November 21, 2011

MEJE 30, MRITHI WA TSHALA MUANA ALIYEAMUA KUPANDA JUKWAANI MTUPU! 
Nilipoiona kwa mara ya kwanza picha ya mdada huyu akiwa mtupu jukwaani akikatika nilistuka kidogo, nikajiuluza inawezekanaje mtu apande kwenye stegi akitegemea umati wa watu utakuwepo asivae ile nguo ndogo na kisha afanye kusudi ili watu wajue kwamba hakuvaa chu**?

 Akili ya kwanza iliyonijia ni kuwa hii itakuwa vijiukumbi vyetu vya uswazi, kama uwanja wa fisi vile maana huko yanafanyika mengi kuliko ya kupanda stejini kuwaburudisha wanywaji wa Komoni, Wanzuki, Kimpumu nk, kuangalia vyema nikaona hapana, sivyo, hili gauni la bei kidogo, wale wa uswazi si rahisi kutinga hili, wenyewe wanaliita evening dress, ikabidi nitafiti zaidi.

 Niliweka post hapa kuoji inakuwaje wadada siku hizi wameamua kujidhalilisha hivi? ni maslahi au ni kitu gani? je wamelazimishwa na wamiliki wa bendi kwamba lazima mpande hivi ili kuvutia wateja? nikaoji tena kutakakumfahamu je huyu ni nani?

 Jibu la swali hilo ndilo lililoniacha kinywa wazi, ati huyu ni Mtarajiwa mrithi wa Miondoko ya Mutwashi toka kwa Tshala Muana! kweli huyu ndio anatarajiwa kuchukua mikoba ya Tshala Muana? sikuelewa haraka, nikaamua kufanya kautafiti kidogo.

 Nikaingia mitandaoni, nikakuta ni kweli, anajiita MEJE30, nikakuta naye ana album kadhaa mitandaoni, tena ni muimbaji mzuri tu, tena picha hili ilipigwa akiwa katika show Kampala 2009, sasa kwanini aliamua kuanika kitumbua chake hadharani akijua kuwa kuna kamera ambazo haziongopi? Je ni mbinu mpya aliyobuni ya kuvutia wateja? ili siku nyingine akija watu wajue wanapa mbili kwa moja? au pengine ilikuwa ni biashara ndani ya biashara?  

 Hiyo kama haitoshi nikakutana na kioja kingine, eti ametafuta mwanasheria na ata wafungulia mashtaka wapiga picha kwa kumvua Ch**, sasa hapa ikabidi niziangalia vyema picha zote kutoka katika show ile ambazo zimejaa mitandaoni, kwa utaalamu wangu wa kupiga picha na kuhariri kwenye duka la picha sijawai sikia kuwa kuna kamera inavua watu nguo, tena za ndani! hiki ni kioja kingine cha Malkia mtarajiwa wa Miondoko ya Mutwashi.

 Huyu ndie MEJE 30 Mrithi mtarajiwa wa Tshala Muana aliyeamua kupanda jukwaani bila nguo ya ndani ama kanguo kadogo na sasa analalama kuwa kamera zimemvua hako kanguo na kuanika kitumbua chake hadharani. Nabaki najiuliza, mbona Dada huyu ni mrembo, anasauti na kipaji pia kipo, kwanini afanye vile? ni nini anataka zaidi? 


1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ni ngumu kuamini ila inawezekana maana miaka hii hakuna kichowezekana.Il duh! Kaaazi kwelikweli..

Google+ Followers

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...