April 29, 2008
VERSE OF THE DAY
“And without faith it is impossible to please God, because anyone who comes to him must believe that he exists and that he rewards those who earnestly seek him.”- Hebrews 11:6
Neno la wiki
Gaurding Your Ways
In Psalm 39:1, we are given an important warning,I said,
"I will guard my ways, lest I sin with my tongue; I will restrain my mouth with a muzzle, while the wicked are before me."
The Hebrew word translated ways in this passage literally means a well-trodden path. It paints the picture of a pathway that has been walked down so many times that a groove has been worn in that path.
The psalmist is drawing our attention to something that has been repeated again and again, a response that has been so often repeated that it has become engrained in our behavior—a habit.You have probably heard the saying, "He's set in his way," meaning it is not likely you are going to change the way a person acts in certain instances. The "ways" are habits, attitudes, and responses that aren't likely to change without a very powerful motivation or without some sort of an encounter with God.
I think virtually every habit we have initially began with a thought. Sow a thought; reap an action. Sow an action; reap a habit. Sow a habit; reap a character. Sow a character; reap a destiny. It all goes back to a thought that perhaps should have been dealt with, but wasn't.Take some time to consider your thoughts.
Are you giving way to thoughts that will lead to ungodly habits? If so, give those thoughts to God and ask Him to help you think the thoughts that will lead to godly habits.
April 28, 2008
KIJANA ADAI ANA VICHWA 50 ZAIDI!!!!
Aliyekutwa akitafuna kichwa cha mtoto atoa madai mazito.
Kijana Ramadhani Seleman Mussa (18), anayedaiwa kukutwa akitafuna kichwa cha mtoto Salome Yohana (3), amedai kumiliki vichwa vingine 50. Mbali ya kumiliki vichwa hivyo, pia kijana huyo amedai kwamba, amekuwa `akitengeneza` ajali barabarani kwa njia za kishirikina kwa lengo la kujipatia damu ya kunywa.
Alitoa madai hayo jana katika kituo kidogo cha polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam ambako anashikiliwa pamoja na mama yake mzazi, Khadija Ally na baba yake wa kufikia, Lucas Kibaya.
Akiwa kituoni hapo, kijana huyo alionekana akitoa maelezo hayo kwa ujasiri na pasipo wasiwasi wowote. Hata hivyo, kutokana na maneno mazito na yakutisha aliyokuwa akiyatoa, polisi walilazimika kuwaondoa baadhi ya watu katika chumba cha mahojiano. Watu walioshuhudia mahojiano hayo , waliiambia Nipashe kuwa, Ramadhani aliwaeleza polisi kwamba, anamiliki vichwa hivyo 50 kwenye maeneo tofauti hapa jijini Dar es Salaam na mkoani Mtwara alikodai alikuwa akiishi na baba yake mzazi.
Aidha, alidai kuwa ametega`kombora` la kichawi la kusababisha ajali katika barabara ya Morogoro pembezoni mwa daraja la Manzese ambalo hutumiwa na watembea kwa miguu. Madai hayo yaliungwa mkono na majirani wa sehemu aliyokuwa akiishi kijana huyo, eneo la Segerea kwa Bibi. Mmoja wa majirani hao, Bw. Sadi Marando, alidai kuwa, kijana huyo alimweleza kwamba, kila baada ya miezi mitatu, hupata kiu ya kunywa damu ya mtu.
Bw. Marando, amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kumshikilia mama wa kijana huyo kwa madai kwamba, Ramadhani alikuwa akisema siku zote kwamba, kazi zote za ushirikina hushirikiana na mama yake Khadija Ally. ``Kijana yule ni hatari ukisikiliza masimulizi yake unaweza kukimbia, hapa mtaani alikuwa na maisha ambayo kwa kweli yalikuwa ya kutisha, si mtu wa kawaida,`` alidai Bw. Marando.
Bw. Marando, alisema kutokana na kijana huyo kutoonekana kama binadamu wa kawaida, majirani walikuwa wakimhoji kila mara na kuna siku alisema kwamba wanacho kikundi chao chenye watu 10 akiwemo mama yake na kwamba yeye ndiye kiongozi.
