kwa wakati husika. Lissu alisema kwamba wateja wao wamekamatwa kuanzia juzi wakahojiwa kwa zaidi ya saa 14 kinyume cha sheria. “Wamehojiwa kwa saa14 na wameachiwa leo asubuhi (jana) kwa dhamana,” alisema. Wakati huo huo, polisi imekiri kuwa inawashikilia baadhi ya watu kwa tuhuma za kupanga vitendo vya kigaidi wakilenga kufanya mashambulizi wakati wa ujio wa Rais wa Marekani George W. Bush. Mkuu wa Polisi Mwema alisema jana kuwa polisi walikuwa na taarifa za watu hao kutokana na mienendo yao na mawasiliano waliyokuwa wanayafanya na baadhi ya watu katika nchi za Kenya na Somalia. Mwema alisema walilazimika kuwakamata watu hao kuzuia kitendo chochote cha kigadi ambacho kililengwa kufanywa na watu hao. IGP alisema hata kama wasingefanikiwa kuleta madhara katika msafara wa Rais huyo wa Marekani, wangefanya kitendo hicho sehemu yoyote. “Sisi tunaamini kuwa kama wangefanya kitendo hicho cha kigaidi sehemu nyingine kwa nia ya kuvuruga ziara hiyo ingekuwa sifa mbaya kwa taifa letu, ni kutokana na hali hiyo tumelazimika kuwakamata na tunaendelea kuwahoji,” alisema Mwema. Hata hivyo, Mwema hakutaja majina ya watu wanaoshikiliwa. Alisema baadhi wamekamatwa mjini Arusha ambako watu wanane wanawahoji wakati mjini Dar es Salaam wanashikiliwa watu wengine wawili na kufanya idadi ya watu hao kuwa tisa. Rais Bush alianza ziara nchini Jumamosi iliyopita na aliondoka juzi baada ya kutembelea mikoa ya Dar es Salaam na Arusha.

February 20, 2008

Lowassa akabidhi Ofisi

Lowassa akabidhi rasmi ofisi leo hii.

Musyoka ndani ya Bongo

Makamu wa Rais wa Kenya kalonzo Musyoka amewasili leo akiwa na ujumbe maalum toka kwa Rais Kibaki kwenda kwa JK.

Art in Photo

Picha zina kazi na eneo kubwa sana la kufanyia kazi hii ni mojawapo.

VERSE OF THE DAY

“He who covers over an offense promotes love, but whoever repeats the matter separates close friends.”- Proverbs 17:9

February 19, 2008

Pinda amtembelea mama Nyerere

Waziri Mkuu Mizengo Pinda leo hii amemtembelea
Mama Maria Nyerere home kwake Msasani.

Bye bye the BUSHES

JK anakilasababu ya kuyarudi mangoma kwani kuwa na ugeni mkubwa kama huu na ukaondoka salama salimini si mchezo. kavarege nayo haikuwa haba mapaparazi wa kibingo tulienda sambamba na wa majuu, ni kweli tunazidiwa kidogo na wenzetu hasa kwenye mambo ya mtandao kwa kweli twaitaji kujiimarisha au kuimarishwa eneo hilo zaida pamoja na vifaa bora zaidi ya tulivyonavyo.

BUSH amaliza ziara Bongo

Rais George Bush amemaliza ziara yake ya kitaifa ndani ya Bongo leo hii na kuelekea Rwanda ambapo atakaa masaa machache na kuendela ktk nchi nyingine za Kiafrica.

VERSE OF THE DAY

“Dear friends, since God so loved us, we also ought to love one another. No one has ever seen God; but if we love one another, God lives in us and his love is made complete in us.”- 1 John 4:11-12

February 18, 2008

Kipanya wa leo

VERSE OF THE DAY

“For I am convinced that neither death nor life, neither angels nor demons, neither the present nor the future, nor any powers, neither height nor depth, nor anything else in all creation, will be able to separate us from the love of God that is in Christ Jesus our Lord.”- Romans 8:38-39

Karamagi Mtaani

Bongo pixs leo imekutana uso kwa uso na aliyekuwa Waziri wa Nishati Mh Karamagi mtaani akisalimu kila anayekutana naye, ni muungwana kweli bwana huyu.

February 17, 2008

Bush ndani ya Bongo

Bush amwambia JK baada ya kusaini mafweza:-
"You are a good man, Mr. President, and I am proud to callyou friend,"
Presidents George W. Bush (US) and Jakaya Kikwete Tanzania signed a multi-million dollar aid deal with the government of Tanzania yesterday morning on the second stop of his five-nation tour of Africa. The compact will provide a $698 million Millennium Challenge grant to the nation the bigest ever. Bush's six-day tour of the continent is intended to stress U.S. initiatives to combat HIV/AIDS, malaria and poverty in the region.

VERSE OF THE DAY

“Who shall separate us from the love of Christ? Shall trouble or hardship or persecution or famine or nakedness or danger or sword? No, in all these things we are more than conquerors through him who loved us.”- Romans 8:35,37

Bush JK Signs MCC

Hapa pasipo mazingira mazuri mpangilio mwanana tusingeweza kupata picha nzuri hizi, kama wangekuwa ni watu wetu hapa wote wangekuwa wamejaa mbele ya waheshimiwa hawa kln angalia jinsi mpangilio ulivyo swaafi.

Bush amwaga mapesa Bongo

Bush aliongozana na mkewe pamoja na Condoleza Rice, yako mambo mengi sana ya kujifunza kutokana na ujio huu kwa kitengo cha mawasiliano cha ikulu, wanausalama pamoja na waandishi na hasa watumia kamera. jinsi ya kufanya kazi au kutuwezesha wapigapicha kupata picha nzuri pasipo na bughuza yoyote nadhani hili ni somo kubwa sana kwa ndugu zetu wa usalama ambao wanadhani kuwa kazi ya ni kuzibiti wapigapicha tu, na si kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa picha bora na si bora picha. Kuna watu wanaitwa Visual Advisors hawa ni watu muhimu sana kuwa nao kama ikulu hakuna mtu kama huyu basi ni vyema kufanyike utaratibu wa kupata mtu huyu. yeye ni kiungo muhimu sana si tu ktk kuhakikisha kuwa panakuwa na mazigira au mandhali nzuri na mwaga tosha eneo la tukio bali pia ni kiungo kati ya kameraman na usalama ktk kuhakikisha kila mtu anafanya kazi yake vizuri.

Bush JK wasaini MCC $700

Marais George Bush wa USA na Kikwete wa Tanzania leo asubui Dar au jiji la Bongo wamesaini MCC wa Dola Milion 700 kwa ajili ya miuondo mbinu na afya, huu ni Msaada mkubwa kabisa kuwai kusainiwa au kutolewa na serikali ya marekani.

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...