February 16, 2009

LILIYEYUKAJE HILI DUBWANA??????????

Mgonjwa wa saratani akipata huduma Ocean Road Cancer Insititute (ORCI) asubuhi leo hii baada ya kununuliwa kwa vifaa vilivyokuwa vimeibwa yapata wiki mbili zilizopita.
Hii ndo aina ya mashine zilizoibwa yapata wiki mbili zilizopita pale ORCI zaitwa Control Console, zimenunuliwa tena mpya kwa gharama ya Dola za US 22,000/- na hivyo wagonjwa wameanza tena leo kupata huduma baada ya kusimama kwa muda wote huo.

Tutafakali. Wadau niliposikia kuibwa/kutoweka au kuyeyuka kama barafu au mafuta kikaangoni isia zangu zilinituma kuwa hako kajifaa katakuwa ni kadogo tu pengine ukubwa wa simu ya kiganjani labda, haikunijia akili kuwa ni lidubwana likubwa kiasi hicho (yaani hiyo hizo kama screen mbili za kompyuta nyeupe na nyeusi mara mbili) ukweli sikuamini macho yangu nilivyonyeshwa na wahusika kuwa zilizoibwa ni kama hizi hapa!!!!!!!!!!

Cha kushangaza zaidi ni kuwa aina hii ya mashine kwa Afrika Mashariki na kati ni Tanzania tu ndo tunayo na huu ulikuwa ni msaaada wa shirika la nguvu za atomic la dunia na ilizinduliwa na JK Mwaka jana Mei tu, yaani hata mwaka mmoja bado toka tusaidiwe mashine hii.

Sitaki kutia chumvi wala kumnyooshea mtu kidole kwani polisi inaendelea na uchunguzi wake na sijui lini watamaliza, lakini nna maswali machache wadau ambayo naomba tushauriane kwa wema tu,

1. Mijidubwana mikubwa kama hii inawezawezaje kuyeyuka ka barafu hapo mezani pasi kuonekana na awaye yeyote????

2. Ikiwa ni Tz tu tunayo na tena hapo tu ORCI katika EAC and C, je yu wapi mteja au mseti ilikopelekwa hiyo mimashine? au inamatumizi gani mengine mbali na kutibu saratani??????

3. Hivi awaye yote alokuja chukua na kutoweka na mashine za namna hiyo au ukubwa huo alizibebabebaje? kwa lambo?? au katia mfukoni tu??????

4. Utaifa uko wapi kwa Watanzania wa leo jamani????? unapoiba kifaa kinachookoa maisha ya nduguzo, rafikizo, kaka na dadazo au mama na baba yako je uitwe nani????????? muuaji????? sijui ila yupo ajuaye.

5 comments:

Faustine said...

Waswahili siku wanasema kila mtu anatengeneza mazingara ya EPA pale alipo.
Hi ni wizi wa ndani na hakuna aliyechukuliwa hatua kwa uzembe au kutia taifa hasara.
Mdau
Faustine

Anonymous said...

Inasikitisha sana, sidhani kama ni mwizi wa nje aliingia hapo hospitalini na kujua mazingira yote ya hospitali na kunyakua hiyo mashine huyu atakuwa ni daktari tu mwenye njaa, akiwepo zamu aliwakeep wenzie busy afu akatorosha mashine ya kutibu watanzania wengiwao wakiwa maskini, kwa sababu mafisadi wanaweza kwenda kutibiwa india ye akaona bora awakomeshe maskini, ila ajue Mwenyezi Mungu amemuona na akipatikana anastahili kifungo cha maisha. Na aieleze jamii lengo lake hasa la kuiba hiyo mashine hata kama alitaka kuanzisha hospitali ya binafsi hii ni hatri sana jamani.., mtaani kumekuwa na madaktari wengi wanaotibu watu majumbani mwao siju serikali inalichukuliaje hili?

(Mzawa)

Anonymous said...

WIZI MTUPU......

Jiang said...

WIZI MTUPU
NAOMBA HILI TULIPIGIE KELELE HADI KIELEWEKE, WANATUFANYA WATU KARBU 50M WAJINGA? SAWA WAO MADOKTA NA MAPROF WA VITU IVYO NA WENGINE HATA DARASA LA SABA HATUKULIONA ILA THIS IS TOOO MUCH.
NAOMBA MTU AELEZEE TUELEWE!

Anonymous said...

Poleni sana Watanzania wenzangu hayo ni maisha ya Bongo chochote kile kinawezekanavyo .Hata hukienda Ikulu hukitaka TV ya JK Hutaletewa mradi huwe na kitu kidogo siyo.Watu wote wananjaa na hawana Uzalendo na nchi yao kila mtu mission hata Mapolice wanakula deal siyo .Aibu tupu but that real life for Wabongo.

Google+ Followers

There was an error in this gadget
There was an error in this gadget

Arts n' Photo sildes

"SILENT VOICES" PHOTO EXHIBITION

Future Stars!

Some of published work

RIGHT TO BE RICH

RIGHT TO BE RICH
The ownership of money and property comes as a result of doing things in a certain way, and those who do things in this certain way — whether on purpose or accidentally — get rich, while those who do not do things in this certain way — no matter how hard they work or how able they are — remain poor. WDW Do things in RIGHT way now, but how? Call: +255716927070/+255784475576

Popular Posts

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...