"Hupati sura zetu hapa leo"
Mtuhumiwa wa ujambazi wa kutumia siraha na wizi wa magari maarufu kama white (kushoto) ambaye aliwahi sababishwa kuuwawa kwa makosa kwa mkurugenzi wa zamani wa usalama wa taifa Imran Kombe na polisi kwa kufananishwa naye pamoja na wenzie 5 wamefikishwa mahakamani leo hii kujibu tuhuma.
July 31, 2007
"Hupati sura zetu hapa leo"
Mtuhumiwa wa ujambazi wa kutumia siraha na wizi wa magari maarufu kama white (kushoto) ambaye aliwahi sababishwa kuuwawa kwa makosa kwa mkurugenzi wa zamani wa usalama wa taifa Imran Kombe na polisi kwa kufananishwa naye pamoja na wenzie 5 wamefikishwa mahakamani leo hii kujibu tuhuma.
A Five Star Shoe shine!
Mshapata sikia mobile shoe shiner?
Kijana Rajabu ameamua kujiajiri kwa kubuni mobile shoe shine, akiwa na kiti cha kivivu cha mteja na kigoda chake na vifaa vingine vyote katika baskeli yake yuko tayari kutoa huduma mahala popote wakati wowote. Hizi ni huduma zipatikanazo ktk Five star hotels
What is 500 million? is just a peanut!!
Aonekana kushangaa Wakili Maarufu, Mbunge na pia Mfanyabiashara Mkono wakti akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Benk M ambayo anasema ni ya kwake pamoja na wanahisa ambao hakuwataja, na kwamba haina uhusiano wowote na Rais Mstaafu Ben Mkapa, anadai kuwa kwa mtu wa rangi yake kuniliki ardhi katikati ya jiji ni ndoto, na kwamba ni ndoto pia kumiliki benki kwa mzawa kama yeye ndo maana ya makombora yanayorushwa kwake pitia magazeti fulani kwa lengo la kuhakikisha hafanikiwi.
Kwa madai yake ni kwamba toka 1991 ametaka kuanzisha benki maarufu kama Shilingi House lakini haikuwezekana.
Kama hayo yote ni kweli basi ni nani hao wanaorusiwa kumiliki ardhi katikati ya jiji? na wanamilikishwa na nani? na ni biashara gani mzawa katika nchi yake anapaswa kufanya? ni umachinga tu? na nani hasa hao wanaoweka vizingiti ivi na kwa faida au hasara ya nani? maswali ni mengi mno na sijui kama majibu yaweza patikana.
Tatizo liko wapi hasa?
July 21, 2007
Hii ni repoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Viwanda inayoonyesha jinsi wataalamu wetu wanavyokimbia nchi yao na kwenda kutafuta malisho mema.
Chonde Wabongo wenzetu mwendako huko oneni huruma na taifa lenu mwendako huko mkumbuke pia mlikotoka kwani kutafuta malisho mazuri zaidi ni vizuri lakini pia mchango wenu wakosekana nyumbani na ivyo kuchelewa kuendelea kwa taifa lenu ambalo pia limewaghalimia elimu zenu.
Tanzania suffers from brain drain: UN report
As a least developed country, Tanzania is also suffering from the brain drain that has backlashed at the development of these countries.The fact was pinpointed by the United Nations Conference on Trade and Development (UNCTAD) and the United Nations Information Center as they published the 2007 report on Least Developed Countries.The report, titled Knowledge, Technological Learning and Innovation for Development, said more qualified people from these poor countries are flocking to the developed world to seek better working conditions and better pays.The UN report revealed that 12 Least Developed Countries had lost over one third of their qualified professionals to emigration in recent years.One million out of 6.6 million people with tertiary level qualifications from developing countries were found to be working in developed countries, the report added.According to available information from the Tanzanian ministries, Tanzania has been losing such qualified professionals as doctors, nurses and teachers to emigration that leads them to South Africa or elsewhere for better pays.But there are no available statistics concerning the emigration
July 14, 2007
July 11, 2007
July 10, 2007
July 9, 2007
UDSM-FCM Almuni Association formed,,,
Viongozi wa Umoja wa waliosoma UDSM Kitivo cha Biashara na Uongozi, L-R David Shambwe Katibu Mmwenezi, Itandula Gambalagi Mkurugenzi, Nehemiah Kyando Mchechu M/kiti na Rebecca Muna wakiongea na wana habari juu ya tukio kubwa la wadau litakafanyika Trh 3/8/2007.
