August 25, 2009

Mishahara ya Waheshimiwa JUU

SERIKALI imewaongezea mishahara viongozi wa kisiasa, majaji, wakuu wa mikoa na wilaya kuanzia Julai mwaka huu, huku jaji mkuu na spika wakiongezewa maradufu.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mshahara wa jaji mkuu na spika, ambao ni viongozi wa mihimili mikuu miwili ya nchi, umepanda kutoka Sh2,760,000 hadi Sh4,850,000 kuanzia mwezi Julai na ongezeko hilo ni sawa na asilimia 75.7

Mishahara ya wabunge,mawaziri na majaji imepandisha huku wa spika wa bunge ukipanda mara dufu. Kwa kifupi tu; Spika na Jaji mkuu Tshs 2,760,000/= mpaka 4,850,000/= Naibu spika Tshs 2,080,000/= mpaka 2,172,000/= Mbunge Tshs 1,840,000/= Mpaka 1,921,000/= jaji wa mahaka kuu tshs 2,160,000/= mpaka 3,645,000/= jaji Mahakam ya rufaa Tshs 2,310,000 mpaka 4,250,000/= Kwa hali hii kweli tutapona? Source:Mwananchi

Mazishi ya Wanafunzi 12 yanafanyika leo

Mazishi ya Wanafunzi 12 wa Shule ya Sekondari ya Idodo mkoani Iringa waliofariki kwa ajali mbaya ya moto Bwenini yanafanyoka leo hii hapo shuleni katika kaburi la pamoja. Wanafunzi waliokufa katika tukio hilo ambalo leo watazikwa kaburi moja ni ni Matrida Mtewele, Adelvina Kwama na Elizaberth Mtavila ambao walikuwa wanasoma kidato cha kwanza.Wengine ni Digna Nduguru, Chake Kuyaa, Seciliana John, Lazia Kihwele, Witness Mbilinyi na Stellah Mwigavilo waliokuwa wanasoma kidato cha pili.Pia wamo Falha Abdallah na Jesca Wissa waliokuwa kidato cha tatu na Maria Ndole wa kidato cha nne ambapo alisema kutokana na marehemu hao kuteketea kiasi cha kutotambulika, wametumia njia zingine kupata majina yao Imebidi miili hii izikwe kwa pamoja kutokana na zoezi la kutambua miili hiyo kuwa gumu kutoka na kuungua vibaya. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Picha za Mazishi zitafuta si muda. Picha kwa hisani ya Fransis Godwini

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...