November 20, 2011

TAQWA YATEKETEZA WANAHISABATI 6 WA UDSM

Moses Mwale (Zambian) mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyesalimika  kati  ya kumi, watatu wamelaza Hospitali ya Ngara. 



  • Vifo vyafikia 18,
  • Wote watambuliwa,
  • Mtoto ahamishiwa Bugando


Ajali ya Basi la Taqwa na Lori la Azam iliyotokea jana Lusaunga wilaya ya Biharamulo imeteketeza wanafunzi 6  wa mwaka wa pili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa wakichukua Masters of Science in Mathematical Modelling, walikuwa wakienda Rwanda kwenye warsha ya Pure Mathematics.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Kozi hiyo yenye wanafunzi toka mataifa mbalimbali katika UDSM Dk Wilson Manera Charles  alisema wanafunzi hao ni kati ya kumi ambao waliteuliwa kuwakilisha katika warsha hiyo ya wanahisabati inayofanyika kila mwaka, wannne wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu, aliongeza kuwa waliokufa ni Mzambia mmoja, Malawi 2, Mganda 1 na Watanzania 2.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Biharamulo Dr Grasmus  Sebuyoya alisema vimeongezeka vifo 2 na kufikia jumla 18 na kuwa mpaka sasa maiti zote zimetambuliwa na nane kuchukuliwa na ndugu zao kwa maziko, mingine insaburi ndugu.

Pia aliongeza kuwa Mtoto mdogo wa kiumu anayekadiriwa kuwa na miaka miwili na nusu ambaye mama yake amefariki ajalini amehamishiwa hospitali ya Bugando Mwanza kwa matibabu zaidi.


Majeruhi walioko Biharamulo ni Tina Elisha, Rose Nula, Janet Kisanga, Moses Mwale, Joseph Bigilimana, Anicet Mrundi, Joseph Baltazary na Masalu Leonard.

Maiti zilizotambuliwa ni Abiba Juma, Faida Abdalah, Aziza Said, Andi Ibrahim, Chanda Congo, Nshaija Muganyizi na  Kasimu Dadi, wengine ni Erick Eliude, Chinuka Hamajata na Ndizeye Pili.  

No comments:

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...