Alisema katika mfululizo wa vituko vya kijana huyo, Alhamis iliyopita alitaka kumchinja mdogo wake, Pascal Lucas. ``Alikuwa ameshamkanyaga chini kama kuku na kuanza kumchinja, bahati nzuri majirani wakafanikiwa kumkamata, nadhani kiu ya damu iliendelea ndiyo maana alimteka na baadaye kumuua Salome,`` alisema Bw. Marando.
Ramadhani amenukuliwa akisema kwamba `makao makuu` ya kundi hilo yako mkoani Mtwara na wameweka `matawi` maeneo ya Manzese Darajani na Buguruni, jijini Dar es Salaam. Polisi mmoja wa kituo cha Stakishari aliyeomba jina lake lisitajwe, alisema Ramadhani bila woga amesisitiza kwamba, si mara yake ya kwanza kula nyama ya mtu na kwamba ataendelea kwa vile nyama za watu ndizo humpa nguvu katika mambo ya kishirikina.
Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Bw. Charles Mkumbo, alisema upelelezi na maneno yaliyozungumzwa na kijana huyo ni siri yao kwa ajili ya kutengeneza kesi. Alisema hata kama kijana huyo anadaiwa kutoa maneno hayo, polisi hawatishiki na watamfungulia kesi kama muuaji wa kawaida. ``Tunachopeleleza sasa ni siri yetu, tunatafuta ushahidi na kujua mazingira ya tukio hilo na sisi tutamshughulikia kama muuaji mwingine yeyote na kamwe suala la uchawi kwetu halipo,`` alisema Kamanda Mkumbo. Alipoulizwa kwamba kama polisi hawasadiki taarifa za uchawi ni kwanini wanawashikilia wazazi wa kijana huyo, Kamanda Mkumbo alijibu kwamba, wanawashikilia kwa kutambua kuwa, huenda wanajua mengi juu ya mtoto wao kutokana na kuishi naye kwa muda wote. Kuhusu mazishi ya marehemu mtoto Salome, Kamanda huyo alisema polisi haina neno juu ya hilo bali inasubiri taratibu za maziko zitangazwe na familia. Hata hivyo, alisisitiza kwamba, kabla ya maziko, lazima mwili wa marehemu ufanyiwe uchunguzi ambapo polisi wameomba ndugu wapeleke mwakilishi atakeyeshuhudia. ``Ndugu wakiwa tayari, muda wowote waje tuwakabidhi mwili, lakini kwaza tutaufanyia auchunguzi,`` alisisitiza Kamanda. Nipashe ilitembelea familia ya marehemu huyo huku mama na baba wa mtoto aliyeuawa kwa kuchinjwa, wakiwa wamegubikwa kwa majonzi. Mama wa mtoto huyo, Bi. Pendo Dunstan, alisema majonzi aliyo nayo hawezi kuyaelezea. ``Ni Mungu tu anayejua moyo wangu unaugua kwa jinsi gani,`` alisema kwa masitiko makubwa. Naye baba wa marehemu, Bw. Yohane Majana, aliwataka polisi wamuachie huru kijana huyo anayedai kuwa ni mchawi ili na yeye amwonyeshe uchawi wa kisayansi. ``Wamwachie! Mimi naomba aachiwe huru ili nikutane naye ana kwa ana tuone,`` alisema.
Kuhusu mazishi, Bw. Majana alisema bado wanajikusanya ili kupata fedha hasa ikizingatiwa kwamba familia yao ni maskini. Alisema ndugu na jamaa walitarajiwa kukutana jana kwa ajili ya michango na kwamba wanatarajia mazishi yafanyike leo eneo la Segerea. Wakati huo huo, Godfrey Monyo na Karama Kenyunko wanaripoti kuwa, polisi jijini Dar es Salaam, inawashikilia wazazi wa mtoto aliyekutwa na kichwa cha mtoto katika mfuko wa rambo. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Bw. Charles Mkumbo, alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo na kwa kuanzia wameanza kwa kuwashikilia wazazi wa mtoto huyo. ``Tumewashikilia wazazi wa mtoto aliyesababisha mauaji hayo na mtoto mwenyewe pia tunaye kwa hiyo tunaangalia nini kifanyike ili kubaini chanzo cha tatizo hilo,`` alisema. Kamanda Mkumbo alisemapolisi hawaamini kama suala hilo ni la uchawi bali ni tukio la uhalifu kama mengine na kuwataka wananchi kuwapa muda ili kulifanyia uchunguzi kwa kina.