Iki ni Kitivo muhimu sana kwa taifa letu hasa kulingana na hali ya dunia inavyoenda hapa wanazalishwa watu muhimu ktk kukuza uchumi wetu, sio siri ukiangalia makampuni mengi kwa sasa yanapendelea kuajiri viongozi toka nchi jirani au hata ulaya kwa kazi ambazo wabongo wanaozalishwa hapa wanaweza kuzifanya,
ni wakati muafaka sasa kuwajengea wahitimu wetu kujiamini ktk uwezo wao kwamba wanaweza kufanya na zaidi ya hao wanaodhaniwa ni bora toka ng'ambo.
July 7, 2007
July 2, 2007
"Halloo!! shikamoo kaka, habari za leo, samahani nakuomba uje leo saa tano na nusu pale Ilala Boma CCM kutakuwa na............."
Hii ilikuwa ni sauti nyororo ya kubembeleza ambayo haikuwa ikiitaji utambulisho wowote uisikiapo mara upokeapo simu hasa kwa wanahabari wenzangu, ni sauti ya aina yake ambayo huwezi ifananisha na ingine au kuikosea na kama vile aliyekuwa anaitoa alikuwa akijua hivyo kwani ni aghalabu sana kusikia akijitambulisha.
Leo hii eti naambiwa sintoiskia tena abadani sauti hii? siamini!! eti ya kwamba imezimika ghafla kama kibatali au mshumaa uzimwao kwa hata kwa upope hafifu? hapana haiwezekani!! ati sasa waitwa marehemu? no haiwezekani!! mbona hukutupigia? mbona husitujulishe wadau wako kwa ile sauti yako nyororo ya kuwa watutoka? mbona husituage wadau wako Amina? Mbona ni mapema mno? yaani ndo kwanza jua lachomoza nawe waondoka? hukututendea haki washikadau.
Wanasema Mungu alikupenda zaidi? nakataa kuamini,, je ni kweli alikupenda mno kuliko vijana ulioapa kuwatetea na wakakuchagua kuwawakilisha? ni kweli alikupenda kuliko mwanao unayemwacha bila mama ktk umri mdogo hivi? Akili yangu ya kawaida yakataa kuamini, niwieni radhi kwa kutokuamini kwangu, pia nafahamu kazi ya Mungu haina makosa, lakini haa! sawa tutafanyaje!!
Imenichukua mda mrefu kuandika tanzia hii kwa kutoamini kwangu, nikidhani labda niko ktk ndoto ndefu na kwamba uenda nikiamka nitasikia tena sauti ile tamu ikinialika kwa ili au lile, sauti toka ktk sura ya tabasamu isiyo jua kununa, Lakini wapi siku zimepita na bado nasoma tanzia toka sehemu mbali mbali nami nalazimika kuamini japo kwa shingo upande kwamba ni kweli umetutoka Amina, waudaku walikufanya mradi, mamilion mengi wametengeneza kwa kupitia sura yako, kiasi najiuliza wapi watapata tena A.C mwingine? je ni nini wamekulipa A.C?
Yako mengi mno ya kuandika juu yako lakini itoshe kusema tu kwamba ulikuwa Kijana jasiri NA SHUJAA.
KWANGU NAAMINI UJAFA BADO BALI WAISHI. KWANI SHUJAA HUWA HAFI BALI ANAPUMZIKA TU.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576
Popular Posts
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
Nimekuta ubishi paala fulani tena kwa watu naweza sema ni waelewa kiasi fulani maana wameenda shule na wengine wako katika fani, ati ile ho...
-
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni-Kinondoni leo imeamua mazishi ya mwili wa Marehemu Paulo Goliama aliyefariki wiki iliyopita yafany...
-
At least 32 people have been killed in multiple explosions after an accident at a munitions dump in Tanzania's commercial capital, Dar e...
-
Kina dada wengi hivi sasa imekuwa ni kawaida kwenye kila shughuri hasa za usiku kukuta wamevaa nguo fupi, wengi wanasema ni fashion...
-
KASHFA YA RICHMOND YAPELEKEA Lowassa kujiuzuru, hii ina maana gani wapendwa? je na baraza zima limepigwa chini au niaje? Pichani juu ak...
-
Baada ya DCI na jeshi la polisi kwa ujumla kukiri kuwa vifaa walivyowekewa wabunge wa upinzani yaani Wilbrod Slaa na Dr Ali Tarib Ali kwam...










