August 9, 2011

Ujumbe kwa katuni na fede,

Mtembelee hapa

Serikali yachimbia mkwala makampuni ya mafuta..


Sehemu ya tamko la serikali lililotolewa na Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja kufuatia hoja binafsi ya Mbunge wa Bumbuli juu ya mgomo wa wauza mafuta uliodumu kwa takriban wiki sasa. 
1.                Mheshimiwa Spika, kufuatia hali iliyojitokeza, EWURA imetoa Compliance Order kwa makampuni manne ambayo ni BP, Engen, Oilcom na Camel Oil, ambapo wanatakiwa watekeleze hatua zifuatazo:
(i)            Mara moja wanatakiwa kuanza kutoa huduma katika maghala yao ikiwa ni pamoja na kuanza kuuza mafuta katika vituo vya rejareja ikiwemo vituo vilivyo chini ya miliki zao;
(ii)          Waache mara moja kitendo chochote kitakachosababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la Tanzania; na
(iii)        katika kipindi cha masaa 24 wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria dhidi yao kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya Mafuta pamoja na Sheria ya EWURA.

2.                Mheshimiwa Spika, baada ya kuisha kwa muda uliotolewa na EWURA, adhabu stahiki zitatolewa kwa wahusika ikiwa ni pamoja na kusitisha ama kufuta leseni.

3.                Mheshimiwa Spika, katika hali ya kawaida na kwa mujibu wa Sheria, mtu asiporidhika na maamuzi ya EWURA anapaswa kukata rufani katika Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal). Hatua hii haijafuatwa hadi sasa na Serikali ingeshauri kwamba masuala kama haya ni vema yakafuata taratibu za kisheria.

4.                Mheshimiwa Spika; naomba kuwasilisha.Msaada kwa wadau: COMPLIANCE ORDER yamaanisha nini kwa kimatumbi? 

London si shwari tena!

Violence erupted in Tottenham, North London, on Saturday after a peaceful protest against the fatal shooting of a 29-year-old local man, Mark Duggan, by police last week.

 It spread over the weekend to Enfield and Walthamstow in north London and Brixton in the south.

 Monday's violence started in Hackney after a man was stopped and searched by police but nothing was found.

 Scotland Yard say 225 people have been arrested as violence spreade across London.

 Businesses have been looted and set on fire in Camden, Clapham, Peckham, Ealing and Notting Hill.

 Violence has also erupted in Birmingham, where shops in the city centre have been attacked and an unmanned police station in the Handsworth area is on fire. 
Source: BBC


Miji hii na nchi ilikuwa salama kabisa mpaka siku ya Ijumaa kabla ya mauaji ya Mark Duggan na polisi, maandamano ya amani yaliibuka na kuenea maeneo mbalimbali na kupelekea vurugu, uporaji, uchomaji na uharibifu mkubwa wa mali katika miji ya London, Birmingham, na mingineyo


Chanzo cha yote hayo? ni mauaji ya mtu mmoja tu na polisi! 


Je twajifunza kitu gani hapa? Watawala na watawaliwa, Polisi na raia twapata somo gani toka UK kwa mama????

Bongo mambo mswano

Barrick yawakodia wabunge ndege kwenda Nyamongo

HATUA ya uongozi wa mgodi wa North Mara Barrick uliopo Nyamongo, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara kukodi ndege tatu ndogo kwa ajili ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kwenda mgodini hapo, imezua malalamiko huku baadhi ya wananchi wakidai kwamba kitendo hicho huenda kikashawishi mtizamo wa kamati hiyo.Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, James Lembeli jana ilifanya ziara ya siku moja mgodini Nyamongo ikitokea mjini Dodoma, ziara ambayo kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel ililenga kukagua utekelezaji wa maelekezo yake iliyoyatoa mwaka jana kuhusu athari za mazingira zilizosababisha baadhi ya wakazi wanaouzunguka kupata athari za kiafya.

Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambari Nyangwine alikuwa amealikwa kuambatana na kamati hiyo, lakini safari yake iliishia Uwanja wa Ndege wa Mjini Dodoma baada ya kubaini kwamba ndege husika zilikuwa zimekodiwa na kampuni ya Barrick.

"Kweli mimi nipo Dodoma, nimerudia pale Airport (Uwanja wa Ndege), siwezi kwenda kuwasaliti wananchi wangu wa Tarime, maana kama tunakwenda kuwakagua Barrick halafu tupande ndege za Barrick sidhani kama tutatenda haki," alisema Nyangwine alipozungumza na gazeti hili kwa simu na kuongeza:

"Barrick ndiyo (kampuni) inayotuhumiwa na wapiga kura wangu kwa kuwanyanyasa kwa kutowalipa baadhi yao fidia za mali zao hadi sasa mbali na kuhamishwa maeneo yao, kumekuwa na madhara makubwa kwa wananchi kutokana na matumizi ya maji yenye kemikali za sumu kutoka mgodini na maji hayo yanaingia Mto Tigite na kuleta madhara pia kwa wanyama, halafu nipande ndege yao! Haiwezekani."

Msimamo wa Nyangwine unafanana na ule ambao umewahi kutolewa na Lembeli katika moja ya vikao vya Bunge mwaka 2009, akisema kwamba amekataa kupanda ndege za kampuni hiyo kwani huweka gharama za safari hizo kama sehemu ya huduma inazotoa kwa jamii.

Lakini jana, Lembeli aliwaongoza wabunge wenzake kupanda ndege za Barrick ambazo zilitua Dodoma majira ya asubuhi na ujumbe wa baadhi ya wakuu wa kampuni hiyo, walioongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Deo Mwanyika kisha kuruka kuelekea Nyamongo.

"Kilichonishtua ni kumwona yule bwana Mwanyika na hapo nilimwuliza Mwenyekiti (Lembeli) kwamba hii siyo rushwa? Lakini yeye akanijibu kwamba siyo rushwa kwa sababu ni jambo ambalo limefanyika kwa uwazi, lakini mimi nikaona kwamba siwezi kwenda na kamati hiyo kwa sababu hapo hakuna uhuru wa kufanya kazi," alisema Nyangwine.

source: Mwananchi

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...