Alisema uchunguzi utakapokamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara moja kujibu tuhuma hizo.
Jumamosi ya wiki iliyopita, kijana Mussa (18) anayedaiwa kuingia jijini Dar es Salaam akitokea Mtwara, alinaswa akiwa na kichwa cha mtoto. Mtoto huyo wa kike, Salome Yohana, alipotea nyumbani kwao Tabata Segerea, wiki iliyopita na baadaye kiwiliwili chake kilikutwa katika choo cha nyumba ya jirani kabla ya kupata taarifa za kuonekana kwa kichwa chake hospitali ya Taifa Muhimbili. source Nipashe
Neno la Leo
“Your attitude should be the same as that of Christ Jesus: Who, being in very nature God, did not consider equality with God something to be grasped, but made himself nothing, taking the very nature of a servant, being made in human likeness. And being found in appearance as a man, he humbled himself and became obedient to death— even death on a cross!”- Philippians 2:5-8
Precision yaja na BOEING 737-300
Abiria wakiwasili ktk jiji la Mwanza au Rock city.
Captain Kalero Mkandawile na First Officer Owen Mshiu wakiwa tayari kuluka ktk Boeing 737-300
Kampuni ya Precision air leo imezindua ndege yake mpya ya Boeing 737-300 yenye uwezo wa kuchukua abiria 116, hii ni ndege ya kwanza kubwa na yenye uwezo wa kuchukua abiria wengi kwa kampuni hii
April 27, 2008
Hii inasikitisha sana jamani. ni KALI YA KARNE.
Huyu ni mmoja kati ya wale vijana waliodaiwa kuanguka kimiujiza pale Mikochen B Assemblies of God kwa Mchungaji Dr Getrude Lwakatare, ila mamlaka zilidai kuwa ni matapeli na hivyo kuonekana kana kwamba Mch. Dr Lwakatare alikuwa amepanga nao, lakini Mungu kadhiirisha ukuu wake.
Hii ni kali ya karne.
Kijana akamatwa na kichwa akifyonza damu
Ramadhani Musa (18) anayedaiwa kuingia Dar es Salaam juzi akitokea Mtwara, amenaswa akiwa na kichwa cha mtoto mdogo. Mtuhumiwa alikamatwa na walinzi wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam jana asubuhi akijaribu kukipitisha kwa staili.
Akiwa na kifurushi aliwahadaa walinzi kuwa anakwenda kumuona shangazi yake, hata hivyo walimshtukia baada ya kuona damu zimetapakaa mdomoni.
Walipokagua kifurushi walikuta kichwa cha mtoto wa kike aliyekuwa amesukwa mtindo wa `twende kilioni` kikichuruizika damu. ``Kijana huyo alikichukua mbele ya walinzi hao na kuanza kufyonza damu na kujilamba midomo, `` alidai mlinzi na kuongeza kuwa aliwauliza kwa ujasiri mnashangaa nini? ``Kwetu ni kitu cha kawaida kula nyama za watu.`` Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Ilala wa Bw. Charles Chambo, alithibitisha kutokea kwa mkasa huo na kueleza kuwa kichwa hicho ni cha Salome Yohana (3).
Kwa mujibu wa mama Salome, Bi. Pendo Dutsan, binti yake alitoweka juzi usiku nyumbani kwa shangazi yake anayeishi Segerea na kwamba kabla ya kuishia alikuwa akicheza nje ya nyumba yao.
Waligundua kuwa hayupo wakati wa chakula cha jioni na kuanza kumtafuta lakini bila ya mafanikio hadi jana asubuhi, mgeni wa jirani yao aliyetajwa kwa jina la Lucas Kibaya, alipogundua kiwiliwili chake chooni. Alidai Kibaya aliingia chooni na kukuta tofali limefunika tundu na alipoliondoa aliona kanga iliyokuwa na damu na kugundua kiwiliwili cha mtoto kilichonasa kwenye tundu hilo.
