May 13, 2008
JK on MWAFAKA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Sasa wakati wa kurudi mezani,
Rais aviambia CCM and CUF
Asema vyama hivyo vinakubaliana kimsingi na kuwa tofauti ni utekelezaji
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa baada ya vyama CCM na CUF kuwa vimeweka misimamo yao kuhusu Mwafaka hadharani, sasa ni wakati wa kurudi mezani kuendeleza majadiliano.
Rais pia amesema kuwa anaamini kuwa majadiliano hayo hatimaye yatazaa matunda mazuri kwa mustakabali wa Tanzania.
Rais ameyaeleza hayo kwa nyakati tofauti leo katika majadiliano na wageni ambao alikutana nao Ikulu, mjini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yake na Waziri wa Nchi wa Ufaransa anayeshughulikia Mahusiano ya Kimataifa na Nchi Zinazozungumza Kifaransa, Alain Joyandet, Rais ametumia muda kumwelezea mgeni historia ya majadiliano ya mwafaka na sababu za msingi zilizopelekea kuanzishwa kwa majadiliano hayo.
“Naamini mambo yatakwenda vizuri. Hatimaye tutafanikiwa katika hili la mazungumzo la Mwafaka,” amesema Rais Kikwete na kuongeza kuwa, kimsingi, CCM na CUF vinakubaliana kuhusu mambo ya kufanyika juu ya Mwafaka, na kuwa tofauti ni katika utekelezaji wa hayo yaliyokubaliwa.
“CCM wanataka suala hilo kubwa la msingi liamuliwe moja kwa moja na wananchi. CUF wao wanataka wanasiasa kuamua kwa niaba ya wananchi. Hivyo, tofauti iko katika namna ya kutekeleza yaliyokubaliwa,” amesema.
Rais pia amemweleza Waziri huyo kuwa uamuzi wa kuwa na Serikali Shirikishi katika Zanzibar ulichukuliwa miaka saba iliyopita, mwaka 2001, wakati wa majadiliano yaliyozaa Mwafaka wa Kwanza kati ya CCM na CUF.
Rais amesisitiza kuwa uamuzi wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha karibu cha Butiama, Musoma haukubadilisha makubaliano ya msingi kati ya vyama hivyo. “Kilichofanyika ni CCM kuongeza mapendekezo mawili ili nayo yajadiliwe na timu za vyama hivyo viwili.”
Amesema kuwa pendekezo moja ni kuwashirikisha wananchi kuamua utekelezaji wa mwafaka kati ya vyama hivyo, na la pili ni kuweka utaratibu wa ukomo wa utekelezaji (sunset clause) wa mwafaka huo.
Amesema “mwafaka unalenga kuitoa Zanzibar katika matatizo ya sasa ya kisiasa. Hauwezi kuwa utaratibu wa daima dumu na kuwa ukifika wakati kuwa mfumo huo wa utawala wa kisiasa umekamilisha kazi yake, basi unaweza kuondolewa na Zanzibar ikarudi katika ushindani wa kawaida wa kisiasa.”
Amesema kuwa hivyo ndivyo ilivyokuwa katika nchi za Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), na sasa katika Kenya.
Katika mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Adam Woods, Rais amesisitiza kuwa bado iko nafasi ya kuokoa mazungumzo hayo ya Mwafaka.
“Wote sasa wamezungumza kiasi cha kutosha. Sasa ni wakati wa kukaa chini na kuendelea na mazungumzo,” Rais amemweleza Balozi huyo.
Amesisitiza: “Maamuzi ya CCM hajabadilisha jambo lolote la msingi katika makubaliano ya Mwafaka –no deviation on fundamental agreement – Tulichofanya sisi ni kuongeza jambo la kuwashirikisha wananchi na kuwataka wanaoendesha majadiliano kulifikiria na hili.”
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Mei, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Arts n' Photo sildes
"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION
Future Stars!
Some of published work
RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576
Popular Posts
-
Chakula chapikwa karibu kabisa na vyoo vilivyo kulia. KABLA YA KUINGIA CAFETERIA WAKUTANA NA VITUUZI MLANGONI. BAFUNI NAKO NI BALAA. NA H...
-
WADAU NADHANI SI VIBAYA SIKU MOJA MOJA TUKAPANUA MAWAZO KIDOGO NDO NAMNA YA KUELIMISHANA KUPITIA NJIA HII. HIKI ni kijiji kipo hapa bo...
-
At least 32 people have been killed in multiple explosions after an accident at a munitions dump in Tanzania's commercial capital, Dar e...
-
Kina dada wengi hivi sasa imekuwa ni kawaida kwenye kila shughuri hasa za usiku kukuta wamevaa nguo fupi, wengi wanasema ni fashion...
-
Ukumbi huko nyuma ya Minara miwili ukiwa ni wa mviringo. Eneoe kubwa la chai na ukaguzi pamoja na usajili kwa waalikwa. Sehemu za waa...
-
KASHFA YA RICHMOND YAPELEKEA Lowassa kujiuzuru, hii ina maana gani wapendwa? je na baraza zima limepigwa chini au niaje? Pichani juu ak...
-
Nimekuta ubishi paala fulani tena kwa watu naweza sema ni waelewa kiasi fulani maana wameenda shule na wengine wako katika fani, ati ile ho...
-
Bila shaka wapo ambao kwa kuona picha tu udenda wawadondoka hapo walipo, msihofu tembeleeni sabasaba kule karibu na banda la Heineken kwa w...
-
Hivi Daktari Bingwa ndo wale wanaoitwa SPESHALISTI? je waweza bashiri hii ni wapi ambapo walipa buku tu kumwona mtaalamu?
No comments:
Post a Comment