Mama huyu aliyejitambulisha kwa majina kibao kama Judith, Rosemary, Mary nk. nadhani anastahili kupewa nishani ya ujasiri wa kitapeli kama ipo.
Mama huyu amekuwa akijitambulisha kama ni Afisa wa polisi wa cheo cha ASP, kikubwa zaidi ni ujasiri wake wa kwenda kujichanganya na polisi halisi na kuwatapeli mapesa kwa namna za udanganyifu tena Sentro Polisi, kafika mpaka kwa Kova mwenyewe kutaka kumtapeli lakini mzee mzima akastikuka.