Baada ya kutoa taarifa, polisi wa kituo cha Stakishari Ukonga walifika na kuopoa kiwiliwili hicho na kutafuta gari ili kunyonya uchafu ili kutafuta kichwa ambacho kilikuwa hakionekani. ``Wakati tunaendelea kukisaka kichwa polisi walitueleza kuwa walipokea taarifa za kukamatwa kwa Musa akiwa na kichwa Muhimbili,`` alisema mwanamke huyo akilia kwa uchungu. Aliongeza kuwa polisi walikichukua kiwiliwili pamoja kuwakamata watuhumiwa ambapo mwili huo ulikuwa chooni kwao hadi kituo cha Stakishari.
Baada ya taarifa za kupatikana kichwa hicho, watuhumiwa ambao kiwiliwili kilikuwa nyumbani kwao walipelekwa Muhimbili hospitali walikoonyeshwa kichwa pamoja na `miliki.` Watuhumiwa hao Kibaya na mkewe Hadija Ali walimtambua kijana wao na kueleza kuwa alikuja Dar es Salaam Ijumaa, siku moja kabla ya tukio, akitokea Mtwara.
Hadija alidai walitengana na mzazi mwenzake (baba wa mtoto huyo) kwa miaka mingi na muda wote alikuwa akiishi Mtwara. Alisema Ramadhan alitoweka juzi jioni na alipigwa na butwaa baada ya kuona kuwa aliyekamatwa na kichwa cha Salome ni mwanae.
Mhudumu wa chumba cha maiti Muhimbili Bw. Mizome Gogo, alisema kichwa hicho kilifikishwa jana asubuhi na polisi na muda mfupi baadaye askari wa Stakishari waliwaletea kiwiliwili.
April 25, 2008
TICTS NA KARAMAGI
Mrs Pinda
Mambo ya Mswati hayooo
Mambo ya mila na utamaduni wa Bondeni kwa Mfalme Mswati, kila mwaka jamaa anakazi ya kuchagua mwali mpya kabisa wa kuoa.
King Mswati alianza kutawala Swaziland mwaka 1986 ana umri wa miaka 40 na mpaka sasa ana wake 13 na anauhakika wa kuoa mke 1 kila mwaka, je akifanikiwa kufikisha miaka 100 atakuwa na wake wangapi?
Wesley Snipes afungwa
Wesley Snipes amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwenye gereza la serikali (federal). Kisa hakulipa kodi aliyostahili kulipa! Denzel Washington alikuwa mahakamani akitoa shuhuda kuhusu jinsi Snipes alivyo mtu mwema. Pia Woody Harrelson alitoa shuhuda. Snipes mwenyewe alimwomba hakimu amwonee huruma! Lakini wapi! Jaji kampa kifungo cha juu kabisa miaka mitatu. Alisema awe mfano kwa wengine!
Kwa hisani ya Dada Chemi.
Neno la Leo
“To them God has chosen to make known among the Gentiles the glorious riches of this mystery, which is Christ in you, the hope of glory. We proclaim him, admonishing and teaching everyone with all wisdom, so that we may present everyone perfect in Christ.”- Colossians 1:27-28
April 24, 2008
mashujaa JWTZ warudi
Baadhi ya askari na maafisa wa jeshi waliokuwa wakishiriki katika oparesheni ya kumuondoa muasi wa kisiwa cha Anjouani Kanali Mohamed Bacar wakipita mbele ya mgeni Rasmi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa, Dk Hussein Mwinyi (hayupo pichani) wakati ya mapokezi ya askari hao jana jijini Dar es Salaam.
Mkonga wa MAWASILIANO
April 23, 2008
JK, JENS na Uzazi Salama
uzinduzi wa kampeni ya mkakati wa kupunguza vifo vya akina mama na watoto wa chini ya umri wa miaka mitano kuanzia mwaka 2008-2015.
( National Road Map Strategic Plan to Accelerate Reduction of Maternal, Newborn and Child Deaths in Tanzania 2008-2015 )
mkakati huo unaoendwshwa na Wizara ya afya na ustawi wa jamii ulizinduliwa jana jijini dar na rais jakaya kikwete kwa kushirikiana na waziri mkuu wa norway Jens Stoltenberg jijini ambae alikuwa katika ziara ya siku mbili nchini.
