August 14, 2009

Fidia ya mabomu ni balaa tupu.

MAANDALIZI ya kuwalipa fidia wakazi wa Mbagala walioathiriwa na mabomu yameingia dosari baada ya baadhi ya majina ya watu kukosekana kwenye orodha ya malipo, huku majina mengine yakitofautiana na namba za nyumba zilizoathiriwa.
Jumla ya Sh8.5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wakazi ambao nyumba zao ziliathiriwa na milipuko ya mabomu iliyotokea Aprili 29 kwenye ghala la silaha la kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) iliyo Mbagala na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 29. Fedha hizo zitatumika kulipa fidia nyumba 9,259 zilizoharibiwa na mabomu hayo na ambazo zilihakikiwa na serikali.
Lakini uchunguzi wa gazeti hili jana umebaini kuwa mchakato wa malipo hayo umeanza kuingia dosari baada ya watu kadhaa waliofika ofisi ya afisa mtendaji kata ya Mbagala Kuu, kugundua kuwa majina yao hayapo kwenye orodha iliyobandikwa ukutani na wengine kukuta tofauti ya majina na namba za nyumba.
Afisa mtendaji wa kata hiyo, Basil David alisema kuwa zaidi ya watu 50 waliofika ofisini kwake kuangalia majina yao, walikuta aidha yamekosewa au hayaendani na namba za nyumba zao. "Ni kweli zimejitokeza kasoro kwenye mchakato huu. Zipo namba za nyumba zilizokosewa na majina mengine yanatofautiana na namba za nyumba hizo,” alisema.
"Kutokana na hali hii tumeziagiza ofisi za serikali za mitaa kuorodhesha majina ya watu ambao majina yao au namba zao zimekosewa, ili ayapeleke kwa mkuu wa mkoa kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho kabla ya kuandaliwa kwa hundi za malipo," alisema.

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Dah!! Natumai SERIKALI ianweza kusimamia hata wale wanaoathiriwa na ajali mbalimbali kupata fidia zao. Tunaamini sheria za Tanzania ni kwa basi kuwa an BIMA ili kuwawezesha wanaomiliki kumudu gharama za dharura kama ajali.
Lakini nina wasiwasi kuwa michakato ya mwakani ndio imeanza na hakuna shaka kuwa malipo haya AMBAYO NI HAKI YA WAATHIRIKA yanatolewa kwa kuwa watu wanajitengenezea mazingira mazuri ya uchaguzi ujao.
Amesema yote Kakangu Kamala nami sina la kuongeza. Labda umfuate hapa (http://kamalaluta.blogspot.com/2009/08/maisha-bora-yashafika-hamyaoni.html)
JUMAPILI NJEMA KAKA

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...