YALE MAANDAMANO YALIYOPANGWA KUFANYWA NA VYAMA VYA UPINZANI DAR KUPINGA MATEKEO YA UCHAGUZI KENYA YALOMRUDUSHA RAIS KIBAKI MADARAKANI NA KULETE MACHAFUKO AMBAKO WATU ZAIDI 300 WAMEUWAWA HAYAKUFANYIKA TOKANA NA ULINZI MKALI ULIOWEKWA NA ASKARI JIJINI PAMOJA NA KUSISITIZA KUWA LAZIMA YANGEFANYIKA LEO.
Kulikuwa na ulinzi mkali toka alfajiri leo maeneo ya Manzese mahakama ya ndizi ambako yalipangwa kuanzia hadi stand ya mapikapu ambako ndipo viongozi hao wangehutubia.
Hali hii ilimlazimu mratibu kuwaita waandishi na kuongea nao uchochoroni maeneo ya Kinondoni badala ya Manzese, lakini mkutano huo ukafa ghafla mara baada ya walinzi wake kumjuza kuwa FFU walishafika eneo hilo nea kuingia mitini.