TBL NA WAJANE
Ofisa Tarafa ya Ilala, Bw. Suleiman Mwenda. akimkabidhi mmoja wa wanachama wa kikundi cha Wanawake Wajane cha The Good News Social Welfare Organisation (GOSOWO), Bibi Haruna Shamte cheti cha kuhitimu mafunzo ya kudarizi nguo pamoja na kutengeneza batiki yaliyogharamiwa hivi karibuni na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Wanaoshuhudia hafla hiyo iliyofanyika Vingunguti, Dar es Salaam jana, ambapo pia TBL iliwakabidhi msaada wa vyerehani vyenye thamani ya sh. milioni 4 ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Bi. Dorris Malulu (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa GOSOWO, Bw. Frank Mshahara.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Dorris Malulu akifurahia kuona kitenge cha batiki chenye jina la kampuni hiyo baada ya kukabidhiwa zawadi na Kikundi cha Wanawake Wajane cha The Good News Social Welfare Organisation (GOSOWO), baada ya kukipatia msaada wa vyerehani vya thamani ya sh. milioni 4 pamoja na kuwagharamia sh. milioni 1.5 za mafunzo ya kudarizi na kutengeneza nguo za batiki. Kulia ni Ofisa Tarafa ya Ilala, Bw. Suleiman Mwenda
April 22, 2008
April 21, 2008
KWA KINA BABA TUUUU!
Atimaye Chenge abwaga manyanga.
Rais akubali kujiuzulu kwa Chenge
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo April 20, 2008, amepokea barua kutoka kwa Waziri wa Miundo Mbinu, Mheshimiwa Andrew Chenge ya kujiuzulu wadhifa wake na Rais amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Rais ameuelezea uamuzi huo wa Mhe Chenge kama uamuzi wa busara kwa kutilia maanani mazingira ya sasa.
Katika barua yake kwa Rais, Mhe Chenge amesema kuwa pamoja na kwamba shutuma dhidi yake bado zinachunguzwa, mapenzi yake kwa nchi na chama chake, yamemsukuma kujiweka pembeni. Mhe Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi.
Mwisho
Imetolewa na Ikulu,
20th April, 2008
Buriani Braza Dito
April 19, 2008
NENO LA LEO
“But Christ has indeed been raised from the dead, the firstfruits of those who have fallen asleep. For since death came through a man, the resurrection of the dead comes also through a man. For as in Adam all die, so in Christ all will be made alive.”- 1 Corinthians 15:20-22
WAWAZA NINI HAWA????
ALA KUMBE!!!!! 3G
Subscribe to:
Posts (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Kumbe tuna utalii wa aina nyingi sana Tanzania!! mpaka huu nao? Waliingizia taifa dola ngapi? Women seeking beach boys ...
-
Prof Aloysius Mwessa Hnonoli ni Mbongo wa kwanza kuwa Mkurugenzi wa Muhimbili na Mkuu wa Chuo kikuu cha Tiba. Mstaafu huyu jana alitu...
-
Nimekuta ubishi paala fulani tena kwa watu naweza sema ni waelewa kiasi fulani maana wameenda shule na wengine wako katika fani, ati ile ho...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...
-
Shibe inapoua kuliko njaa Obesity kills more people than hunger Most of the world's populations live in countries where overweight a...
-
The Himba are an ethnic group of about 20,000 to 50,000 people living in northern Namibia, in the Kunene region (formerly K...
-
Mineral occurrence in Tanzania by TMAA UONGEZAJI WA PATO LA MTANZANIA Mheshimiwa Spika, 46. Lengo la Dir...
-
Kina dada wengi hivi sasa imekuwa ni kawaida kwenye kila shughuri hasa za usiku kukuta wamevaa nguo fupi, wengi wanasema ni fashion...
-
Ukumbi huko nyuma ya Minara miwili ukiwa ni wa mviringo. Eneoe kubwa la chai na ukaguzi pamoja na usajili kwa waalikwa. Sehemu za waa...