August 30, 2007

Moja ya Mambo niliyokutana nayo ni huduma za jamii, kina mama wanaua ndege wawili kwa jiwe moja ukija kutibiwa wachota na maji kabisa, pia umeme huku ni mgao mtindo mmoja kwani ni jenereta inayotumika ila kwa kuwa Rais wa Mkoa yupo haa ni masaa 24, hii yaitwa mgeni njoo mwenyeji apone.
Wadau niko Newala au "New Well" tegemeeni vituuzi toka huku mwisho kabisa mwa TZ karibu kabisa na mpaka wa Nchumbiji.

August 21, 2007

Ikulu yajibu, Lile sakata la kusaini mkataba aliloliibua Zitto Kabwe bado bichi, sasa Ikulu yakili kwamba Rais hakujua na kwamba si lazima ajue kama mwandishi wake anavyonukuliwa ktk gazeti la leo la Habari Leo.Nini hatima ya hayo yote???????? tusubiri kwani subira yavuta kheri, na pia Mhe JK anatarajiwa kuzuru huko mgodini wiki hii, Je nini kitajitokeza? na ukweli hasa ni upi? TIME WILL TELL!

August 20, 2007

MGOMO WANUKIA TAZARA Wafanyakazi wa TAZARA kupitia chama cha wafanyakazi wa reli leo wametangaza mgogoro na uongozi wakidai kulipwa mishahara yao kwa thamani ya dola ya marekani viwango vya miaka ya 90 ambayo ilikuwa 890 kwa Dola. kwa upande wa wenzao wa Zambia ahh kwa ni poa. mmmh jamani hivi sasa kwa walioughaibuni US$ 1 = TZS 1280, sasa hawa TAZARA dola kwa haipandi tu.

August 18, 2007

Mbowe, Slaa na Zitto wakipanga mikakati kabla ya Zitto Kuhutubia Umati uliojitokeza Jangwani.
Viongozi wa vyama vinne vya upinzani walikuwepo katika maandamano hayo yaliyoanzaia Ubungo Maji hadi viwanja vya Jangwani.
Nawaletea hali halisi ilivyokuwa leo mchana wakati wa maandamano ya kumpokea Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini baada ya kusimamishwa na bunge wiki iliyopita, Kuna mdau toka kanada kaomba nimpatie jinsi mambo yalivyokuwa, pata uondo.
CUF wakubali kurudi kwenye meza ya mazungumzo.
Hatimaye Chama cha Wanachi CUF kimeitika wito wa Rais Kikwete na kukubali kurudi ktk meza ya majadiliano juu ya Muafaka wa Zanzibar. Hii ni hatua ya kupongezwa na wote wanaoitakia mema nchin yetu.Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif akisoma tamko hilo. Mungu Ibariki Tanzania.

August 11, 2007

Maandamano ya wafanyakazi jijini Dar leo Asubui wanapinga nyongeza iliyotangazwa na serikali hivi karibuni ya kima cha chini cha 84,000/- kwa mwezi, wanataka kiwe 315,000.

August 7, 2007

Muhogo fresh kabisa huo, wenzetu mlio majuu mwaupata huu, je wale wa longi mwakumbuka enzi za primary za mihogo ya kukaanga, kachumbali kwa wingi na kushushia kwa togwa? aaaah we acha tu.
Kibao cha shule ya msingi Luis Jijini Dar, ikiwa hii ni hali ya jijini je kijijini kutakuwaje?

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...